Kosa la kumlilia marehemu ndio chanzo cha kuendelea kufa

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Yesu alipokuwa akipita zake alikuta watu wakilia na kuomboleza, Yesu akawaambia kwanini mnalia? Wakamjibu binti yetu kafariki; Yesu akawajibu msilie; Binti yenu yu Hai amelala tu; akamwamuru binti ainuke; Binti akaamuka! Ukitafakari sana juu ya kumlilia marehemu ni sawa na kujisumbua bure, haisaidii chochote kwa Mungu.

Kumlilia marehemu ni zaidi ya kumkosoa Mungu! Mungu ndiye aliyeamua kuleta kiumbe duniani; na ndiye anayekitoa: Inatupasa tufike mahali kama mtoto akizaliwa tunasherekea, vivyo hivyo mtu anapofariki yatupasa kusherekea; Ifike wakati uendapo Msibani sema unaenda kwenye sherehe ya kuhifadhi mwili wa fulani.

Bibilia inasisitiza kushukuru. "SHUKURUNI KWA KILA JAMBO" Tunakumbuka kushukuru pekee tunapozaa, ila ndugu yetu anapotutoka hatushukuru.
NINAIMANI ENDAPO TUKIACHA KULIA NA KUSONONEKA MSIBANI; Mungu atagundua ukomavu wa imani zetu:

Huenda ndiyo siri ya kifo ilipo jificha ni hapo kwenye kilio; unapolia maanake na wewe unahesabiwa KIFO! Hadi hapo kizazi hiki kinacholia kitakapo koma.
"KAZI YA BWANA HAINA MAKOSA " Tuishi Kwa kutendea haki kauli mbiu hiyo.

NOTE;
KWA WASIYO AMINI UWEPO WA MUNGU; Jadilini huu uzi kwa kuamini Mungu yupo. (discuss Assuming God is present)

KARIBUNI
 
Are you serious? Hata yesu alimlilia rafiki yake Lazaro, hata alipokua msalaban alilia, hata kabla ya kufa alitoka had jasho la damu na aliomba ikiwezekana kikombe (kifo ) hicho kimuepuke , sasa wewe leo unatuambia kifo sherehe? Labda kwa misingi ya kabila lenu sio biblia dats y hata Mungu aliwaambia Adam na eva wakila tunda watakufa which means ni adhabu sio tuzo, hatuwezi kukifanyia Sheree.

Halaf eti ndomana tunakufa kwajili ya kulia, are u for real? Biblia gan unatumia? Coz biblia imeweka waz kila nafsi itaonja umaut. Hebu wewe usie lia tuone utavyoishi milele.

Kulia kwenye msiba inategemea na venye umeguswa na tukio bt wengine machoz yapo kwenye kisigino so hata akiwa na uchungu huon choz bt analia.
 
Aiseee sielew unatumia biblia gani

Kumbuka Yesu alimlilia lazaro.
Aliomba kikombe kimuepuke...alisali sana kuomba mateso yasimpate ..

Kulia au huzuni pind unavyofiwa sio dhambi mkuu.
 
Biblia ukiisoma kwa mihemko jumlisha na maisha magumu ni hatari....soma biblia kwa tafakari ya kina....mbona hata Yesu mwenyewe alilia machozi??? Yoh. 11:35-36
 
Eti hata asiyeamini Mungu ajadili kwa kuamini Mungu yupo, unazungumzia Mungu yupi?, wahindi wanaamini Mungu wao ni ng'ombe, baadhi ya watu wanaamini mlima fulani unaotoa volcano ndiyo Mungu wao, hao wanaosali makanisani na misikitini ndiyo wanaopora ushindi wa ukawa hadharani bila ya aibu na Mungu wao anawaangalia tu
 
Ahahaaaaa...hawa wa misikitini na makanisan ndio wanafki hasa mkuu...ingawa na mm nasali kanisan
 
Mkuu sio wote wanaosali kanisani na msikitini ni wanafiki nazungumzia baadhi yao kama wakina jecha, mahiga, ndalichako na kadhalika
 
Are you serious? Hata yesu alimlilia rafiki yake Lazaro, hata alipokua msalaban alilia, hata kabla ya kufa alitoka had jasho la damu na aliomba ikiwezekana kikombe (kifo ) hicho kimuepuke , sasa wewe leo unatuambia kifo sherehe? Labda kwa misingi ya kabila lenu sio biblia dats y hata Mungu aliwaambia Adam na eva wakila tunda watakufa which means ni adhabu sio tuzo, hatuwezi kukifanyia Sheree.

Halaf eti ndomana tunakufa kwajili ya kulia, are u for real? Biblia gan unatumia? Coz biblia imeweka waz kila nafsi itaonja umaut. Hebu wewe usie lia tuone utavyoishi milele.

Kulia kwenye msiba inategemea na venye umeguswa na tukio bt wengine machoz yapo kwenye kisigino so hata akiwa na uchungu huon choz bt analia.
Kama bibilia imeandika "kila nafsi itaonja mauti" Sasa kitu gani kinakufanya ULIE wakati unajuwa
Are you serious? Hata yesu alimlilia rafiki yake Lazaro, hata alipokua msalaban alilia, hata kabla ya kufa alitoka had jasho la damu na aliomba ikiwezekana kikombe (kifo ) hicho kimuepuke , sasa wewe leo unatuambia kifo sherehe? Labda kwa misingi ya kabila lenu sio biblia dats y hata Mungu aliwaambia Adam na eva wakila tunda watakufa which means ni adhabu sio tuzo, hatuwezi kukifanyia Sheree.

Halaf eti ndomana tunakufa kwajili ya kulia, are u for real? Biblia gan unatumia? Coz biblia imeweka waz kila nafsi itaonja umaut. Hebu wewe usie lia tuone utavyoishi milele.

Kulia kwenye msiba inategemea na venye umeguswa na tukio bt wengine machoz yapo kwenye kisigino so hata akiwa na uchungu huon choz bt analia.
Sasa kama bibilia IPO wazi kwamba kila nafsi itaonja Mauti; KILIO CHA NINI
 
Mungu mwenyewe kasema; KUISHI NI KRISTU; KIFO NI FAIDA.
 
dmkali
Kulia ni kosa..?
Halafu mbona unapinga unachokiamini.?
maana kwa mujibu wa biblia adam na eva kula lile tunda ndio kulipelekea watu kufa so are you against it or...?
 
Back
Top Bottom