Kosa la karne kwa CCM ni kujitenga na hoja ya Katiba na kuwaacha upinzani watambe nayo

Evarist Chahali

JF-Expert Member
Dec 12, 2007
1,004
2,000
Kwasababu bado sina chama cha siasa, nataka kuwashauri viongozi wakuu wa CCM. 'Msijitenge na hoja ya katiba na kuwaachia upinzani pekee, mnafanya kosa kubwa'

Nimeangalia trend mpaka sasa huko mitandaoni, nimesikitika kuona kwamba kila mwana CCM ambaye ataongea kuhusu katiba mpya, basi ataongelea kwa kusema kwamba nchi haihitaji katiba mpya kwa sasa. Hili ni kosa kubwa sana, nadhani ambacho CCM wangepaswa kufanya kwa sasa ni kufanya utafiti wa kisayansi wa kujiridhisha ni kwa asilimia ngapi wananchi milioni 60 wana kiu ya katiba mpya.

Baada ya kujiridhisha ndipo haswa wanatakiwa kuja na hoja ama za kupinga katiba mpya ama na wao wajiingize moja kwa moja kwenye ajenda ya katiba mpya.

Kufuatia miaka mitano ya 'stress' ni wazi kwamba upepo uliopo sasahivi ni upepo wa mabadiliko, na wala CCM wasidhani kwamba upepo huu wakudai mabadiliko ni hoja ya CHADEMA, la hasha, kuna wana CCM wengi tu sasahivi nao wanahisi kwamba kuna mabadiliko yanahitajika kufanyika.

Sasa ukiwa kwenye hali hiyo ya uchu wa watu kutaka kubadilika, kama chama cha siasa na wewe itabidi uone namna gani uta flow na mawimbi, na hii itakuwa na matokeo makubwa sana kwenye umaarufu wa chama cha mapinduzi chenyewe, hatari kubwa na ya mapema ya CCM ni kuanza kuonesha eti wanapinga katiba mpya.

Ningeshauri uongozi mpya wa CCM waone namna ya wao kuikumbatia hii ajenda ya kuwa na katiba mpya, wasiwaachie upinzani peke yao, kama kweli wanamipango ya CCM kuendelea kuonekana kwenye uso wa Tanzania miaka 20 inayokuja. Hakuna namna CCM itataka kupinga katiba mpya na kuendelea kutawala kwa miaka 20 inayokuja, sidhani kama taifa hili la vijana wenye uchu wa mabadiliko wataacha hichi kitu kitokee.

Sidhani kama ndani ya miaka 10 hadi 20 ijayo ambapo nchi itakuwa na watu kati ya milioni 70 au 80, asilimia zaidi ya 65% wakiwa vijana ambao wengi watakuwa wamesoma na hawana ajira, hapo hapo kiwango cha umasikini bado ni kikubwa, halafu hapo hapo nchi bado inaishi bila katiba mpya, hichi kitu kitakuwa kigumu sana kuwezekana, na kuna watu huwa wanafanya analysis ya kutabiri matukio ya miongo miwili ijayo, ni wazi kwamba kwa dunia ya sasa inavokwenda, CCM hawatakiwi kabisa kufikiria kwamba wataendelea ku exist salama bila nchi kuwa na sheria na katiba ya kueleweka. Na itakuwa ngumu sana ku guarantee Tanzania isiyomwaga damu kama hakuta kuwa na katiba na sheria za kueleweka ndani ya miaka 10 mpaka 20 inayokuja.

Kiwango cha subira na uvumilivi sidhani kama kitakuwa kwa watanzania walio wengi.

So mi nachukulia huu utawala wa mama kukichukulia hichi kipindi cha utawala wake kama ni cha muhimu na mpito kwa mustakabali wa utulivu wa nchi ya Tanzania kwa miaka 10 na 20 inayokuja. Ni kipindi ambacho ni critical sana

So kwa mtizamo wangu, katiba mpya ni damu na moyo wa CCM kama kweli itataka kusalia madarakani.
Moja ya mapungufu makubwa ya Watanzania ni usahaulifu. Huyu anayesema "kiwango cha subira na uvumilivu sidhani kama kitakuwa kwa Watanzania wengi" ameshasahau kuwa porojo za "tunataka katiba mpya" hazijaanza Machi 19 baada ya Mama Samia kuapishwa. Zilianza mwaka 1992 pengine wakati huo mtoa mada alikuwa hajazaliwa.

Na kati ya wakati huo na sasa, yamejiri mambo mengi ambayo kwa wenzetu wanaojielewa, basi huenda muda huu CCM ingekuwa historia. Kwa kukumbusha tu, utawala wa Mkapa ulitawaliwa na ubabe uliopelekea vifo vya Wazanzibari kadhaa Januari 2001. Lakini Mkapa alimaliza muda wake salama. Akaja Jk, ambaye aliigeuza Tanzania kuwa shamba la bibi, ufisadi ukawa kama umehalalishwa na Katiba. Nae akatawala hadi muda wake ulipoisha 2015.

Na ilipotokea fursa bora kabisa kwa Upinzani kuing'oa CCM mwaka 2015 kwa kuzingatia rekodi ya kutisha ya ufisadi wa Jk na CCM yake, Upinzani ukaamua kumpokea na kumsimamisha Lowassa kuwa mgombea wake wa urais, licha ya upinzani huohuo kumtangaza tangu 2006 kuwa ni papa la ufisadi.

Na 2015 hadi Machi 2021, Tanzania ilipitishwa kwenye tanuru ka moto mkali chini ya utawala wa Magufuli. Na laiti korona isingemwondoa, angeendelea kutawala hadi aamue kuachia madaraka.

Sasa hizi "hasira mpya" na "uvumilivu una mwisho" vinatoka wapi? Usahaulifu au kujimwambafai ilhali uwezo pekee uliopo ni kwenye kufuatilia ubuyu?

Yes Katiba mpya ni muhimu lakini you guys need to be realistic. Itapatikana kwa matakwa ya Mama Samia na si kwa porojo za mtandaoni. I'm not saying kwamba Katiba inahitaji ridhaa ya Rais bali nakumbusha tu hali halisi ilivyo.
 
dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
678
1,000
S
Kwasababu bado sina chama cha siasa, nataka kuwashauri viongozi wakuu wa CCM. 'Msijitenge na hoja ya katiba na kuwaachia upinzani pekee, mnafanya kosa kubwa'

Nimeangalia trend mpaka sasa huko mitandaoni, nimesikitika kuona kwamba kila mwana CCM ambaye ataongea kuhusu katiba mpya, basi ataongelea kwa kusema kwamba nchi haihitaji katiba mpya kwa sasa. Hili ni kosa kubwa sana, nadhani ambacho CCM wangepaswa kufanya kwa sasa ni kufanya utafiti wa kisayansi wa kujiridhisha ni kwa asilimia ngapi wananchi milioni 60 wana kiu ya katiba mpya.

Baada ya kujiridhisha ndipo haswa wanatakiwa kuja na hoja ama za kupinga katiba mpya ama na wao wajiingize moja kwa moja kwenye ajenda ya katiba mpya.

Kufuatia miaka mitano ya 'stress' ni wazi kwamba upepo uliopo sasahivi ni upepo wa mabadiliko, na wala CCM wasidhani kwamba upepo huu wakudai mabadiliko ni hoja ya CHADEMA, la hasha, kuna wana CCM wengi tu sasahivi nao wanahisi kwamba kuna mabadiliko yanahitajika kufanyika.

Sasa ukiwa kwenye hali hiyo ya uchu wa watu kutaka kubadilika, kama chama cha siasa na wewe itabidi uone namna gani uta flow na mawimbi, na hii itakuwa na matokeo makubwa sana kwenye umaarufu wa chama cha mapinduzi chenyewe, hatari kubwa na ya mapema ya CCM ni kuanza kuonesha eti wanapinga katiba mpya.

Ningeshauri uongozi mpya wa CCM waone namna ya wao kuikumbatia hii ajenda ya kuwa na katiba mpya, wasiwaachie upinzani peke yao, kama kweli wanamipango ya CCM kuendelea kuonekana kwenye uso wa Tanzania miaka 20 inayokuja. Hakuna namna CCM itataka kupinga katiba mpya na kuendelea kutawala kwa miaka 20 inayokuja, sidhani kama taifa hili la vijana wenye uchu wa mabadiliko wataacha hichi kitu kitokee.

Sidhani kama ndani ya miaka 10 hadi 20 ijayo ambapo nchi itakuwa na watu kati ya milioni 70 au 80, asilimia zaidi ya 65% wakiwa vijana ambao wengi watakuwa wamesoma na hawana ajira, hapo hapo kiwango cha umasikini bado ni kikubwa, halafu hapo hapo nchi bado inaishi bila katiba mpya, hichi kitu kitakuwa kigumu sana kuwezekana, na kama kuna watu huwa wanafanya analysis ya kutabiri matukio ya miongo miwili ijayo, ni wazi kwamba kwa dunia ya sasa inavokwenda, CCM hawatakiwi kabisa kufikiria kwamba wataendelea ku exist salama bila nchi kuwa na sheria na katiba ya kueleweka.

Na itakuwa ngumu sana ku guarantee Tanzania isiyomwaga damu kama hakuta kuwa na katiba na sheria za kueleweka ndani ya miaka 10 mpaka 20 inayokuja maana ni kipindi ambacho kiwango cha subira na uvumilivi kwa watanzania walio wengi kitakuwa kimefika ukomo.

So mi nachukulia huu utawala wa mama kuwa ni kipindi cha muhimu na cha mpito kwa mustakabali wa utulivu wa nchi ya Tanzania kwa miaka 10 na 20 inayokuja. Hili suala lisichukuliwe ki uwepesi, watanzania wengi hawapo tayari kwa 'another Magufuli' ndo mana hili vugu vugu la katiba mpya ni tofauti na vugu vugu la katiba kwenye enzi ya Kikwete. Completely different atmosphere.

So kwa mtizamo wangu, katiba mpya ni damu na moyo wa CCM kama kweli itataka kusalia madarakani.
Sidhani kama CCM haitaki katiba mpya au katiba bora suala hapa ni muda mwafaka wa kutekeleza hilo. Ni wazi kuitaka katiba mpya na lini wazo hilo linahitaji kutekelezwa kwa mmaana ya TIMING ni jambo lingine. Utekelezaji wa hatua hii unahitaji umakini ili kuepuka madhara, maandalizi na kutathmini matokeo ya utekelezaji ni muhimu sana. Jambo lolote lenye sura ya kitaifa kugawanyika" if mishandled" linahitaji umakini mkubwa. Nashauri Rais asikurupuke ili mradi upande wa pili unashinikiza. Dhamana ya usalama wa taifa na utulivu wake uko mikononi mwa Ccm.
 
Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
7,233
2,000
Tena kama kuna kipindi kizuri cha CCM ku pioneer katiba mpya, ni kipindi hichi ambacho Rais Mama Samia ameonekana kuungwa mkono na watanzania wengi, hii ndo ilikuwa point ya CCM ku win popularity ambayo its obvious imepotea lakini naona wao wenyewe wanajirudisha kwenye tope la kwamba CCM ni 'Doctrine na Ideology' ambayo lazima ilindwe.. kosa kubwa
Hapa umemaliza kila kitu.
Huu ndio ukweli halisi.
Mama alipata Golden chance in political platform lakini akaamua kuichezea nafasi vibaya. Ipo siku itajuta na kuikumbuka hiyo nafasi. Huu ndio ulikuwa wakati bora zaidi kwa mama Samia kuvuna point zote tatu za kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa kuifungulia nchi kutoka kwenye gereza la utumwa wa utawala wa kimabavu kwa kuwapa katiba mpya.

Sasa amewapa wapinzani agenda nzuri ya kuipinga serikali yake, wapinzani wanaibeba agenda ya Katiba mpya nzima nzima na kwenda kuiuza kwa wananchi, na wananchi watainunua kwa gharama yoyote.

Mama ajiandae kukosa usingizi.
Atapata tabu sana.
 
mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
14,125
2,000
Waikubali kwanza halafu waone kitakacho wakuta kwenye uchaguzi mkuu wa 2025! Yaani wakubali Katiba Mpya, na yenye Tume Huru ya Uchaguzi ndani yake!

Hakuna polisi wa kuingiza masanduku ya kura bandia, au kutimua mbio na kura za wapinzani!! Hakuna uvccm wanaoruhusiwa kuwatisha wapiga kura, huku wakijifanya eti ni tiss!!

Kudadek, saa mbili tu asubuhi!! Ccm chali!!!
Tate Mkuu nakusalimia

Katiba mpya ni kwa maslahi ya nchi sio ya Chama
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
9,783
2,000
Tate Mkuu nakusalimia

Katiba mpya ni kwa maslahi ya nchi sio ya Chama
Ila kwa bahati mbaya hii katiba ya mwaka 1977, iliandaliwa kwa ajili ya kunufaisha vitu viwili tu; ccm na makada wake, na Mwenyekiti/Rais kutoka ccm! Full stop.

Wengine tuliobaki ni maumivu tu. Hili halikubaliki hata kidogo rafiki yangu mama D
 
4 7mbatizaji

JF-Expert Member
Dec 8, 2019
2,923
2,000
Kwasababu bado sina chama cha siasa, nataka kuwashauri viongozi wakuu wa CCM. 'Msijitenge na hoja ya katiba na kuwaachia upinzani pekee, mnafanya kosa kubwa'

Nimeangalia trend mpaka sasa huko mitandaoni, nimesikitika kuona kwamba kila mwana CCM ambaye ataongea kuhusu katiba mpya, basi ataongelea kwa kusema kwamba nchi haihitaji katiba mpya kwa sasa. Hili ni kosa kubwa sana, nadhani ambacho CCM wangepaswa kufanya kwa sasa ni kufanya utafiti wa kisayansi wa kujiridhisha ni kwa asilimia ngapi wananchi milioni 60 wana kiu ya katiba mpya.

Baada ya kujiridhisha ndipo haswa wanatakiwa kuja na hoja ama za kupinga katiba mpya ama na wao wajiingize moja kwa moja kwenye ajenda ya katiba mpya.

Kufuatia miaka mitano ya 'stress' ni wazi kwamba upepo uliopo sasahivi ni upepo wa mabadiliko, na wala CCM wasidhani kwamba upepo huu wakudai mabadiliko ni hoja ya CHADEMA, la hasha, kuna wana CCM wengi tu sasahivi nao wanahisi kwamba kuna mabadiliko yanahitajika kufanyika.

Sasa ukiwa kwenye hali hiyo ya uchu wa watu kutaka kubadilika, kama chama cha siasa na wewe itabidi uone namna gani uta flow na mawimbi, na hii itakuwa na matokeo makubwa sana kwenye umaarufu wa chama cha mapinduzi chenyewe, hatari kubwa na ya mapema ya CCM ni kuanza kuonesha eti wanapinga katiba mpya.

Ningeshauri uongozi mpya wa CCM waone namna ya wao kuikumbatia hii ajenda ya kuwa na katiba mpya, wasiwaachie upinzani peke yao, kama kweli wanamipango ya CCM kuendelea kuonekana kwenye uso wa Tanzania miaka 20 inayokuja. Hakuna namna CCM itataka kupinga katiba mpya na kuendelea kutawala kwa miaka 20 inayokuja, sidhani kama taifa hili la vijana wenye uchu wa mabadiliko wataacha hichi kitu kitokee.

Sidhani kama ndani ya miaka 10 hadi 20 ijayo ambapo nchi itakuwa na watu kati ya milioni 70 au 80, asilimia zaidi ya 65% wakiwa vijana ambao wengi watakuwa wamesoma na hawana ajira, hapo hapo kiwango cha umasikini bado ni kikubwa, halafu hapo hapo nchi bado inaishi bila katiba mpya, hichi kitu kitakuwa kigumu sana kuwezekana, na kama kuna watu huwa wanafanya analysis ya kutabiri matukio ya miongo miwili ijayo, ni wazi kwamba kwa dunia ya sasa inavokwenda, CCM hawatakiwi kabisa kufikiria kwamba wataendelea ku exist salama bila nchi kuwa na sheria na katiba ya kueleweka.

Na itakuwa ngumu sana ku guarantee Tanzania isiyomwaga damu kama hakuta kuwa na katiba na sheria za kueleweka ndani ya miaka 10 mpaka 20 inayokuja maana ni kipindi ambacho kiwango cha subira na uvumilivi kwa watanzania walio wengi kitakuwa kimefika ukomo.

So mi nachukulia huu utawala wa mama kuwa ni kipindi cha muhimu na cha mpito kwa mustakabali wa utulivu wa nchi ya Tanzania kwa miaka 10 na 20 inayokuja. Hili suala lisichukuliwe ki uwepesi, watanzania wengi hawapo tayari kwa 'another Magufuli' ndo mana hili vugu vugu la katiba mpya ni tofauti na vugu vugu la katiba kwenye enzi ya Kikwete. Completely different atmosphere.

So kwa mtizamo wangu, katiba mpya ni damu na moyo wa CCM kama kweli itataka kusalia madarakani.
Tatizo sio ccm tu,imekua ni kasumba ya viongozi wengi wa Afrika, kuweka maslai Binafsi badala ya nchi zao wanazoziongoza, kiongonzi anasema kuleta maendeleo kwenye nchi yake wakati mifumo bora ya kuongeza uwajibikaji ili maendeleo wayasemayo yawepo haupo,inabaki ni utashi wa kiongonzi alipo, alafu utasikia mie mzalendo wizi mtu,
 
simon2016

JF-Expert Member
Oct 19, 2020
309
1,000
Kosa kubwa ni mama aliwapa kichwa kuwa mtandaoni wajadili mambo ya msingi na watachukua ushauri CCM hawata lala salama kwa hili la katiba la litafika kwa wanachi

Hizi katiba ni kwa ajili ya vyama vya siasa na sio wanachi kama wanavyo dai tangu lini mwana siasa akawa yupo juu kwa ajili ya mwananchi badala ya masilahi yake.
 
malantu

Senior Member
May 26, 2021
104
250
Moja ya mapungufu makubwa ya Watanzania ni usahaulifu. Huyu anayesema "kiwango cha subira na uvumilivu sidhani kama kitakuwa kwa Watanzania wengi" ameshasahau kuwa porojo za "tunataka katiba mpya hazijaanza Machi 19 baada ya Mama Samia kuapishwa. Zilianza mwaka 1992 pengine wakati huo mtoa mada alikuwa hajazaliwa.

Na kati ya wakati huo na sasa, yamejiri mambo mengi ambayo kwa wenzetu wanaojielewa, basi huenda muda huu CCM ingekuwa historia. Kwa kukumbusha tu, utawala wa Mkapa ulitawaliwa na ubabe uliopelekea vifo vya Wazanzibari kadhaa Januari 2001. Lakini Mkapa alimaliza muda wake salama. Akaja Jk, ambaye aliigeuza Tanzania kuwa shamba la bibi, ufisadi ukawa kama umehalalishwa na Katiba. Nae akatawala hadi muda wake ulipoisha 2015.

Na ilipotokea fursa bora kabisa kwa Upinzani kuing'oa CCM mwaka 2015 kwa kuzingatia rekodi ya kutisha ya ufisadi wa Jk na CCM yake, Upinzani ukaamua kumpokea na kumsimamisha Lowassa kuwa mgombea wake wa urais, licha ya upinzani huohuo kumtangaza tangu 2006 kuwa ni papa la ufisadi.

Na 2015 hadi Machi 2021, Tanzania ilipitishwa kwenye tanuru ka moto mkali chini ya utawala wa Magufuli. Na laiti korona isingemwondoa, angeendelea kutawala hadi aamue kuachia madaraka.

Sasa hizi "hasira mpya" na "uvumilivu una mwisho" vinatoka wapi? Usahaulifu au kujimwambafai ilhali uwezo pekee uliopo ni kwenye kufuatilia ubuyu?

Yes Katiba mpya ni muhimu lakini you guys need to be realistic. Itapatikana kwa matakwa ya Mama Samia na si kwa porojo za mtandaoni. I'm not saying kwamba Katiba inahitaji ridhaa ya Rais bali nakumbusha tu hali halisi ilivyo.
Nimeishia hapo uliposema kuwa upinzani ulifanya kosa kumsimamisha Lowasa na ndio maana ukashindwa. Kusema ukweli umeongea pumba tu.
 
Rwazi1

JF-Expert Member
May 3, 2013
1,019
2,000
Na hii ndo naona pia ni tatizo kwa CCM na viongozi wake, kitendo cha wao kuhisi kwamba CCM kama chama ni ideology ambayo inapaswa kulindwa ndo ambacho kinadumaza hii nchi. Mi kwa mawazo yangu, CCM has to die ili hii nchi itoke hapa ilipo. Kama ilivotokea Kenya kwa chama cha KANU, for good reason, na manufaa ya hii nchi.

Inatakiwa tufike mahali mtu kama NAPE yupo kwenye chama chake na mtu kama January yupo kwenye chama chake na wanapambana kwa hoja, hatutaki watu waendelee kujificha kwenye koti la U CCM hapo ndipo hii nchi itaamka.

Ingalikuwa nina say kwenye deep state ya hii nchi ningefanya namna CCM kama chama kife, kwa manufaa ya Tanzania
Kwenye ccm kufariki ndo nimekuelewa hasa. Hii nchi bado ni mfumo wa chama kimoja. Hata wapinzani ni kama wanashindana na goliath. Hawana hadh ya chama cha siasa dhidi ya chama cha siasa kisera na kiitikad. Wanabakishiwa ka roho kiduchu kama tu ishara ya uwepo wa demokrasia
Wanaccmm vigogo na wapambe wameshaiba na kuibiana kwa miongo mingi kiasi hakuna wa kujitoa faham kuikomboa nchi kiuchumi, kisiasa na kifikra. Ndo mana zilizokuwa mali za ccm kikiwa chama dola pekee ati hadi leo ni mali yao badala ya zingerudishwa serkalini hasa viwanja vya wazi na michezo na majengo na kumbi.
Changamoto kubwa ni hatuna wapinzani wa kweli hadi sasa. Sabab wanafanya siasa kwa hisan ya ccm na si kidemokrasia. Wanaofurukuta nao wengi ni juu ya tumbo zao. Ndo mana hoja ya kutathmin malipo yao na KODI hawaip ushirikiano. Hata raia tumeshamezwa na ccm kias kwamba wapinzan wanaonekana wapingaji badala ya sera mbadala. Tusubiri kizaz flan kiishe labda! ccm ndo ikufe. Ni suala la muda tu.
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
18,493
2,000
Kwasababu bado sina chama cha siasa, nataka kuwashauri viongozi wakuu wa CCM. 'Msijitenge na hoja ya katiba na kuwaachia upinzani pekee, mnafanya kosa kubwa'

Nimeangalia trend mpaka sasa huko mitandaoni, nimesikitika kuona kwamba kila mwana CCM ambaye ataongea kuhusu katiba mpya, basi ataongelea kwa kusema kwamba nchi haihitaji katiba mpya kwa sasa. Hili ni kosa kubwa sana, nadhani ambacho CCM wangepaswa kufanya kwa sasa ni kufanya utafiti wa kisayansi wa kujiridhisha ni kwa asilimia ngapi wananchi milioni 60 wana kiu ya katiba mpya.

Baada ya kujiridhisha ndipo haswa wanatakiwa kuja na hoja ama za kupinga katiba mpya ama na wao wajiingize moja kwa moja kwenye ajenda ya katiba mpya.

Kufuatia miaka mitano ya 'stress' ni wazi kwamba upepo uliopo sasahivi ni upepo wa mabadiliko, na wala CCM wasidhani kwamba upepo huu wakudai mabadiliko ni hoja ya CHADEMA, la hasha, kuna wana CCM wengi tu sasahivi nao wanahisi kwamba kuna mabadiliko yanahitajika kufanyika.

Sasa ukiwa kwenye hali hiyo ya uchu wa watu kutaka kubadilika, kama chama cha siasa na wewe itabidi uone namna gani uta flow na mawimbi, na hii itakuwa na matokeo makubwa sana kwenye umaarufu wa chama cha mapinduzi chenyewe, hatari kubwa na ya mapema ya CCM ni kuanza kuonesha eti wanapinga katiba mpya.

Ningeshauri uongozi mpya wa CCM waone namna ya wao kuikumbatia hii ajenda ya kuwa na katiba mpya, wasiwaachie upinzani peke yao, kama kweli wanamipango ya CCM kuendelea kuonekana kwenye uso wa Tanzania miaka 20 inayokuja. Hakuna namna CCM itataka kupinga katiba mpya na kuendelea kutawala kwa miaka 20 inayokuja, sidhani kama taifa hili la vijana wenye uchu wa mabadiliko wataacha hichi kitu kitokee.

Sidhani kama ndani ya miaka 10 hadi 20 ijayo ambapo nchi itakuwa na watu kati ya milioni 70 au 80, asilimia zaidi ya 65% wakiwa vijana ambao wengi watakuwa wamesoma na hawana ajira, hapo hapo kiwango cha umasikini bado ni kikubwa, halafu hapo hapo nchi bado inaishi bila katiba mpya, hichi kitu kitakuwa kigumu sana kuwezekana, na kama kuna watu huwa wanafanya analysis ya kutabiri matukio ya miongo miwili ijayo, ni wazi kwamba kwa dunia ya sasa inavokwenda, CCM hawatakiwi kabisa kufikiria kwamba wataendelea ku exist salama bila nchi kuwa na sheria na katiba ya kueleweka.

Na itakuwa ngumu sana ku guarantee Tanzania isiyomwaga damu kama hakuta kuwa na katiba na sheria za kueleweka ndani ya miaka 10 mpaka 20 inayokuja maana ni kipindi ambacho kiwango cha subira na uvumilivi kwa watanzania walio wengi kitakuwa kimefika ukomo.

So mi nachukulia huu utawala wa mama kuwa ni kipindi cha muhimu na cha mpito kwa mustakabali wa utulivu wa nchi ya Tanzania kwa miaka 10 na 20 inayokuja. Hili suala lisichukuliwe ki uwepesi, watanzania wengi hawapo tayari kwa 'another Magufuli' ndo mana hili vugu vugu la katiba mpya ni tofauti na vugu vugu la katiba kwenye enzi ya Kikwete. Completely different atmosphere.

So kwa mtizamo wangu, katiba mpya ni damu na moyo wa CCM kama kweli itataka kusalia madarakani.
Ukweli ni kwamba wananchi wengi kwanza hawajui hata katiba ni nini.

Pili, Ni ukweli usiopingika kwamba CCM bado inao uwezo wa kushinda uchaguzi kwa haki kabisa kutokana na machinery waliyonayo. Makundi yote muhimu kama wazee, wanawake bado yako upande wao.

Vyama vya upinzani vinaungwa mkono na vijana ambao wengi ni OYA OYA, kiasi kwamba kupiga kura inategemea mihemko yao imepandaje.

Tatu, Ni kweli taifa hili linahitaji sera mpya kiuchumi kutokana na wingi wa watu hasa miaka 10 ijayo.

Kwa vyovyote vile kama ni joto la kisiasa litakuwepo hata kama itakuwepo katiba mpya.

Kwanza katiba mpya ni kitu relative sana, haijulikani ni ipi na iliyoje maana mpaka sasa siasa na madaraka tu ndio yameteka mjadala na ndio maana hata imekwama.
 
Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
4,575
2,000
Moja ya mapungufu makubwa ya Watanzania ni usahaulifu. Huyu anayesema "kiwango cha subira na uvumilivu sidhani kama kitakuwa kwa Watanzania wengi" ameshasahau kuwa porojo za "tunataka katiba mpya" hazijaanza Machi 19 baada ya Mama Samia kuapishwa. Zilianza mwaka 1992 pengine wakati huo mtoa mada alikuwa hajazaliwa.

Na kati ya wakati huo na sasa, yamejiri mambo mengi ambayo kwa wenzetu wanaojielewa, basi huenda muda huu CCM ingekuwa historia. Kwa kukumbusha tu, utawala wa Mkapa ulitawaliwa na ubabe uliopelekea vifo vya Wazanzibari kadhaa Januari 2001. Lakini Mkapa alimaliza muda wake salama. Akaja Jk, ambaye aliigeuza Tanzania kuwa shamba la bibi, ufisadi ukawa kama umehalalishwa na Katiba. Nae akatawala hadi muda wake ulipoisha 2015.

Na ilipotokea fursa bora kabisa kwa Upinzani kuing'oa CCM mwaka 2015 kwa kuzingatia rekodi ya kutisha ya ufisadi wa Jk na CCM yake, Upinzani ukaamua kumpokea na kumsimamisha Lowassa kuwa mgombea wake wa urais, licha ya upinzani huohuo kumtangaza tangu 2006 kuwa ni papa la ufisadi.

Na 2015 hadi Machi 2021, Tanzania ilipitishwa kwenye tanuru ka moto mkali chini ya utawala wa Magufuli. Na laiti korona isingemwondoa, angeendelea kutawala hadi aamue kuachia madaraka.

Sasa hizi "hasira mpya" na "uvumilivu una mwisho" vinatoka wapi? Usahaulifu au kujimwambafai ilhali uwezo pekee uliopo ni kwenye kufuatilia ubuyu?

Yes Katiba mpya ni muhimu lakini you guys need to be realistic. Itapatikana kwa matakwa ya Mama Samia na si kwa porojo za mtandaoni. I'm not saying kwamba Katiba inahitaji ridhaa ya Rais bali nakumbusha tu hali halisi ilivyo.
Well, umejaribu kujibu hoja yangu lakini tatizo moja umemulika hili suala kwa darubini ya kihistoria zaidi ambayo kwa sasa ni kama haina nafasi tena kwenye hili taifa.

Unaanza kwa kusema vuguvugu la katiba halikuanza leo lilianza mwaka 1992, lakini unashindwa kutambua kwamba unafanya reference ya miaka 30 nyuma ambapo population ya Tanzania ilikuwa kama watu milioni 26 na sasa hivi ni watu tunaenda milioni 60 (Tayari kuna tofauti kubwa sana)

Darubini yako pia haijaeleza mchango wowote wa literacy rate ya sasa na ya miaka ya nyuma, kuna issue ya demography pattern ya sasa na kipindi cha nyuma, kuna issue ya mitandao ya kijamii na mawasiliano kipindi cha sasa na kilichopita. Hivi vyote vinafanya matamanio ya katiba kwa sasa na vugu vugu yawe tofauti kabisa na kipindi cha nyuma, sio tu kwa kufananisha na mwaka 1992, bali hili vugu vugu la sasa lina utofauti mkubwa hata na vugu vugu la katiba kipindi cha kikwete.

So, naona moja kwa moja, unakuwa umejifunga kwenye darubini ya historia kuliko uhalisia, whihc means hata hoja uliyoitoa haina nguvu na haipo tangible.

Nakushauri urudi kufanya utafiti tena, unajua kuandika vizuri ila unakosa contents.
 
Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
4,575
2,000
S

Sidhani kama CCM haitaki katiba mpya au katiba bora suala hapa ni muda mwafaka wa kutekeleza hilo. Ni wazi kuitaka katiba mpya na lini wazo hilo linahitaji kutekelezwa kwa mmaana ya TIMING ni jambo lingine. Utekelezaji wa hatua hii unahitaji umakini ili kuepuka madhara, maandalizi na kutathmini matokeo ya utekelezaji ni muhimu sana. Jambo lolote lenye sura ya kitaifa kugawanyika" if mishandled" linahitaji umakini mkubwa. Nashauri Rais asikurupuke ili mradi upande wa pili unashinikiza. Dhamana ya usalama wa taifa na utulivu wake uko mikononi mwa Ccm.
Vyovyote CCM itavoamua, shida kubwa na ambayo inajulikana ni kwamba CCM wanakwepa mwamvuli wa katiba mpya kwa msingi wa kulinda madaraka na 'doctrine na ideology ya CCM' ila wanasahau kwamba kwa mabadiliko haya ya demographia, kijamii, kiuelewa, ki social media, miaka 10 mpaka 20 itakuwa mingi sana kwa nchi kuendelea kuishi kwa katiba iliyotungwa miaka 50 iliyopita.

Ni changes ambozo itakuwa ngumu kuzizuia.
 
Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
4,575
2,000
Ukweli ni kwamba wananchi wengi kwanza hawajui hata katiba ni nini.

Pili, Ni ukweli usiopingika kwamba CCM bado inao uwezo wa kushinda uchaguzi kwa haki kabisa kutokana na machinery waliyonayo. Makundi yote muhimu kama wazee, wanawake bado yako upande wao.

Vyama vya upinzani vinaungwa mkono na vijana ambao wengi ni OYA OYA, kiasi kwamba kupiga kura inategemea mihemko yao imepandaje.

Tatu, Ni kweli taifa hili linahitaji sera mpya kiuchumi kutokana na wingi wa watu hasa miaka 10 ijayo.

Kwa vyovyote vile kama ni joto la kisiasa litakuwepo hata kama itakuwepo katiba mpya.

Kwanza katiba mpya ni kitu relative sana, haijulikani ni ipi na iliyoje maana mpaka sasa siasa na madaraka tu ndio yameteka mjadala na ndio maana hata imekwama.
Kwa sababu hakuna tafiti rasmi iliyofanyika, huwezi kusema eti 'wananchi wengi hawajui katiba ni nini' nadhani unafanya makosa makubwa, kwani wewe tafsiri ya wengi maana yake nini?

Na kumbuka kinachopiganiwa hapa kwa mwamvuli wa 'Katiba', ni mjumuisho wa sheri zote kandamizi ambazo watu huku mtaani wamekuwa wakipambana nazo kila uchwao, mambo tunalia dhidi ya ardhi, kodi, demokrasia.. vyote hivo framework yake ni katiba, halafu unasema watu hawafahamu.. sio kweli ... rudi kafanye utafiti tena.

Unasema vyama vya upinzani vinaungwa mkoko na vijana ambao ni OYA OYA... Oya oya maana yake ni nini? jaribu unapotoa mada uwe specific na unachosema, unafanya generalization ambayo inafanya unapoteza maana ya unachosema mkuu.
 
Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
4,575
2,000
Kwenye ccm kufariki ndo nimekuelewa hasa. Hii nchi bado ni mfumo wa chama kimoja. Hata wapinzani ni kama wanashindana na goliath. Hawana hadh ya chama cha siasa dhidi ya chama cha siasa kisera na kiitikad. Wanabakishiwa ka roho kiduchu kama tu ishara ya uwepo wa demokrasia
Wanaccmm vigogo na wapambe wameshaiba na kuibiana kwa miongo mingi kiasi hakuna wa kujitoa faham kuikomboa nchi kiuchumi, kisiasa na kifikra. Ndo mana zilizokuwa mali za ccm kikiwa chama dola pekee ati hadi leo ni mali yao badala ya zingerudishwa serkalini hasa viwanja vya wazi na michezo na majengo na kumbi.
Changamoto kubwa ni hatuna wapinzani wa kweli hadi sasa. Sabab wanafanya siasa kwa hisan ya ccm na si kidemokrasia. Wanaofurukuta nao wengi ni juu ya tumbo zao. Ndo mana hoja ya kutathmin malipo yao na KODI hawaip ushirikiano. Hata raia tumeshamezwa na ccm kias kwamba wapinzan wanaonekana wapingaji badala ya sera mbadala. Tusubiri kizaz flan kiishe labda! ccm ndo ikufe. Ni suala la muda tu.
Yaani neno CCM inatakiwa kufa kabisa, hatari ambayo naiona ni kwamba, itafika kipindi hawa viongozi watadhani CCM ni dini ambayo ni dhambi kufa na ambayo ni lazima ilinde kitu ambacho sio sawa
 
Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
4,575
2,000
Tatizo sio ccm tu,imekua ni kasumba ya viongozi wengi wa Afrika, kuweka maslai Binafsi badala ya nchi zao wanazoziongoza, kiongonzi anasema kuleta maendeleo kwenye nchi yake wakati mifumo bora ya kuongeza uwajibikaji ili maendeleo wayasemayo yawepo haupo,inabaki ni utashi wa kiongonzi alipo, alafu utasikia mie mzalendo wizi mtu,
Umemaliza kabisa mkuu, hata Kenya uchumi wao upo na nguvu sana sasa hivi ni kwa sababu walikaa chini wakatengeneza katiba ambayo ni bora kwa nchi yao, sisi bado tupo na makasia.. sijui kama tutafika kama viongozi wanaogopa katiba ambayo itanyoosha hizi taasisi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom