Kosa kubwa Watanzania tunaloelekea kulifanya

Godwine

JF-Expert Member
Jan 15, 2010
1,371
281
Kila mtanzania anatambua wazi kinachoendelea katika nchi etu, vuguvugu kubwa la mageuzi zimeshika kasi na nadhani hakuna namna ya kuzuilika ili ni jambo jema kwani nchi isiyo na mabadiliko basi imekufa.

Lakini kosa kubwa linaloelekea kufanyika ni kufanya mabadiliko kwa kuua chama tawala (CCM) na kuingiza chama cha wanamageuzi(CHADEMA) . mimi nakubaliana kuwa moja kwa moja CCM inatakiwa kupunzika kwani imechoka na mtu asidhani kuipunzisha CCM ni kuua CCM kabisa ili litakuwa kosa kubwa sana kwani chadema ikiwa madarakani bila mpinzani wa kweli CCM basi chama hiki nacho kitajisahau na kuwa kama CCM.

Tusije kufanya kosa la kukiua CCM bali tukipunzishe na kukifanya kuwa chama imara cha upinzani kitachokuja kuibana Chadema itapokuwa madarakani, na kuwe na uwiano wa nguvu katika bunge yani kama chadema wakichukua nchi basi CCM nao kama chama cha upinzani kipate wabunge wa kutosha kiweze kukisimamia chadema vizuri
 
Nani mwenye uwezo wa kukiuua chama cha siasa?. Chama cha siasa kinakufa kutokana na mwamko wa wanachama wake kuwa mdogo. Ulichoongea sijui ulilenga nin?
 
Weka data kwamba ccm inauawa
Idadi ya wanachama wapya wenye umri mdogo wanaojiunga na chama hiki ni inaelekea kuwa na karibu sifuri hivyo baada ya muda fulani chama kitakufa

Pili migogoro inayosababishwa na wanachama na viongozi wake nayo inapelekea chama hiki kufa mapema
 
Kila mtanzania anatambua wazi kinachoendelea katika nchi etu, vuguvugu kubwa la mageuzi zimeshika kasi na nadhani hakuna namna ya kuzuilika ili ni jambo jema kwani nchi isiyo na mabadiliko basi imekufa.

Lakini kosa kubwa linaloelekea kufanyika ni kufanya mabadiliko kwa kuua chama tawala (CCM) na kuingiza chama cha wanamageuzi(CHADEMA) . Mimi nakubaliana kuwa moja kwa moja CCM inatakiwa kupunzika kwani imechoka na mtu asidhani kuipunzisha CCM ni kuua CCM kabisa ili litakuwa kosa kubwa sana kwani chadema ikiwa madarakani bila mpinzani wa kweli CCM basi chama hiki nacho kitajisahau na kuwa kama CCM.

Tusije kufana kosa la kukiua CCM bali tukipunzishe na kukifanya kuwa chama imara cha upinzani kitachokuja kuibana Chadema itapokuwa madarakani...

Mmmh! I am very troubled na statement yako hasa hapo penye red. Why not kuimarisha CUF, NCCR etc ili vifanye kazi yakuibana CDM kama mtizamo ndio huo? Why CCM ? What is so special about CCM? Kwa upande wangu I careless about vyama, however: najaribu kuangalia mantiki ya "u-special" wa CCM kuwa chama kinachokosoa chama kingine.

Nisaidieni kwenye hili tafadhali.
 
Mwaka wa kufa nyani miti yote huteleza,na mgonjwa wa kufa anaonekana kwa hali yake ya kutapa tapa na kukosa kauli mzuri yenye msimamo,hao magamba washaishiwa pumzi kilichobak wapishe wenye pumzi,wakilazimisha ndo huko kuumbuka mbeleni! INATOSHA SANA
 
Mmmh! I am very troubled na statement yako hasa hapo penye red. Why not kuimarisha CUF, NCCR etc ili vifanye kazi yakuibana CDM kama mtizamo ndio huo? Why CCM ? What is so special about CCM? Kwa upande wangu I careless about vyama, however: najaribu kuangalia mantiki ya "u-special" wa CCM kuwa chama kinachokosoa chama kingine. Nisaidieni kwenye hili tafadhali.

ni chama kinachoelewa muundo wa serikali na uongozwaji wake, pia ni chama chenye rasilimali nyingi kutosha kujiendesha na vile vile ni miongoni mwa vyama vya kihistoria ambavyo vinaweza kushiriki kideplomasia kiurahisi
 
Godwine, ina maana chama kingine kikishika uongozi una uhakika bado rasilimali za CCM zitabakia kuwa zao e.g. viwanja, majengo etc??

By the way, CCM ina rasilimali nyingi zinazowasaidia kujiendesha au zina "wafadhili" wengi wanaosaidia kukiendesha chama?

Je CCM ikikosa kipande cha keki (madaraka) hao "wafadhili" wataendelea kuwafadhili? Je CCM wakiondoka madarakani source yao hasa ya pesa itakuwa nini? Je kama ni ruzuku pekee na ada ya uanachama, will this be enough kwa wao kuendelea kuwa strong?

Je CCM ikiondoka madarakani ni wanachama wangapi hasa watakaobaki kuwa wanachama hai watakaoamua kubaki kukiimarisha? Nafikiri kama tungekuwa na majibu ya uhakika kwenye maswali haya tuwengeweza ku-support your argument. Kuhusu kuelewa muundo wa serikali sidhani kama ni "chama" kinaelewa muundo wa serikali bali watu.

Kuna watu kwenye upinzani wanaelewa vizuri sana muundo wa serikali na vilevile kuna watu CCM hawaelewi hata serikali inaendeshwaje. Kumbuka wanachama wengi wa upinzani ni hao hao walikuwa CCM kabla ya mfumo wa vyama vingi. Na pia tukumbuke chama kingine kikiingia madarakani kinaweza kika-introduce mambo mapya/muundo mpya wa serikali (whether ni kwa ridhaa au bila ridhaa ya wananchi). Yote itategemea na wemeingiaje.
 
Tatizo la CHADEMA ni kudhani kuwa wataikamata DOLA kiurahisi kwa CCM kuiachia dola kiurahisi. Walitakiwa kuanzia sasa waunde idara maalum ya kijasusi ya kudhibiti kura ikiwemo kuzilinda. Waanzishe sasa hivi idara ya mawasiliano itakayokuwa na ufanisi wakati wa uchaguzi mwaka 2015.

Vinginevyo wakidhani ikulu itakuja kwenye kikombe cha dhahabu basi wasiitarajie hata kama CCM wataweka mgombea shetani kupambana nao.
 
Nani kakudanganya kuwa ccm inakaribia kufa? Na mbona dalili zako ulizozitoa ni kama hazina nguvu ya kutosha? Hao vijana wa sasa hivi wanaoikimbia ccm nenda kawaulize wangapi wana kadi za vyama pinzani? Kama si maneno tu ya mdomoni!na hiyo migogoro uliyosema mi nadhani si migogoro bali ulipaswa kuziita ni harakati ya kukijenga upya chama hicho kwani kiukweli kilijisahau sana madarakani.

Binafsi naamini kitajengeka upya huku kikiendelea kula bata madarakani kwani bado sijaona chama pinzani chochote chenye nguvu ya kukitoa ccm madarakani! Tofauti ya ccm na hivyo vyama vingine vya upinzani ni kuwa ccm ina wanachama wengi walio hai ambao ni wapiga kura wazuri sana na sio kama chadema ambao watu wao wengi ambao ni vijana si wanachama hai na si wapiga kura wazuri,wanajazana kibao kwenye mkutano lakini siku ya uchaguzi utakuta wamejazana gesti kutimiza ahadi zao za ngono badala ya kujazana kwenye vituo ya upigaji kura ili watimize ahadi ya chama chao.

Kiukweli wengi si watiifu kulinganisha na vijana wa ccm!
 
Godwin... Unaongea kana kwamba wananchi wao ndio wanai favour CCM kuwepo ilipo... kama vile yale yoote yanayotokea yalikua supported na majority Tanzanians alafu ndio yaka buma! na sasa wanataka kuahirisha...

Unasema kuwa tusifanye kosa la Kuua CCM?? Kweli are you serious?? CCM wanajiua wenyewe... a natural death at that.. inaweza isiwe the next election but they are already dead in the hearts of the people na tayari wao ni wafu... Unayosema kuhusu CDM ni kweli... but let them come nao wafanye their own mistakes ili iwe dhahiri kua bado we have a long way to go kumpata Raisi mzalendo... Ili hizi assumptions tulizo nazo kuhusu which is a better chama ziishe...

Note that CCM ikija anguka (which is inevitable... its rise will never happen again) for ni dhahiri makundi yao ndani ya Chama ni wazi hakuna Umoja - kinawaweka pamoja ni kua woote ni wana CCM.. Hasa unategemea after its fall kuna mtu atabaki pale?? Labda Nape....
 
Idadi ya wanachama wapya wenye umri mdogo wanaojiunga na chama hiki ni inaelekea kuwa na karibu sifuri hivyo baada ya muda fulani chama kitakufa

Pili migogoro inayosababishwa na wanachama na viongozi wake nayo inapelekea chama hiki kufa mapema

sasa hapa nani anaeua chama. Nani aliyekatazwa asijiunge na ccm.
 
Nani kakudanganya kuwa ccm inakaribia kufa? Na mbona dalili zako ulizozitoa ni kama hazina nguvu ya kutosha? Hao vijana wa sasa hivi wanaoikimbia ccm nenda kawaulize wangapi wana kadi za vyama pinzani? Kama si maneno tu ya mdomoni!na hiyo migogoro uliyosema mi nadhani si migogoro bali ulipaswa kuziita ni harakati ya kukijenga upya chama hicho kwani kiukweli kilijisahau sana madarakani.

Binafsi naamini kitajengeka upya huku kikiendelea kula bata madarakani kwani bado sijaona chama pinzani chochote chenye nguvu ya kukitoa ccm madarakani! Tofauti ya ccm na hivyo vyama vingine vya upinzani ni kuwa ccm ina wanachama wengi walio hai ambao ni wapiga kura wazuri sana na sio kama chadema ambao watu wao wengi ambao ni vijana si wanachama hai na si wapiga kura wazuri,wanajazana kibao kwenye mkutano lakini siku ya uchaguzi utakuta wamejazana gesti kutimiza ahadi zao za ngono badala ya kujazana kwenye vituo ya upigaji kura ili watimize ahadi ya chama chao.

Kiukweli wengi si watiifu kulinganisha na vijana wa ccm!

Aisee una matusi kweli, kwa hiyo wizi wote unofanyika na CCM vijana hatuoni ila tumekalia NGONO kwenye magesti wakati ninyi vijana wa ccm mnakwenda kupiga kura ee? Hongera bwana huo ndio ulevi wa madaraka! hata gadafi bado anasema wananchi wa Libya hawataki waasi na watapigana mpaka tone la mwisho kuwatoa!lakini anasemea shimoni kwenye maficho! hivi huoni huruma watu wanaokufa kwa njaa,hospital zisizo na vifaa, elimu duni nk,hivibado tu unashabiakia chama ambacho kinaongoza nchi tajairi kwa madini hebu fikilia mamigodi ya bulyankulu, kahama, buhemba na mengine mengi tu lakini wanaongoza kulipa kodi nchi hii ni kampuni za bia?

Hata chibuku wanatoa kodi zaidi ya kahama minining huoni ajabu? na bado unashabikia tu!makampuni kibao yanachuma hapa Tanzania lakini hayalipi kodi ya kutosha na wanapeleka pesa yote nje wewe unachekelea tu na ushabiki usio na maana! hata kama wewe unafaidika ndugu zako wote wako kama wewe?

Hivi wewe ni Mtanzania kweli?????????? au mtanzania mwenye asili ya? unamaudhi sana Nchi inaibiwa kila kitu wewe unashabikia halafu unatukana wanao jaribu kupigania Nchi yao!
 
Marehemu ccm ananyongwa na ndugu zake,sisi tunasuri mda wa mazishi tukamzike.
 
Godwin... Unaongea kana kwamba wananchi wao ndio wanai favour CCM kuwepo ilipo... kama vile yale yoote yanayotokea yalikua supported na majority Tanzanians alafu ndio yaka buma! na sasa wanataka kuahirisha...

Unasema kua tusifanye kosa la Kuua CCM?? Kweli are you serious?? CCM wanajiua wenyewe... a natural death at that.. inaweza isiwe the next election but they are already dead in the hearts of the people na tayari wao ni wafu... Unayosema kuhusu CDM ni kweli... but let them come nao wafanye their own mistakes ili iwe dhahiri kua bado we have a long way to go kumpata Raisi mzalendo... Ili hizi assumptions tulizo nazo kuhusu which is a better chama ziishe...

Note that CCM ikija anguka (which is inevitable... its rise will never happen again) for ni dhahiri makundi yao ndani ya Chama ni wazi hakuna Umoja - kinawaweka pamoja ni kua woote ni wana CCM.. Hasa unategemea after its fall kuna mtu atabaki pale
?? Labda Nape....
Hapo ndipo kwenye msingi na hoja yangu nilipenda chama cha CCM kianguke tena mapema mno lakini kisife kiwe hai na tanzania tuwe na vyama vya siasa viwili vyenye nguvu ambayo kuanzia hapo viwe vikibadilishana madaraka kama wamarekani walivyokuwa na democratic na republican

Llakini CCM kinapoelekea si kuchokwa tu na wananchi bali mpaka kinachokwa na viongozi wa chama chao wenyewe hili ndilo kosa kubwa ambalo halitoweza kukifanya kiwepo hai tena baada ya kudondoka
 
Back
Top Bottom