Kosa kubwa Watanzania tunaloelekea kulifanya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kosa kubwa Watanzania tunaloelekea kulifanya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Godwine, Sep 1, 2011.

 1. G

  Godwine JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kila mtanzania anatambua wazi kinachoendelea katika nchi etu, vuguvugu kubwa la mageuzi zimeshika kasi na nadhani hakuna namna ya kuzuilika ili ni jambo jema kwani nchi isiyo na mabadiliko basi imekufa.

  Lakini kosa kubwa linaloelekea kufanyika ni kufanya mabadiliko kwa kuua chama tawala (CCM) na kuingiza chama cha wanamageuzi(CHADEMA) . mimi nakubaliana kuwa moja kwa moja CCM inatakiwa kupunzika kwani imechoka na mtu asidhani kuipunzisha CCM ni kuua CCM kabisa ili litakuwa kosa kubwa sana kwani chadema ikiwa madarakani bila mpinzani wa kweli CCM basi chama hiki nacho kitajisahau na kuwa kama CCM.

  Tusije kufanya kosa la kukiua CCM bali tukipunzishe na kukifanya kuwa chama imara cha upinzani kitachokuja kuibana Chadema itapokuwa madarakani, na kuwe na uwiano wa nguvu katika bunge yani kama chadema wakichukua nchi basi CCM nao kama chama cha upinzani kipate wabunge wa kutosha kiweze kukisimamia chadema vizuri
   
 2. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Nani mwenye uwezo wa kukiuua chama cha siasa?. Chama cha siasa kinakufa kutokana na mwamko wa wanachama wake kuwa mdogo. Ulichoongea sijui ulilenga nin?
   
 3. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Umenena!
   
 4. Desteo

  Desteo JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 448
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Weka data kwamba ccm inauawa
   
 5. makwimoge

  makwimoge JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 294
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kuua CCM waachiwe wana CCM wenyewe
   
 6. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ccm itakufa kutokana nawao kwa wao wala sio CDm maana makundi yaliyomo ndio yataisamabalatisha
   
 7. G

  Godwine JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Idadi ya wanachama wapya wenye umri mdogo wanaojiunga na chama hiki ni inaelekea kuwa na karibu sifuri hivyo baada ya muda fulani chama kitakufa

  Pili migogoro inayosababishwa na wanachama na viongozi wake nayo inapelekea chama hiki kufa mapema
   
 8. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mmmh! I am very troubled na statement yako hasa hapo penye red. Why not kuimarisha CUF, NCCR etc ili vifanye kazi yakuibana CDM kama mtizamo ndio huo? Why CCM ? What is so special about CCM? Kwa upande wangu I careless about vyama, however: najaribu kuangalia mantiki ya "u-special" wa CCM kuwa chama kinachokosoa chama kingine.

  Nisaidieni kwenye hili tafadhali.
   
 9. Wakusini

  Wakusini JF-Expert Member

  #9
  Sep 1, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 456
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 80
  Mwaka wa kufa nyani miti yote huteleza,na mgonjwa wa kufa anaonekana kwa hali yake ya kutapa tapa na kukosa kauli mzuri yenye msimamo,hao magamba washaishiwa pumzi kilichobak wapishe wenye pumzi,wakilazimisha ndo huko kuumbuka mbeleni! INATOSHA SANA
   
 10. G

  Godwine JF-Expert Member

  #10
  Sep 1, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  ni chama kinachoelewa muundo wa serikali na uongozwaji wake, pia ni chama chenye rasilimali nyingi kutosha kujiendesha na vile vile ni miongoni mwa vyama vya kihistoria ambavyo vinaweza kushiriki kideplomasia kiurahisi
   
 11. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #11
  Sep 1, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Godwine, ina maana chama kingine kikishika uongozi una uhakika bado rasilimali za CCM zitabakia kuwa zao e.g. viwanja, majengo etc??

  By the way, CCM ina rasilimali nyingi zinazowasaidia kujiendesha au zina "wafadhili" wengi wanaosaidia kukiendesha chama?

  Je CCM ikikosa kipande cha keki (madaraka) hao "wafadhili" wataendelea kuwafadhili? Je CCM wakiondoka madarakani source yao hasa ya pesa itakuwa nini? Je kama ni ruzuku pekee na ada ya uanachama, will this be enough kwa wao kuendelea kuwa strong?

  Je CCM ikiondoka madarakani ni wanachama wangapi hasa watakaobaki kuwa wanachama hai watakaoamua kubaki kukiimarisha? Nafikiri kama tungekuwa na majibu ya uhakika kwenye maswali haya tuwengeweza ku-support your argument. Kuhusu kuelewa muundo wa serikali sidhani kama ni "chama" kinaelewa muundo wa serikali bali watu.

  Kuna watu kwenye upinzani wanaelewa vizuri sana muundo wa serikali na vilevile kuna watu CCM hawaelewi hata serikali inaendeshwaje. Kumbuka wanachama wengi wa upinzani ni hao hao walikuwa CCM kabla ya mfumo wa vyama vingi. Na pia tukumbuke chama kingine kikiingia madarakani kinaweza kika-introduce mambo mapya/muundo mpya wa serikali (whether ni kwa ridhaa au bila ridhaa ya wananchi). Yote itategemea na wemeingiaje.
   
 12. HT

  HT JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kama kitakufa acha kife. Tuna vyama vingi mno
   
 13. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #13
  Sep 2, 2011
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,126
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Tatizo la CHADEMA ni kudhani kuwa wataikamata DOLA kiurahisi kwa CCM kuiachia dola kiurahisi. Walitakiwa kuanzia sasa waunde idara maalum ya kijasusi ya kudhibiti kura ikiwemo kuzilinda. Waanzishe sasa hivi idara ya mawasiliano itakayokuwa na ufanisi wakati wa uchaguzi mwaka 2015.

  Vinginevyo wakidhani ikulu itakuja kwenye kikombe cha dhahabu basi wasiitarajie hata kama CCM wataweka mgombea shetani kupambana nao.
   
 14. B

  Bucad Senior Member

  #14
  Sep 2, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 120
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nani kakudanganya kuwa ccm inakaribia kufa? Na mbona dalili zako ulizozitoa ni kama hazina nguvu ya kutosha? Hao vijana wa sasa hivi wanaoikimbia ccm nenda kawaulize wangapi wana kadi za vyama pinzani? Kama si maneno tu ya mdomoni!na hiyo migogoro uliyosema mi nadhani si migogoro bali ulipaswa kuziita ni harakati ya kukijenga upya chama hicho kwani kiukweli kilijisahau sana madarakani.

  Binafsi naamini kitajengeka upya huku kikiendelea kula bata madarakani kwani bado sijaona chama pinzani chochote chenye nguvu ya kukitoa ccm madarakani! Tofauti ya ccm na hivyo vyama vingine vya upinzani ni kuwa ccm ina wanachama wengi walio hai ambao ni wapiga kura wazuri sana na sio kama chadema ambao watu wao wengi ambao ni vijana si wanachama hai na si wapiga kura wazuri,wanajazana kibao kwenye mkutano lakini siku ya uchaguzi utakuta wamejazana gesti kutimiza ahadi zao za ngono badala ya kujazana kwenye vituo ya upigaji kura ili watimize ahadi ya chama chao.

  Kiukweli wengi si watiifu kulinganisha na vijana wa ccm!
   
 15. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #15
  Sep 2, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Godwin... Unaongea kana kwamba wananchi wao ndio wanai favour CCM kuwepo ilipo... kama vile yale yoote yanayotokea yalikua supported na majority Tanzanians alafu ndio yaka buma! na sasa wanataka kuahirisha...

  Unasema kuwa tusifanye kosa la Kuua CCM?? Kweli are you serious?? CCM wanajiua wenyewe... a natural death at that.. inaweza isiwe the next election but they are already dead in the hearts of the people na tayari wao ni wafu... Unayosema kuhusu CDM ni kweli... but let them come nao wafanye their own mistakes ili iwe dhahiri kua bado we have a long way to go kumpata Raisi mzalendo... Ili hizi assumptions tulizo nazo kuhusu which is a better chama ziishe...

  Note that CCM ikija anguka (which is inevitable... its rise will never happen again) for ni dhahiri makundi yao ndani ya Chama ni wazi hakuna Umoja - kinawaweka pamoja ni kua woote ni wana CCM.. Hasa unategemea after its fall kuna mtu atabaki pale?? Labda Nape....
   
 16. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #16
  Sep 2, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  CCM haijui siasa za kistaarabu na kushindana kwa hoja, TO HELL CCM.!
   
 17. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #17
  Sep 2, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  sasa hapa nani anaeua chama. Nani aliyekatazwa asijiunge na ccm.
   
 18. k

  kajembe JF-Expert Member

  #18
  Sep 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 756
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Aisee una matusi kweli, kwa hiyo wizi wote unofanyika na CCM vijana hatuoni ila tumekalia NGONO kwenye magesti wakati ninyi vijana wa ccm mnakwenda kupiga kura ee? Hongera bwana huo ndio ulevi wa madaraka! hata gadafi bado anasema wananchi wa Libya hawataki waasi na watapigana mpaka tone la mwisho kuwatoa!lakini anasemea shimoni kwenye maficho! hivi huoni huruma watu wanaokufa kwa njaa,hospital zisizo na vifaa, elimu duni nk,hivibado tu unashabiakia chama ambacho kinaongoza nchi tajairi kwa madini hebu fikilia mamigodi ya bulyankulu, kahama, buhemba na mengine mengi tu lakini wanaongoza kulipa kodi nchi hii ni kampuni za bia?

  Hata chibuku wanatoa kodi zaidi ya kahama minining huoni ajabu? na bado unashabikia tu!makampuni kibao yanachuma hapa Tanzania lakini hayalipi kodi ya kutosha na wanapeleka pesa yote nje wewe unachekelea tu na ushabiki usio na maana! hata kama wewe unafaidika ndugu zako wote wako kama wewe?

  Hivi wewe ni Mtanzania kweli?????????? au mtanzania mwenye asili ya? unamaudhi sana Nchi inaibiwa kila kitu wewe unashabikia halafu unatukana wanao jaribu kupigania Nchi yao!
   
 19. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #19
  Sep 2, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,000
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Marehemu ccm ananyongwa na ndugu zake,sisi tunasuri mda wa mazishi tukamzike.
   
 20. G

  Godwine JF-Expert Member

  #20
  Sep 2, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hapo ndipo kwenye msingi na hoja yangu nilipenda chama cha CCM kianguke tena mapema mno lakini kisife kiwe hai na tanzania tuwe na vyama vya siasa viwili vyenye nguvu ambayo kuanzia hapo viwe vikibadilishana madaraka kama wamarekani walivyokuwa na democratic na republican

  Llakini CCM kinapoelekea si kuchokwa tu na wananchi bali mpaka kinachokwa na viongozi wa chama chao wenyewe hili ndilo kosa kubwa ambalo halitoweza kukifanya kiwepo hai tena baada ya kudondoka
   
Loading...