Kosa kubwa wanalofanya waajiriwa ndio maana wanalipwa mishahara midogo

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,883
NG'ANGANIA KUONGEZA UTAALAMU SIO MSHAHARA

Kwa Mkono wa, Robert Heriel

Watu wengi wamekuwa wakilalamika mishahara yao ni midogo, hivyo huwashurutisha waajiri wao waongeze mishahara. Tangu ningeli mdogo malalamiko haya yapo, na bila shaka mpaka nitaondoka duniani yataendelea kuwapo dunia ingalipo.

Serikali imekuwa ikilaumiwa kwa kulipa wafanyakazi na watumishi wake mishahara ya wagonga urimbo, mishahara kiduchu. Pia wafanyakazi wa viwandani wamekuwa wakilalamika kila iitwapo leo kuhusu mishahara yao kuwa midogo. Ni kweli mishahara yao ni midogo mno, nilifuatilia mahali mahali kwenye viwanda vya hapa nchini kuanzia Dar es salaam, Morogoro, Arusha na kule Kagera ambapo asilimia kubwa ya mishahara ya wafanyakazi hulipwa si zaidi ya laki na themanini kwa mwezi. Hii ni hatari sana.

Sio ajabu siku hizi mtu mwenye shahada siku hizi kulipwa 200,000/= kwa mwezi kama mshahara. Huo ni mshahara mdogo sana. Lakini licha ya udogo wake usishangae watu wakiupigania kwa udi na uvumba kusudi mkono uende kinywani.

Leo Taikon wa Fasihi ninamaneno machache sana katika suala hili.

Mtu halipwi mshahara mkubwa kwa kufanya kazi kubwa au kwa kazi inayochukua muda mrefu. Mtu hulipwa mshahara mkubwa kulingana na utaalamu wake katika kazi anayoifanya, hiyo huitwa thamani ya mtu kwenye kazi.

Kufanya kazi pekeake haitoshi bali kufanya kazi kitaalamu na kuzalisha zaidi. Kusema nafanya kazi sana na kazi ngumu haitoshi pekeake, kwani hata Punda au ng'ombe anaweza kufanya kazi tena zaidi yako na malipo yake yanafahamika ni chakula na sehemu ya kulala. Hii ni kutokana na sababu kuwa Punda licha ya kufanya kazi ya nguvu na kwa muda mrefu lakini hafanyi kazi kitaalamu.

Ukiona mshahara unaopewa unaishia kwenye chakula, nguo na malazi basi wewe hauna tofauti na Punda na Ng'ombe wanaokokota jembe shambani ambao nao malipo yao ni hayo hayo. Jua kabisa hufanyi kazi kitaalamu bali unafanya kazi isiyo na utaalam mkubwa.

Using'ang'anie kulipwa mishahara mikubwa wakati hauna utaalamu mkubwa, huo huitwa wendawazimu, kuchanganyikiwa na kutojielewa.

Mshahara unaongezwa kulingana na utaalamu wa kazi yako, na matokeo ya kazi yako.

Kwa mfano, mwalimu hauwezi taka uongezwe mshahara wakati huna utaalamu wowote katika kazi yako ya kufundisha, Hujui kufundisha vizuri, watoto wanafeli kila matokeo yatokapo, unakuta kwenye somo lako zaidi ya 90% wamepata F alafu unataka kuongezewa mshahara. Huo ni wendawazimu.

Unakuta Wakili kwenye kesi anazozisimamia kwenye kesi kumi, kashinda tatu, alafu saba zote kashindwa kwa nini usipewe mshahara mdogo

Unakuta Daktari wa upasuaji, kwenye kila upasuaji anashindwa, yaani zaidi ya 80% anashindwa kwa nini asilipwe mshahara mdogo.

Kuwa na elimu kubwa sio kuwa na utaalamu mkubwa. Wapo watu wana Phd ya Mambo ya IT lakini wanashindwa utaalamu na watu ambao hata hawajafika chuo.

Sifa kuu ya mtaalam hadai mshahara mkubwa, yaani wewe mwenyewe unayemuajiri utajikuta unampa mshahara mkubwa huku ukimbembeleza asije akaondoka kwani yeye ni muhimu kwenye ofisi yako.

Hakuna mtaalamu anayenyanyaswa hata siku moja, ukiona unafanya kazi alafu unanyanyaswa jua wewe sio chochote kwenye hiyo ofisi.

Mtu mwenye utaalamu katika fani fulani pale anapoona maslahi ni madogo, hawezi kulalamika kuwa analipwa mshahara mdogo, atakachosema ni kuwa anataka kupumzika kazi kidogo abadilishe mazingira, alafu utashangaa mwajiri wake atakavyomuomba aendelee kubaki, tena atamuambia kuwa; kama ni mshahara nitakuongezea mara mbili kabisa. Ukiona umefikia level hii ujue wewe ni mtaalamu.

Lakini mwenzangu na mie, kazi huna lolote, hapo ofisini unakaa kwa kujipendekeza ili usipunguzwe, kwa nini usilipwe mshahara wa punda unaoishia kwenye chakula na malazi.

Ukitaka kupima thamani ya utaalam wa kazi yako, jaribu kumuambia boss wako unataka upumzike kazi ubadilishe mazingira, uone siku hiyo hiyo kama hutaondolewa.

Vijana mliochuoni acheni kukariri madesa, jitahidini kuwa mahiri katika fani mnazosomea, sio unakariri na kupata ufaulu mkubwa sijui Divishen one, sijui GPA ya First class lakini kichwani huna lolote.

Hakuna mtu anayeweza kukunyanyasa kama wewe ni mtaalamu katika fani yako.

Embu angalia Wachungaji kama wakina Mwamposa, Gwajima, Suguye, Mchungaji Daniel Mgogo hao ni wataalamu wa masuala ya injili na mahubiri. Hao lazima uwalipe vizuri upende usipende, usipowalipa vizuri ndio huanzisha makanisa yao kwani wanaona unawapotezea muda wao. Mtu ibada moja watu wanachanga sadaka zaidi ya milioni tatu alafu uje umlipe laki mbili, unafikiri atakubali? thubutu!

Kwenye muziki halikadhalika, kuna viwanamuziki mshenzi havina utaalamu wowote wa muziki lakini vinapenda malipo mazuri, wanamuziki wa hivi wengi ndio hulalamika kuwa wananyonywa, wanaibiwa pesa zao na mapromota kama sio wadhamini. Sasa kama uwezo wako uko chini unataka ulipwe posho kubwa kweli! Ajabu hii.

Sishangai wasanii hao wanapoachana na hao mapromota huanguka kimuziki kisha husingizia kuwa wanafanyiwa figisu figisu ili wasiendelee. Wewe kama unauwezo na umtaalamu wa muziki mbona ushindwe sasa, wenzako mbona wanaweza kujisimamia wenyewe na kutoboa au kama unauwezo na umtaalamu wa kiwango cha juu unapoachwa na promota huyu huwezi kukosa promota mwingine. Muangalie Diamond Platnum, Muangalie Kondeboy miongoni mwa wengine.

Using'ang'anie kupewa mshahara mzuri, bali ng'ang'ania kuwa na uwezo mkubwa katika fani yako, kuwa mtaalamu katika fani yako

Mwangalie Messi, na Ronaldo hawa ni watu wanaouwezo wa kuitishia timu walizomo

Mtaalamu ukichoka kufanya kazi, unaowezo wa kumwambia Boss kuwa unataka ukalale nyumbani mara moja kisha utarudi kesho kutwa kazini, na akakuelewa. Lakini wewe kibushuti kwa vile huna lolote, hata mkeo akiumwa utaandika na kumwomba boss wako akupe ruhusa ukamuuguze mkeo na ruhusa hiyo usipewe.

Sipo hapa kuponda yeyote bali ninachojaribu kukipenyeza kwenye akili yako msomaji wangu ni kuwa, unalipwa kulingana na thamani ya utaalamu wako unaoutoa katika ofisi unayofanyia kazi na sio kwa sababu unafanya kazi kwa hata punda anafanya kazi pia.

Fanya kazi kitaalamu sio ufanye kazi ilmradi. Tofauti ya binadamu na mnyama ipo kwenye utaalamu sio kufanya kazi, hata wanyama hufanya kazi. Hivyo usifanye kazi kama mnyama kwani matokeo yake ndio hayo ya kuambulia hela ya kula, malazi na mavazi.

Ulikuwa nami;

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa, Tandahimba
 
Kwakuwa umejifunza fasihi mpaka umeanza kujiita taikon wa fasihi, nadhani ni wakati muafaka sasa uanze kujifunza vitu vifuatavyo vinafanyaje kazi.

1. Soko huria

2. Labor markets

3. Rare talents

4. Demand and Supply

Note: Likizo kwa wafanyakazi huwa ni ukumbusho kuwa kampuni inaweza kwenda vizuri tu bika uwepo wako.
 
Ninakupa muda wa kufikiri upya halafu urudi tena.....waza kuhusu ukweli wa ulichooandika na serikali yako.na Mimi nipo tandahimba karibu na hospital ya wilaya ndipo ninapoishi
 
Kwakuwa umejifunza fasihi mpaka umeanza kujiita taikon wa fasihi, nadhani ni wakati muafaka sasa uanze kujifunza vitu vifuatavyo vinafanyaje kazi.

1. Soko huria....

Mkuu nashukuru sana kwa ushauri wako.

Na kwa mtaalamu, likizo ndio sehemu pekee anajitathmini kuwa anaweza kuishi vizuri bila uwepo wa kampuni iliyomwajiri.
 
Ninakupa muda wa kufikiri upya halafu urudi Tena.....waza kuhusu ukweli wa ulichooandika na serikali yako.na Mimi nipo tandahimba karibu na hospital ya wilaya ndipo ninapoishi

Mkuu mpaka nimeandika ujue nimeshafikiri vya kutosha mzee Baba?

Bila shaka unajua maana ya mtaalamu
 
Huwezi kujifunzia kuishi nje ya mfumo wa kampuni wakati wa likizo wakati huo huo, hiyo hiyo likizo utaiishi kwa mshahara wa kampuni.

Huyo hawezi kuwa mtaalamu mkuu, huyo ni mfanyakazi au mtumishi.

Mtaalamu lazima awe anajua kuishi nje ya mfumo na ndani ya mfumo mzee baba.

Yaani ni kama vile mwanajeshi na Komando
 
Mkuu ubarikiwe kwa kuandika kitu cha maana sana hasa kwa nyakati hizi ambazo vijana wanapambana na soko la ajira........

Andiko ni la thamani kubwa sana kwa vijana wanaojitambua na kutambua thamani yao.......

Ulichokiandika hapa ndio uhalisia wa soko la ajira na huko makazini....

UBARIKIWE SANA MTOA MADA.....
 
Back
Top Bottom