Kosa kubwa walilofanya Nyerere, Kaunda, Mugabe, Nkrumah & Co. !

Na wewe una tofauti gani za kuwalaumu marehemu kwa hali yako ya sasa ?

Kama hujui shida waliyopata watu wa kipindi hicho nenda kasome yaliyowakuta kina Thomas Sankara na Patrice Lumumba among the few....

Najua, lkn siyo wao tu waliopata shida, Dunia nzima nchi zote zilizotawaliwa walipata shida sana, Wachina walitawaliwa na Japani waliuliwa na kuchuliwa rasilimali zao nyingi, Korea waliteswa sana na Ukoloni wa Japani lkn wamemove on na hawana victim mentality, I mean huwezi kukuta Mchina anakwambia yeye ni masikini sababu alitawaliwa na Japan au huwezi sikia Mvietnam akilia umaskini kisa alitawaliwa na Ufaransa.

Wanatambua ilitokea lkn hawana victim mentality, wanafanya biashara na Dunia nzima, sisi mpaka leo hii tunalia ukoloni mamboleo, kwa nini?
 
Kuna ukweli fulani ndani ya hii topic yako... lakini, kwa mfano, Mzee wetu Nyerere, si ni haohao wazungu ndio waliokuwa wanafadhili his economic vision? Kujaribu ku- create a welfare state kwa kutegemea misaada kutoka nje. At the same time, wazungu wengine wakiitwa mabepari na makabaila.
 
Hivi hao wa zamani uliwahi wasikia hata siku moja wanawaita wazungu wenye makampuni ya kuiba rasilimali zetu kama Barick "WANAUME WA SHOKA"?
Fuatilia historia utaona jinsi hao wa zamani kwa namna fulani walikuwa jeuri kuliko hata huyu wa awamu hii anayejifanya huku ndani kuwaita "mabeberu" lakini mbele yao anawaita "wanaume" na mara kishika uchumba mara sijui nini!

Aliyeanzisha kumuita Muzungu Beberu ni Nyerere na watu wake, sasa hivi hilo neno limefufuliwa tu.
 
Ili kuanza kushindana na wazungu hatua ya kwanza ni kuungana afrika nzima,hapo ndipo tutaanza kuwa na kifua??
Swali gumu kujibika utawezekana vipi kuungana?? Na ikizingatiwa ya kuwa ndani ya nchi za kiafrika ndani yake kuna waarabu???
 
Umeongea point wallah nawaambia mzungu angekuwepo mpaka miaka ya tisini hii Dar ingekuwa kama Geneva, halafu hyo mikoa morogoro, tanga arusha, moshi, ndio yangekuwa ni majiji ya maana hiyo washington ingesubiri.
 
Na wewe una tofauti gani za kuwalaumu marehemu kwa hali yako ya sasa ?

Kama hujui shida waliyopata watu wa kipindi hicho nenda kasome yaliyowakuta kina Thomas Sankara na Patrice Lumumba among the few....
, Hawakuwa na chochote zaidi ya falsafa za hovyo tu, sasa kiko wapi?congo ipo vile vile,Namibia, zambia, zimbabwe kote njaa tu nini faida ya kumfukuza mzungu?angalia South kinachoendelea utaelewa mzungu alivyo wapa nchi nini kinaendelea Africa wana akili ndogo sana,Bora wakoloni warudi
 
Ili kuanza kushindana na wazungu hatua ya kwanza ni kuungana afrika nzima,hapo ndipo tutaanza kuwa na kifua??
Swali gumu kujibika utawezekana vipi kuungana?? Na ikizingatiwa ya kuwa ndani ya nchi za kiafrika ndani yake kuna waarabu???
Kabla ya kuiunganisha Africa kifikra Tayari wazungu wamesha wavurunga, mfano mzuri aliyetaka kuiunganisha Africa ni Gadaffi!!!!
 
, Hawakuwa na chochote zaidi ya falsafa za hovyo tu, sasa kiko wapi?congo ipo vile vile,Namibia, zambia, zimbabwe kote njaa tu nini faida ya kumfukuza mzungu?angalia South kinachoendelea utaelewa mzungu alivyo wapa nchi nini kinaendelea Africa wana akili ndogo sana,Bora wakoloni warudi
Enzi zao ningeshindwa maisha mjini ningekwenda kijijini kulima au nikiugua at least ningepata matibabu, sasa hivi vijijini ardhi yote imechukuliwa na so called wawekezaji.., yes Africa Kusini matabaka ya have and have nots are there for everyone to see.., sasa hivi hauna pesa hata watoto wako chuo watakisikia kwa jirani kwa kukosa mkopo (kumbuka sio grant ni mkopo) ila hata huo haupo..,to put it bluntly grass in not that green on the other side....
 
Ni kulia lia na kujifanya wao (sisi) ni victim, hiyo dhambi ya victim mentality imeendelea na tumerithishwa mpaka leo.

Nyerere & Co. walimuona Muzungu ni adui na walitufundisha hivyo, walimuona Muzungu ana jukumu la kutusaidia kwa sababu alitutawala, lkn walisahau Muzungu alitawala Dunia nzima na siyo sisi tu, kwanza sisi ndo wa mwisho kutawaliwa na hatukutawaliwa kwa muda mrefu kama wengine.
Uingereza ilikaa India zaidi ya miaka 150 hata British empire ni shauri ya India, China - Hong Kong wameaondoka juzi kati tu.

Laana hii imepelekea sisi Waafrika kumuona Mzungu kama siyo equal wetu na kwamba ana deni la kutulipa.

Ni kama kijana anayemlaumu Baba yake kwa kushindwa kwake maishani, kwamba hakumsaidia ndo maana anashindwa.

Sasa tuvunje hii kete ya laana walioturithisha kizazi cha kwanza.

Tuanze kumuona Muzungu kama competitor wetu na siyo baba tunayemlaumu kwa kila kitu maishani mwetu, ...

Uwezo wa akili ndiyo UKUBWA na NGUVU, Angalia Tembo na Binadamu ndipo unaweza kujifunza hapo.
 
Mzungu ni dhulumati amechamgia kwa 50% udumavu wa maendeleo ya Africa

Mpaka sasa bado wanaihujumu Africa
 
Mzungu ni dhulumati amechamgia kwa 50% udumavu wa maendeleo ya Africa

Mpaka sasa bado wanaihujumu Africa

Na hiyo 50% nyingine iliyobakia amechangia nani? Isitoshe kwa nini ahujumu Afrika tu wakati ametawala sehemu nyingi Duniani zikiwemo India, Vietnam, Malaysia, Singapore, Indonesia, Hong Kong na kwingineko?
 
Africa walikubali defeat kutoka kwa hawa Mabeberu kirahisi mno Ukiondoa mtawala wa mansa musa
Africa tilikuwa mbali sana tilikuwa tunapiga hatua kwa kasi kubwa ila walipokuja walivuruga kila kitu

Lkn usisahau Afrika Mzungu hajakaa sana ukilinganisha na sehemu nyingine kama Asia, India Mzungu amekaa zaidi ya miaka 150 na kwingineko.
 
Mkuu unajichanganya sana
Mzungu mpaka leo bado Yupo Africa unaposema hajakaa sana unamaanisha nini?

Angalia walivyomshughulikia Mugabe alipojaribu kuirudisha ardhi kwa Wananchi
Angalia Africa kusini Ardhi ni mali ya Mzungu
Angalia Congo mfaransa anavyoichezea

Na alituweza alipotuletea demokrasia ya kishenzi kabisa

Nchi za Africa hizi demokrasia hazina faida kwa Wananchi ila zinafaida kwa wazungu

It is either democracy or defeated from office
Lkn usisahau Afrika Mzungu hajakaa sana ukilinganisha na sehemu nyingine kama Asia, India Mzungu amekaa zaidi ya miaka 150 na kwingineko.
 
Tunafanya kosa lilelile kwa kuwalaumu kina Nyerere kuwa ndiyo wametuletea utegemezi kwa kudai matatizo yetu yamesababishwa na utumwa na Ukoloni. Wakoloni hawajasababisha tatizo lolote, walikuja kwa ajili ya kutafuta malighafi za viwanda vyao. Lakini baadae wakaondoka baada ya kuweka mfumo wa kupata wanachokitaka bila wao kuwepo hapa.

Kuanzia elimu yetu mpaka upatikanaji wa Viongozi wetu ni kutokana na mfumo wao uliosukwa vyema.

Tunachotakiwa kufanya ni kujitambua na kuangalia ni kipi tunacho na namna tunaweza kukitumia kujikwamua.

Hakuna Taifa ambalo halijawahi kupitia madhila ya namna moja ama nyingine. Inabidi tuitumie Historia yetu kujifunza tu na kusonga mbele.
 
Back
Top Bottom