Uchaguzi 2020 Kosa kubwa walilofanya CCM kwenye kampeni zao ni kupoteza muda kusifia yaliyopita badala ya kueleza watafanya nini

Ccm ya bashiru,mahera na polepole awakutegemea kabisa ujio wa Lisu walikuwa wamejiandaa kupita bila kupingwa, thus pumzi imekata majukwaani hawana sera, wanarudia rudia waliyoongea miaka 5 sgr, corona, ndege, flyover Hadi vijijini ambapo havina msaada kwao
 
kigogo.jpg
 
CCM walikua wanasafisha njia kwa uongo na ulahai wenu mlowalisha wananchi katika kampeni.

Kwamba ndege,ujenzi wa nchi,maendelo ya vitu hayaitajiki nchi hii.

Hapo ndo watu wakawaona nyinyi kweli Ni mwezi mchanga
Unaandika utafikiri unasombwa na maji.
 
Re
Mitano tena ya Bombardier
Mitano tena ya Meli na vivuko
Mitano tena ya barabara
Mitano tena Madaraja
Mitano tena ya Masoko ya kisasa
Mitano tena ya Shule
Mitano tena ya hospitali na vituo vya afya na zahanati
Mitano tena ya kukamilisha SGR
Mitano tena ya SMEs
Mitano tena ya ajira za elimu,afya,fundi mchundo
Mitano tena ya Umeme Imara na vijiji vyote
Mitano tena ya pembejeo za Kilimo
Mitano tena ya chanjo za kizalendo za mifugo
Mitano tena ya miundombinu ya IT
Mitano tena ya Utalii wa kiutamaduni
Mitano tena ya AFCON na World CUP.

KWA CCM UTEKELEZAJI NI AHADI.
CHAGUA JPM
Review jina lako dadangu.
 
Kuna swali limulizwa. Wakati jiwe anaingia nauli za fast jet kutoka Dar Mwanza ilikuwa 70,000 tu! sasa ni 400,000!

Sukari ilikuwa 1800tu! sasa ni 3000-3500
MAUZO YA MAZAO
Pamba ilikuwa inauzwa 2500@kg sasa ni 1200 na wanunuzi wote ni makada wa ccm!!

Kahawa ilikuwa inauzwa sh 2500-3000@kg, sasa inauzwa 1200

Kwa kifupi. Magufuli ameua uchumi wa nchi yetu!!! lazima aende!!!
MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUPIGA KURA TAREHE 28 OKTOBA.
------------------------------------

1. Miaka mitano iliyopita hatukua na Zahanati kila Kata, sasa kila Kata nchi nzima kumejengwa Zahanati.

2. Miaka mitano iliyopita watumishi walikua wanapata mishahara yao tarehe tatu hadi tano ya mwezi unaofuata. Sasa kila tarehe 23 siku saba kabla ya mwezi kuisha mshahara umelipwa.

3. Miaka mitano iliyopita Machinga na Mama Ntilie walikua wanafanya biashara kwa tabu na manyanyaso makubwa, sasa wanaheshimika na biashara zao zimehalilishwa kwa tsh. 20,000/= kwa mwaka.

4. Miaka mitano iliyopita Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu walikuwa wakipata pesa za boom wiki tatu hadi nne baada ya kusain. Sasa ni express siku tatu hadi tano kwisha kusaini pesa imejaa ktk akaunt bila usumbufu wowote.

5. Miaka mitano iliyopita tulipoteza mabilioni ya pesa kwa ajili ya foleni katika jiji la Daslamu, kwa sasa alhamdullah foleni zimepungua na zinakwenda kuisha kabisa baada ya ujenzi wa njia NANE na Flyovers, Tazara na Ubungo.

6. Miaka mitano iliyopita Ziwa Victoria kulikua na Meli moja tu ambayo pia ilikua imechakaa, hivi tunazungumza Meli Mpya ya NEW VICTORIA inachana mawimbi Mwanza to Bukoba na nyingine nyingi zimekamilika, Ukerewe, Ukara Ruvuma, Kilwa nk.

7. Miaka mitano iliyopita tulikua hatuna Ndege ya Serikali hata moja, yaani hata ya dawa lkn kwa sasa zipo zimetapakaa ktk anga la Tanzania Ndege NANE kwa hewa.

8. Miaka mitano iliyopita vijijini waliusikia UMEME kwenye redio lakn sasa hadi bibi yangu Kisiwani Kome anawashia UKUTANI. Tumeongeza uzalishaji kutoka megawati 1308 hadi megawati 1602.32. Bado ule wa Mto Rufiji, haya ni maajabu yanayostahili heshima kubwa.

9. Miaka mitano iliyopita maji ya bomba ilikua ni ndoto katika baadhi ya mikoa nchini, sasa mtandao wa maji umeongezwa kwa nchini nzima na tunaendelea kusambaza ili maji safi na salama yawafikie Wananchi ktk maeneo yote.

10. Miaka mitano iliyopita RUSHWA ilikua ni donda ndugu, bila kidogo hupati huduma hata kama ni haki yako. Miaka mitano baadae taratibu tunaendelea kunyooka, rushwa inapungua na haki inapatikana kwa halali.

11. Miaka mitano iliyopita kulikua na utitiri wa tozo na KODI katika biashara ya mazao. Sasa ni free of charge gunia la kilo 100 safirisha uwezavyo Tunduma hadi Ukerewe.

12. Miaka mitano iliyopita Watumishi wa Umma wote walikua KAMBALE, hakuba mkuvwa wala mdogo wote walikua na ndevu. Kama humfahamu utamfahamu, walikua hawaambiliki wala kugusika, sasa kila mtumishi wa Umma ni mfanyakazi wa Mwananchi. Sasa nidhamu imerudi na heshima ipo kazini.

13. Miaka mitano iliyopita wachimbaji wagodo wa Madini hawakutambulika katika ardhi ya kwao, sasa wanatambulika kwa leseni, wamepatiwa vitalu vya kuchimba madini ili wajipatie kipato. Katika hali hii kuna mtu anataka kuweka rehani MADINI, hakikisha unapiga KURA kwa CCM kutoa ujumbe kuwa madini yetu ni mali yetu.

14. Miaka mitano iliyopita Reli ya Kanda ya Kati haikua na mbadala wake, siku tatu Dar hadi Mwanza. Sasa karibuni kutakua na mtambo wa kusaga na kukoboa unaitwa SGR, yaani saa saba tu umetoka Mwanza unakula lunch Silver Paradise Hotel pale TIPTOP Daslam.

15. Miaka mitano iliyopita Salender haikufikiriwa kuwa na daraja la baharini, busisi ilikua ndoto kuweka daraja ziwani, sasa mda si mrefu tutakua tunachagua wenyewe kupita katikati ya maji au barabarani. This is wonders brothers and Sisters.

16. Ni hivi; miaka mitano iliyopita ilikua ya kwetu. Tulifanya tukaisha hapo, sasa tumesogea zaidi ya pale. Tunaomba miaka mingine mitano tupige hatua kubwa maradufu!

Orodha ni ndefu, Oktoba 28, piga KURA kwa Diwani wa CCM, Mbunge wa CCM na Rais wa CCM kazi iendelee!!!
Utakosa PEPO bure, kuwa muungwana tumefanya mambo mengi mazuri kwa miaka mitano tunastahili KURA yako.
#MitanoTena!
 
Nani alikuambia CCM wana akili? Kwa ubongo ipi? Na uongozi upi? Haya majamaa yaitwayo Bashiru, Polepole, na Jiwe ndiyo think tanks za chama? Utasubiri sana.
Hakuna mtu mwenye akili kubwa anaweza kuishi ndani ya CCM. Hakuna super intelligent ndani ya CCM. Msifanganyike na titles za Drs au Profs. Wapo Drs na Profs low minds pia. Na hao ndio wapo ndani ya CCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kawaida na hulka ya binadamu ni kutamani kusikia au kuona kitu kipya kuliko cha zamani, wazungu wanasema test the difference.

Tangu kampeni zianze CCM wamekuwa wakipoteza muda mwingi kuelezea vitu walivyo fanya wakasahau kuwaeleza wapiga kura nini kipya watawafanyia wananchi endapo watachaguliwa tena.

Kwenye kampeni zao mara nyingi utawasikia tumejenga hiki, tumenunua hiki, tumejenga flyover, tumenunua ndege, tume... tume... zilikuwa nyingi, vitu ambavyo tayari watu wanavijua, inaboa, ndio maana baada ya wasanii kumaliza watu walikuwa wanaondoka kwa sababu wanajua wataambiwa yaleyale ya jana, nashangaa kwanini kampeni meneja alikuwa haja notice hilo.

Tofauti na Chadema ukienda kwenye kampeni zao walikuwa wanasema mkituchagua tuta fanya hiki, tutabadili hiki... tuta... tuta... hadi hotuba inaisha bado unawaacha watu na hamu ya kusikiliza wakidhani labda utasema kingine kipya.

Kampeni ni tofauti na hotuba au mahubiri ya kanisani ambapo waumini wanajua lazima utawaambia juu ya Yesu kurudi, kampeni ni technique ushawishi sio kutumia nguvu na kulazimisha watu wakusikilize, matendo kama ya kina Sabaya hayaongezi kura badala yake yanajenga chuki na kuipunguzia kura CCM.
Chama chochote ambacho kipo madarakani lazma kieleze yaliyo waahidi wananchi kipindi kilichopita yametelezwa KWa kiasi gani na wanaahidi nini KWa kipindi kijacho na CCM inaongozwa na ilani ndio mwongozo wetu Sio nyie sera zenu Lila siku ni umbea tu na sio kusema nini mtawafanyia wananchi KWa hiyo anachofanya magufuli ni kuwaonesha wananchi vile alivyoahidi ametekeleza lakini pia ilani inayotugwa inazingatia Changamoto za wananchi
 
Lisu ni mpango wa Mungu, hayo yote lazima yatokee ili kuwepo na utimilifu wa neno la Nyerere, kwamba, wakuitoa ccm ni ccm wenyewe,
Nimeamini maneno hayo kwani naona kabisa akina
@Hpolepole
@AllyBashiru
@KheriJames
@DkMagufuri
@DcSabaya

Ndiyo wataiangusha ccm kwa vimbwanga wanavyovionyesha wazi na vimeongeza chuki kwa wananchi
Tundu lissu kama shetani anashawishi watu kwenye mabaya
 
Kosa kubwa ni kuikabidhi Tanzania kwa mtu anayejiita MWENDAWAZIMU Mkuu. Huwezi kukabidhi Nchi kwa MWENDAWAZIMU halafu utegemee Watanzania waendelee kukupenda. Sasa wanaweweseka wanaona maji yanazidi UNGA ni mdebwedo tu.
Kawaida na hulka ya binadamu ni kutamani kusikia au kuona kitu kipya kuliko cha zamani, wazungu wanasema test the difference.

Tangu kampeni zianze CCM wamekuwa wakipoteza muda mwingi kuelezea vitu walivyo fanya wakasahau kuwaeleza wapiga kura nini kipya watawafanyia wananchi endapo watachaguliwa tena.

Kwenye kampeni zao mara nyingi utawasikia tumejenga hiki, tumenunua hiki, tumejenga flyover, tumenunua ndege, tume... tume... zilikuwa nyingi, vitu ambavyo tayari watu wanavijua, inaboa, ndio maana baada ya wasanii kumaliza watu walikuwa wanaondoka kwa sababu wanajua wataambiwa yaleyale ya jana, nashangaa kwanini kampeni meneja alikuwa haja notice hilo.

Tofauti na Chadema ukienda kwenye kampeni zao walikuwa wanasema mkituchagua tuta fanya hiki, tutabadili hiki... tuta... tuta... hadi hotuba inaisha bado unawaacha watu na hamu ya kusikiliza wakidhani labda utasema kingine kipya.

Kampeni ni tofauti na hotuba au mahubiri ya kanisani ambapo waumini wanajua lazima utawaambia juu ya Yesu kurudi, kampeni ni technique ushawishi sio kutumia nguvu na kulazimisha watu wakusikilize, matendo kama ya kina Sabaya hayaongezi kura badala yake yanajenga chuki na kuipunguzia kura CCM.
 
Kawaida na hulka ya binadamu ni kutamani kusikia au kuona kitu kipya kuliko cha zamani, wazungu wanasema test the difference.

Tangu kampeni zianze CCM wamekuwa wakipoteza muda mwingi kuelezea vitu walivyo fanya wakasahau kuwaeleza wapiga kura nini kipya watawafanyia wananchi endapo watachaguliwa tena.

Kwenye kampeni zao mara nyingi utawasikia tumejenga hiki, tumenunua hiki, tumejenga flyover, tumenunua ndege, tume... tume... zilikuwa nyingi, vitu ambavyo tayari watu wanavijua, inaboa, ndio maana baada ya wasanii kumaliza watu walikuwa wanaondoka kwa sababu wanajua wataambiwa yaleyale ya jana, nashangaa kwanini kampeni meneja alikuwa haja notice hilo.

Tofauti na Chadema ukienda kwenye kampeni zao walikuwa wanasema mkituchagua tuta fanya hiki, tutabadili hiki... tuta... tuta... hadi hotuba inaisha bado unawaacha watu na hamu ya kusikiliza wakidhani labda utasema kingine kipya.

Kampeni ni tofauti na hotuba au mahubiri ya kanisani ambapo waumini wanajua lazima utawaambia juu ya Yesu kurudi, kampeni ni technique ushawishi sio kutumia nguvu na kulazimisha watu wakusikilize, matendo kama ya kina Sabaya hayaongezi kura badala yake yanajenga chuki na kuipunguzia kura CCM.
Bila kuyasahau matendo ya mbeleko wanazo tumia ambazo zinagharimiwa na walipakodi bila ya ubaguzi,huyu wa Kule na huyu was huku.pia Zina gharama kubwa zaidi ya faida kwao.
 
piga KURA kwa Diwani wa CCM, Mbunge wa CCM na Rais wa CCM kazi iendelee!!!
Utakosa PEPO bure, kuwa muungwana tumefanya mambo mengi mazuri kwa miaka mitano tunastahili KURA yako.
#MitanoTena!
Mitano KWANZA kwa TAL ndo habari ya mujini mkuu..

Ni YEYE 2020-2025
 
Mtandao jipeni moyo Ila mtaani uhalisia mnaujua na mnajua rais ni nan anakuja achana na kibaraka wenu huyu naye wengi tunamkubali hapa Ila mtaani siku ya kura mkijua hatumpi
 
Lissu hawezi kuja kuwa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Sio 2020 bali ni kamwe (NEVER). CCM sio wajinga wapo jikoni wanaset mitambo wakati nyie mmekazana na Mambo yasiyo na impact mpo bize kushangilia helicopter aliyokodi Lissu. Kwa akili hizi za kujipa moyo CCM itaondoka madarakani miaka 50 ijayo.
Kwa hiyo unaunga mkono kupata viongozi kwa set mitambo kuliko wakaeleza sera zao na kuchaguliwa kwa umahiri wao ambao wataleta maendeleo kwa watu waliowaweka madaraka.

Usiwe na tabia/mawazo ya dhuruma. Waza haki,tendea haki.
 
Kulikuwa na ndege za FASTJET,
Dar - Mwanza ilikuwa sh elfu 70, sasa jiwe kaua Fastjet ameleta madege ya Bombadier ya kinyonyaji, Dar - Mwanza kwa sasa ni sh laki 4, afu jiwe anawadhihaki wanyonge kuwa anawasaidia!
Kabisa mzee,kusafiri kwa ndege enzi za fastjet haikuwa anasa. Sasa jamaa wameturudisha huko,watu wanaosafiri kwa ndege wanaonekana ni matajiri na wanafanya anasa.

Hakika tumerudi miaka ya 60.
 
Lissu naye aanze kueleza yajayo - shule, maji, kipato, kilomo, ufugaji, mikopo ya wanafunzi, maji, umeme, afya, nk. Anapoteza muda mwingi kwenye ukatili wa watawala.
 
Lissu hawezi kuja kuwa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Sio 2020 bali ni kamwe (NEVER). CCM sio wajinga wapo jikoni wanaset mitambo wakati nyie mmekazana na Mambo yasiyo na impact mpo bize kushangilia helicopter aliyokodi Lissu. Kwa akili hizi za kujipa moyo CCM itaondoka madarakani miaka 50 ijayo.
Tukipiga kura tutazilinda ili kuzuia maboksi yenu ya kura fake kuingizwa vituoni, safari hii hamna pakutokea wapuuzi nyie.
 
Back
Top Bottom