Kosa kubwa tulilolifanya, na kwanini tunasahihisha 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kosa kubwa tulilolifanya, na kwanini tunasahihisha 2010

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 4, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 4, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  [​IMG] [​IMG]

  Ningeweza kutumia maneno mengi kuelezea kosa hili ambalo hata hivi sasa bado tunalifanya lakini hatuna budi kujisahihisha kama mabadiliko tunayoyataka yataweza kupata nafasi yoyote. Kosa hilo ni kosa ambalo hatujaona ubaya wake na ni nafasi hii kutafakari kama kuendelea nalo tunaendelea kujihukumu sisi wenyewe na uzao wetu kwenye utegemezi na uombaomba wa kudumu.

  Kosa tulilolifanya ni Kuwaachia wanasiasa wetu kuendelea kutengeneza ajenda za kisiasa kwa taifa letu na kutuletea sisi wananchi; tumewaacha waandike ilani zao na kutuletea sisi; tumewaacha wao waamue nini tunataka halafu wanatuomba kura kwa msingi huo..

  Nasema sasa yatosha; 2010 "sisi wananchi wa Tanzania mahali popote tulipo na katika hali zetu zote tulizonazo, tutaamua tunataka nini, lini, na kwa namna gani; tutauza ajenda hiyo kwa wanasiasa wetu na ni kwa msingi huo ndio tutawachagua".

  Sijali tena CCM itaahidi nini; sijali CUF wataahidi nini; sijali Chadema wataahidi nini au watakuja na ilani gani. Wakati huu wao ndio watagombania kile tunachokitaka ili watuletee kwa namna tunayotaka.

  Kwa maneno mengine, hatima ya kisiasa na kiuongozi ya nchi yetu tunataka kurudisha mikononi mwa wananchi wenyewe.
   
 2. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Kama utaweza kuwaelimisha wananchi hayo mawazo yako yanaweza kufanikiwa. Otherwise kwa ninavyowafahamu waTZ akuna jipya. Ndiyo sababu CCM wamepeta na 93 % serikali za mitaa.
   
 3. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Siku zote katika jamii yoyote lazima kuwe na watu wanaofikiri kwa niaba ya wengine halafu wauze yale mawazo kwa watu. kama yanakubalika wanapewa dhamana ya kutekeleza.

  I would expect chaos if every single Tanzania will be selling his ideas to politicians for implementation. How could it be documented?

  I would expect to have a forum of elite Tanzanias to come out with proposals for what tanzanians need and what are the priorities of our nation.
   
 4. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #4
  Jan 4, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Ninachoamini adui wa maendeleo ya kisiasa Tanzania ni wasomi, hawashiriki siasa, waoga, wanapenda kunyenyekea, aibu tupu.

  U
  kitaka kuamini maneno yangu angalia takwimu za ushindi wa CCM mijini ambako kunawatu wengi wenye elimu ya uraia, kweli ni aibu tupu, maeneo yote kuzunguka vyuo vya elimu ya juu ndipo ambako CCM ilishinda kwa kishindo zaidi.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jan 4, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  we are going to change this; we have to if we really to leave to our children a better country than we have today. Change we must.
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  Jan 4, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  kama Raia Watanzania tutakua na roho ngumu ya kutoogopa mabadiliko kisiasa kweli tunaweza kubadilisha utawala huu uliovuruga maisha yetu na ustawi wa kizazi chetu kijacho.
  lazima wanasiasa na wasio wanasiasa tukubali kujitoa muhanga, tukubali kupoteza kwa faida ya vizazi vyetu vya leo na kesho, tukiwaachia hawa kina Mrema Lyatonga hatima yetu kisiasa na kimaendeleo tumekwisha. kweli tuamke ,tufunge vibwebwe, tuache siasa za habari maelezo na kwenye magazeti, tuunganishe nguvu kwa pamoja, tutawang'oa watawala hawa na vibaraka vyao.
   
 7. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280

  Mwanakijiji acha utani bwana. Before we start thinking of the future generation we should first think of ourselves. Are we really better now now than before. If we are failing to improve our situatioan now how can we prepare better future for our children??
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jan 4, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Zero.. ukifikiria sasa hivi utaishia kujinufaisha sasa hivi tu; na hii ni mojawapo ya tofauti kati yetu na wenzetu walioendelea; wao wanaangalia mapungufu waliyonayo leo hii na wananuia kurekebisha sasa hivi ili watoto wao na uzao wasikutane nayo huko mbeleni. You see, when you think about your children you start changing right now; if you are content now then you don't need to prepare for now for "tomorrow will look afteritself".. Hujajiuliza kwanini wazungu wameng'ang'ania climate change wakati sasa hivi hatuoni madhara yake makubwa..?
   
 9. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #9
  Jan 4, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  katika ulimwengu wakufuta ujinga na kupambana na umasikini inasikitisha kuona hadi leo Waafrika tunafikiri leo tunakula nini, leo tunajengs nini, leo tunaanzisha nini, mipango yetu haizidi miaka hamsini, tuko hobelahobela kila mtu na lwake.
  hatuna viona mbali kama wenzetu wa magharibi, wao huyatazama maisha katika miaka ya kizazi kijacho......maana kizazi hiki waliishaandaliwa maisha .
  Hubu angalia harakati za kina LIVINGSTONE,STANLEY na wachunguzi wengine kabla ya ukoloni, hawakujali mmbu,nzi ,wanyama wakali wala nini, walijituma kwa manufaa ya nnchi yao miaka mingi baadae, angalia hatari na changamoto za kina columbus n wenzao, walisafiri kwenda maili nyingi na kwao kwa manufaa ya vizazi na vizazi vijavyo.
  sasa lazima Watanzania na Waafrika kwa ujumla wao tuanza kufikiri zaidi ya upeo wa kizazi chetu, tufungue mageti ya uwoga, tuwaandalie maisha bora watoto wetu miaka zaidi ya hamsini ijayo.
   
 10. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Vikundi vya kijamii vimeshaanza kuja na Ilani na Miongozo yao, nadhani hicho unachosema Mwanakijiji kimeshaanza kufanyika ingawa Watawala wamekuwa mbogo. Hata hivyo, hizo Ilani na Miongozo ya vikundi hivyo kwa kweli inashangaza sana na kusikitisha-wanajitanguliza wao na maslahi yao na watu wa jamii yao (Rejea Mwongozo wa Shura ya Maimamu) badala ya Watanzania. Ikiwa kila kikundi kitakuja na hizo Ilani na Miongozo yao tutaishia wapi na tukubali Ilani/Mwongozo wa nani kuwa ajenda ya Wananchi?
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Jan 4, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  nguvumali.. unajua nchi kama Marekani hawajawa na miradi mikubwa ya barabara ya kitaifa kwa miaka mingi sana.. hizi highway tunazoziona sasa hivi zilijengwa miaka ya hamsini.. leo hii ni kupanua tu hapa na pale.. kumodernize madaraja n.k.. sisi bado tunahangaika na Ubungo na traffic lights zake!
   
 12. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Vikundi vya kijamii vimeshaanza kuja na Ilani na Miongozo yao, nadhani hicho unachosema Mwanakijiji kimeshaanza kufanyika ingawa Watawala wamekuwa mbogo. Hata hivyo, hizo Ilani na Miongozo ya vikundi hivyo kwa kweli inashangaza sana na kusikitisha-wanajitanguliza wao na maslahi yao na watu wa jamii yao (Rejea Mwongozo wa Shura ya Maimamu) badala ya Watanzania. Ikiwa kila kikundi kitakuja na hizo Ilani na Miongozo yao tutaishia wapi na tukubali Ilani/Mwongozo wa nani kuwa ajenda ya Wananchi?
   
 13. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #13
  Jan 4, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  MKJJ,

  Nafikiri hukunipata sawasawa. My point hapa ni kuwa hali ya sasa ni mbaya na inaendelea kuwa mbaya. Kwa sisi kuweza kuprepare a better future for the next generation inatakiwa turekebishe hali ya sasa kwanza!!!
   
 14. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #14
  Jan 4, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...Una maana kubadilisha constitutional rights? ...labda baada ya miaka 100 kuanzia sasa!

  'Rights' ndogo ndogo ambazo zingeweza kubadilishika, zimehujumiwa kiasi kwamba Elimu ya uraia haikusudiwi tena kuwafikia walengwa, ila wahitimu wachache wa Sheria walioshika hatamu za uongozi. Ubaya na wao hutumia udhaifu huo kwa manufaa ya matumbo yao.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Jan 4, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  nilikuelewa vizuri kweli bila ya shaka; jibu langu ni kuwa hicho unachosema ndicho tumekuwa tukikifanya kwa miaka karibu hamsini sasa; kujaribu kushughulikia matatizo ya sasa ili tuondokane nayo sasa.

  Hivyo, tutaziba shimo la barabarani ili tusipate taabu sasa hivi
  Tutaweka gogo barabarani wakati wa mvua ili tuweze kupita sasa hivi
  Tutaongeza ujenzi wa shule nyingi ili tuongeze wanafunzi zaidi sasa
  n.k

  Motivation ya "sasa" ni mbaya sana kwa sababu ni kama ya kumridhisha mtoto kwa kumrushia nyonyo akilia na hivyo kuondoa tatizo la njaa yake ya sasa.. huku mtu hana uhakika kesho mtoto akikua atakula nini!
   
 16. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #16
  Jan 4, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  MM,
  how are you going to implement the strategies?....

  by typing only??????....
   
 17. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #17
  Jan 4, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280

  Nafikiri hata hawa wazungu walianza vilevile, kutatua matatizo waliyonayo kwanza. Tofauti yetu na wao sisi tukiweka gogo leo ili tupite kwenye mvua ikinyesha tunasahau mpaka msimu ujao tena wakati wenzetu baada ya kuvuka kwenye gogo wanaanza kufikiria kuweka daraja ili msimu ujao wasihangaike kutafuta gogo jingine.
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Jan 4, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  words have more power than swords.. unafikiri tumefikia hapa kwa kulima?
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Jan 4, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  I'll argue differently.. wao wanapoweka gogo leo wanafikiria kuwa litawasaidia na baadaye na huko mbeleni.. hivyo watachagua gogo la aina gani, lenye sifa gani na lenye kukidhi mahitaji gani ya sasa na ya mbeleni. Hivyo wanapotatua tatizo lao la "sasa" wakati huo huo wanatatua tatizo lao la baadaye. Sisi tunatenganisha (kama ulivyojaribu) kuwa tutatue matatizo ya sasa kwanza halafu tukishayatatua tufikirie namna ya kutatua matatizo ya baadaye.. this as I have pointed out, is what we have been doing for almost 50 years..

  guess what happens? tunajikuta bado tuna matatizo ya jana!
   
 20. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #20
  Jan 4, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  BUT finally watu wanatakiwa kushika hayo mapanga!......
  hapo kwenye kulima umenikumbusha kwetu kalenga!
   
Loading...