Kosa kubwa la serikali ya awmu ya kwanza kwa watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kosa kubwa la serikali ya awmu ya kwanza kwa watanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Salary Slip, Jun 1, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,022
  Likes Received: 37,755
  Trophy Points: 280
  Binafsi ktk moja ya mambo ambayo mpaka leo yananisikitisha kuhusiana na serikali ya awamu ya kwanza chini ya mwalimu Nyerere ni kutoruhusu mfumo wa vyama vingi.Wako watanzania wengi wanaamini kuwa Nyerere hakufanya makosa ingawa yeye mwenyewe binafsi alikiri ktk moja ya hotuba zake kuwa kuna mambo ya kijinga yalifanywa chini ya uongozi wake na moja kati ya hayo mimi nasema ni kuminya demokrasia ya vyama vingi.
  Watanzania wa leo tujiulize ktk hali ya sasa ya ufisadi na wizi wa kutisha ambao bila shaka ulikuwepo tangu enzi za mwalimu kusingekuwa na hofu ya upinzani kukishinda chama tawala hali ingekuwaje?Nyere aliligundua jambo hili na ndio maana alitumia ushawishi wake kutaka uwepo mfumo wa vyama vingi.
  Hata ktk serikali ya awamu ya kwanza tulitakiwa kuwa na mfumo wa vyama vingi kwani mfumo huo ungeongeza uwajibikaji wa watawala kwa hofu ya kupokonywa madaraka na wapinzani.Tukumbuke waliobuni mfumo wa vyama vingi hawakuwa wajinga bali waliona faida zake ambazo naamini hata sisi watanzania wa leo tunaziona.Ni mtanzania gani makini wa leo anaweza kubeza mchango wa wapinzani ktk kulinda na kutetea rasilimali za watanzania?Tazama wabunge wa upinzani wanavyosaidia taifa hili linaloporwa kila kukicha.
  Sasa tafakari mwenyewe ni hatua kiasi gani tungekuwa tumepiga kama taifa endapo mfumo wa vyama vingi ungekuwepo tangu enzi za baba wa taifa.
  Ni jambo la kusikitisha na hasara kubwa kwa watanzania licha ya mazuri ya kuigwa ya marehemu baba wa taifa.Hata hivyo tumsamehe bure kwa kulinganisha na mengi mazuri aliyoyafanya kwa taifa hili.Bali si dhambi kujua uzaifu wake.
   
Loading...