Kosa kubwa la Malecela wa NIMR: Rais kaona mbali athari za ZIKA

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
579
Zika na NIMR

Dk. Mwele Ntuli Malecela leo si Mkurugenzi tena wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). Ikulu leo imemtangaza Profesa Yunus Mgaya kuwa mbadala wake.

Kwanini Mwele kaondolewa? Nimeulizwa hili swali na baadhi ya watu nami nikauliza hapa na pale ili kupata majibu. Na hili ndilo nililoambiwa.

Mosi, kwamba ugonjwa wa Zika upo Tanzania. Ugonjwa huu ulianzia Uganda na upo pia kwetu kwa muda mrefu. Ila upo katika hali iliyodhibitiwa, wataalamu wanaitwa Endemic. Si tatizo kubwa lakini upo.

Lakini Tanzania haina tatizo la ZIKA. Kwa jinsi tatizo la ugonjwa huo lilivyo kubwa, kabla halijatangazwa, kuna taratibu za kufuatwa ikiwamo kuhusisha Serikali na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Imefanyika hivi kwa sababu madhara ya kutangaza ugonjwa huo kwa taifa ni makubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Tatizo ni kwamba tangazo la Mwele halikufuata hizo taratibu. Na zaidi, halikuzingatia athari ambazo zingejitokeza kwa yeye kutoa taarifa kama zile.

Kwenye Kiswahili, tofauti ya maneno Endemic na Epidemic ( ugonjwa uliodhibitiwa na uliolipuka) ni ndogo. Ukisema Zika ipo, magazeti yatasema ZIKA imeingia.

Sasa, labda, Rais mwingine, kwenye Serikali nyingine, angeweza ˊkupotezea` tu kauli ile ya Mwele. Lakini binti huyu wa mzee John Malecela hakuwa amesoma vema alama za nyakati.

Hivyo, kwa maana ya kosa, Mwele alikosea. Ishu ya ZIKA haikuwa ya kutangazwa na taasisi yake pekee bila kuhusisha serikali na wadau wengine.

Hivyo, hapa, tatizo si serikali kukataa taarifa ya kitaalamu. Ni kwamba mhusika amekiuka taratibu ambazo zimewekwa. Na huo ugonjwa haujaja sasa hivi. Upo siku nyingi ila umedhibitiwa.
 
Yeye katangaza tafiti ya kisayansi, na anatangazaga kila siku. Hivi mwananchi wa kawaida utataka kujua kuwa ugonjwa upo? au utataka kujua aliyesema ni nani? Kwangu ni bora nijue ugonjwa upo ili nichukue tahadhari, sio mnifiche kwa kigezo cha kuusubiria uwe epidemic ili mimi ndio niwe statistic
 
hakuna kosa lolote alilofanya zaidi ya kudidimiza ubunivu na kujituma kwa wafanyakazi wetu , na hii si dalili njema kwa watendaji wa serikali
 
Sidhan atua alizochukuliwa ni stahili.
Ilipaswa watafute siku nyingine waweke Mambo sawa.

Sasa sipati picha ugonjwaa huu ukilipuka sijui huyo Pogba atasema nini?


Mbona hapo Uganda inatambulika ZIKA ipo lkn mnayosema sijui matatizo ya kiuchumi, kijamii hatuyaoni?

Tuache Ushamba!!
 
Kolimba-ccm imekosa dira-kafukuzwa
Mafuru-hakuna mshahara wa milioni 40
Mwele malecela-kuna zika
 
Hiv? Alitoa matokeo ya tafiti au alitangaza kuwa ugonjwa upo? Mi sioni shida kama alitoa tu matokeo ya utafiti uliofanyika
 
Yeye katangaza tafiti ya kisayansi, na anatangazaga kila siku. Hivi mwananchi wa kawaida utataka kujua kuwa ugonjwa upo? au utataka kujua aliyesema ni nani? Kwangu ni bora nijue ugonjwa upo ili nichukue tahadhari, sio mnifiche kwa kigezo cha kuusubiria uwe epidemic ili mimi ndio niwe statistic

Umechukua tahadhari gani mpaka sasa?
 
Back
Top Bottom