Kosa kubwa ambalo chadema inafanya!

Lazima nijenge msingi imara wa arguments zangu kwa kushirikisha maoni mbalimbali kutoka kwa watu mbalimbali. Jukumu la kujenga CDM imara si la wanasiasa pekee ni jukumu la wapenda mabadiliko. In such sijaongea siri yoyote ambayo ni muflisi kwa cdm bali ni ukweli kamili ambao lazima ufanyiwe kazi.

Pia CDM imejikuta imecopy muundo mzima wa CCM bila ya kujali kuwa haina raslimali wala uzoefu wa kuhimili changamoto zitokanazo na muundo.
 
Wapo akina mama au wanawake wengi ambao hawahitaji uongozi ila wanahitaji kukombolewa kifikra.Tuwaangalia akina Halima Mdee na wenzake ambao ni wabunge wanaifanyia nini CHADEMA na Tanzania kwa ujumla.Ningemuomba Halima Mdee na wenzake wawangalie wanawake kama chachu ya maendeleo.Je kwenye ofisi za kanda au wilaya nafasi za wanawake zikoje? CCM inaweza kuhonga jamani wanawake ni rahisi kuhongwa sababu ya uchumi na elimu duni.Akina Halima ,Josephine aka First Lady anzeni sasa halafu tukiona juhudi zenu tutasaidia pale panapo stahili.
 
Umejitahidi kutoa mawazo ya kufikirisha. Lakini unapoweka mkazo kwenye ujenzi wa chama tokea chini kwenda juu basi ni bora ukaelezea kivipi katika mazingira halisi ya nchi yetu. Ulichoandika katika aya ya kwanza inabidi ukipe uzito unaostahili. Bila shaka unaelewa kuwa sehemu kubwa ya nguvu za kiuchumi za CCM si toka vyanzo halali na matumizi yake ni ya kifisadi hata katika siasa. Aidha, mitandao yake na hizo taasisi ulizotaja si muafaka kwa utawala bora. Hapo ndipo lilipo tatizo kubwa si kwa CDM tu bali kwa vyama vyote vya upinzani na ujenzi wa demokrasia ya kweli nchini.

Kuhusu kujenga chama tokea chini sidhani kama inaweza kutokea bila kubata hamasa toka juu. Inabidi viongozi wa juu wenye mvuto waende chini kuwapiga tafu na kwaandalia mazingira ya utendaji makada wanaochipukia kisha kuwaacha waendelee huku kukiwa na mawasiliano mazuri ya mashauriano. Tatizo linaweza kuwa kama viongozi wa juu wanadhibiti na kuingilia madaraka ya ngazi za chini wakati wote isivyostahili.

Kwa upande mwingine, kwa mazingira ya sasa, sidhani kama CCM na mitandao yake inayohusisha vyombo vya dola itaachia ujenzi wa vyama vya upinzani ufanyike huko ngazi za chini kwa amani. Usidhani wakuu wa mikoa na wilaya wana kazi muhimu zaidi ya kuhakikisha kuwa hilo halitokei kirahisi. Hivyo, ni bora pia uainishe ni jinsi gani chama kama CDM kitajenga chama from bottom up zaidi ya kinavyofanya hivi sasa kwa opereshini zake kama sangara na M4C zikihusisha pia mikutano ya ndani.

Kuhusu mafunzo kwa viongozi hasa wa ngazi za chini hilo ni wazo jema sana; CDM wanahitaji kulizingatia kikamilifu manake si wote wanaoelewa malengo na mikakati ya kiutendaji ya kufikia mageuzi yanayokusudiwa.
 
Kuhusu kujenga chama tokea chini sidhani kama inaweza kutokea bila kubata hamasa toka juu. Inabidi viongozi wa juu wenye mvuto waende chini kuwapiga tafu na kwaandalia mazingira ya utendaji makada wanaochipukia kisha kuwaacha waendelee huku kukiwa na mawasiliano mazuri ya mashauriano. Tatizo linaweza kuwa kama viongozi wa juu wanadhibiti na kuingilia madaraka ya ngazi za chini wakati wote isivyostahili.

Tatizo langu kubwa lipo kwenye monitoring ya chama hasa katika suala la kiutendaji, tukumbuke tunapambana wa wenzetu ambao wako well equiped lakini hili halipaswi kuwa chanzo wa woga na hofu, kinachofanya CDM kushindwa kuibana CCM kikamilifu kisiasa ni kutokana na kutokwepo na base ngazi za chini, mbinu za kuishindani na motivation kwa viongozi.


Hivyo, ni bora pia uainishe ni jinsi gani chama kama CDM kitajenga chama from bottom up zaidi ya kinavyofanya hivi sasa kwa opereshini zake kama sangara na M4C zikihusisha pia mikutano ya ndani

Hili naliandalia mada(uzi) maalum.
 
Back
Top Bottom