Kosa kubwa ambalo chadema inafanya! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kosa kubwa ambalo chadema inafanya!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbelwa Germano, Oct 30, 2012.

 1. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0


  Ni ukweli usiopingika (undeniable truth) kwamba tofauti ya kiuchumi baina ya CCM na CDM inachangia sana CDM kutofanikisha baadhi ya malengo yake kisiasa. Vilevile CCM imejenga coalition na taasisi zote nchini zenye nguvu kiuchumi, kisiasa na kijamii. Kwa mfano, sekta binafsi (wafanyabiashara); majeshi ya ulinzi na usalama; mashirika ya umma n.k.

  Silaha kubwa ya kupambana na CCM ni kwa kutumia akili, maarifa na ubunifu. Ni vizuri kwa CDM kuwa more strategic mfano M4C imeleta hamasa sana kwa kuongeza kiu ya mabadiliko lakini imekuwa wimbo zaidi wa kuitoa CCM madarakani bila kutoa tafakari ya tafsiri pana ya mabadiliko na kukijenga chama kiushindani.

  Kosa kubwa ambalo CDM imekuwa inafanya ni kujenga chama kutoka juu kwenda chini “from the top to the bottom” badala ya kujenga chini kwenda juu “from the bottom to the top”. Kuna kutoaminiana (mistrust) ya viongozi wa juu kwenda chini na jambo hili kusababisha kudhoofika kwa base ya chama. Mfano uchaguzi wa wadiwani umekuwa fruitless in a large extent kwa sababu hakukuwa na mikakati dhabiti kwa viongozi wa chini kwa maana ya kujenga misingi imara ya ushindi kuelekea kuanza kwa kampeni. Imani kubwa iliyojengeka ni kwamba viongozi toka makao makuu ya chama ikiwepo wabunge wangeweza kuifanya kazi hii kwa ufanisi kuliko viongozi wa ngazi za chini. Lakini imani hii ime-prove failure tofauti na matarajio ya wengi.

  Tofauti kubwa kati yetu na CCM inatokana na dhana hii ya kujenga chama juu kwenda chini “from the top to the bottom” na chini kwenda juu “from the bottom to the top”. Tumeamini sana tunaweza kujenga chama kupitia majukwaa ya kisiasa kuliko kujijenga kupitia mikutano ya ndani ya chama kuanzia ngazi za chini kabisa za chama. Vilevile monitoring ya chama hasa katika suala la Leadership Audit bado ni tatizo. Flow of information kati ya wilaya na wilaya, jimbo na jimbo n.k bado ni tatizo kubwa. Ipo changamoto kubwa sana ya uwepo wa viongozi wenye taaluma na ujuzi apart from political figures ambao watafanya kazi ya monitoring and Leadership Audit kuanzia ngazi za chini kabisa za chama kutambua mapungufu ya chama na kuwezesha kupanga mikakati madhubuti ya chama ambayo itakuwa na mafanikio zaidi kulingana na mazingira husika.

  Vilevile, awareness ya viongozi wa wilaya/majimbo katika kutafiti na kudadisi utekelezaji wa majukumu ya serikali katika maeneo husika ni jambo ambalo lazima lizingatiwe. Uzoefu wangu mdogo ndani ya siasa ndani ya CDM unaniaminisha kwamba watu hawana interest sana na mambo ya kitaifa kisiasa kuliko mambo ambayo yanawazunguka katika maeneo yao hasa katika ngazi za vijiji/mitaa,vitongoji, udiwani na ubunge.. Mfano katika kampeni za udiwani viongozi wengi wa CDM wamekuwa wakizungumzia sana tuhuma na matukio ya kitaifa bila kugusia masuala ambayo yanawazunguka mfano udhaifu wa usimamizi wa halmashauri za wilaya/miji ambalo ni tatizo kubwa chini ya utawala wa CCM.

  Mafunzo (training) kwa viongozi wa ngazi za chini lazima liwepe kipaumbele na jambo hili lazima lifanyike in a regular basis kwa dhumuni la kuwajenga viongozi hawa katika mazingira ya kiushindani. Tukifanya hivi tunaweza kuondoa ile dhana ya money is everything na kujenga dhana ya money is nothing without strategies. Lazima viongozi hawa waandaliwe vizuri kukabiliana na changamoto za kiutendaji na kisiasa katika ngazi za chini za chama tofauti na ilivyo sasa.

  Naomba nimalizie maelezo haya machache kwa kusisitiza kuwa, ni ukweli kamili watu wamechoka na CCM lakini hili sio jibu la rahisi kwamba wanahitaji mabadiliko bila kuwa na mipango, ubunifu, mbinu na mikakati thabiti ya kuongoza mabadiliko yenyewe. Na mabadiliko haya hayawezi kuletwa na viongozi wa makao makuu ya chama tu au msomi mmoja mmoja bali mabadiliko haya yanaweza kuletwa kwa ushirikiano na uaminifu kati ya viongozi wa juu wa chama na viongozi wa ngazi za chini wa chama pamoja na makundi mbalimbali katika jamii.

   
 2. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Huo ushauri wako si ungepeleka kwenye chama chenu moja kwa moja.
   
 3. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Lazima nijenge msingi imara wa arguments zangu kwa kushirikisha maoni mbalimbali kutoka kwa watu mbalimbali. Jukumu la kujenga CDM imara si la wanasiasa pekee ni jukumu la wapenda mabadiliko. In such sijaongea siri yoyote ambayo ni muflisi kwa cdm bali ni ukweli kamili ambao lazima ufanyiwe kazi.
   
 4. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Base ya arguments zangu imeanza hapa "Kosa kubwa ambalo CDM imekuwa inafanya ni kujenga chama kutoka juu kwenda chini "from the top to the bottom" badala ya kujenga chini kwenda juu "from the bottom to the top". Tafadhali naomba urudie kusoma na jifunze kujenga hoja.
   
 5. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,563
  Likes Received: 16,531
  Trophy Points: 280
  Nadhani kosa kubwa wanalolifanya CDM ni kutokuwa na Umoja wa Wanawake wenye nguvu kwenye sytem yao.Tumeona umoja wao wa vijana ulivyo na nguvu sasa viongozi wangejenga mhimili imara wa wanawake maana bila ya wanawake bado CHADEMA itakuwa haijafanya kazi.Kwani wanasema Ukimwelimisha Mwananke mmoja umeielimisha jamii.Wakianza na wanawake huko vijijini ni rahisi kupenya.
  Wajaribu waone!
   
 6. C

  Concrete JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Nina uhakika mleta mada haujawahi kushiriki kwenye operation za M4C, Kampeni za chaguzi ndogo, hukusimamia kura na wala hukupiga kura.

  Ni rahisi kusema hayo kwa sababu umekaa kwenye keyboard na kufuatilia mtandaoni tu.

  Karibu ground field nitakuelewa vizuri.
   
 7. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimekuelewa mkuu, umeandika vizuri sana kwamba ipo changamoto kubwa sana kupenyeza vijijini na kazi hii lazima ifanywe kwa ukaribu na viongozi wa chini wa chama. Bila BAWACHA imara chini, hata ikiwepo BAWACHA yenge nguvu juu bado tutaendelea kugalagazwa na CCM, lazima kuwepo na monitoring ya chama kuanzia ngazi za chini kabisa za chama.
   
 8. m

  msolopa ganzi Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 57
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  nakubaliana na mada ya mtoa hoja kwanza tunahitaji kuijenga CHADEMA kuanzia chini kwenda juu kwa huku chini ndipo wanapopatikana wapiga kura wengi so wapiga kura wakiona kiongozi wao wa ngazi ya chini hana ushawishi wowote kisiasa basi wanaona bora waendelee kuichagua CCM,Ni muhimu kwa viongozi wa CHADEMA kuanza kufanyia kazi mapeama mapungufu yaliojionyesha kabda ya uchaguzi mkuu wa 2015.
   
 9. d

  dotto JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Strategy ingine nzuri ni Kuwachoma mikuki tumboni wapinzani wako kama kule Shinyanga. Majambazi wakubwa nyie!!
   
 10. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inshort naijua CDM In n Out na nimeshiriki kwenye shughuli za chama kwa zaidi ya miaka mitatu sasa, lazima tukubailiane na jambo moja; bado chama chetu hakijawa competitive kwa ngazi za chini za CDM dhidi ya CCM, CCM bana base imara sana kisiasa kwa ngazi za chini za chama.
   
 11. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  mkuu ukiwa unaoga unaanzia wapi?? Taasisi nyingi zikiwemo vyama vya siasa vinatumia top to bottom! ndio maana post za awali ni Board members,MD,senior managers,junior managers,staff......huu ni mfano wa mashirika na taasisi mbalimbali.
   
 12. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Nakushauri huu ushauri wako ungeupeleka moja kwa moja Makao Makuu ya Chadema pale Kinondoni Mtaa wa Ufipa. Humu kuna Chadema JF hawa huwezi kuwapa ushauri waulize Mkandara, Pasco, Mzee Mwanakijiji,
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. C

  Concrete JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Yapo mapungufu ya msingi katika CHADEMA lakini haya mnayozungumzia humu sio kabisa.

  Ukweli ni kwamba huko ''kushindwa'' kwa chadema mnakozungumzia kimsingi hakutokani na hayo mapungufu bali VITU VINGINE KABISA.

  Karibu Ground field uone hali
  halisi kwanza.
   
 14. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Haisaidii mtu yoyote kudai ukweli ulivyo sivyo...mfano wako ni maneno rahisi nje ya misingi imara ya kujenga chama kama taasisi ya kiushindani anyway kwanini ni rahisi kwa mwanaume kukaa kifua wazi kuliko kukaa bila suruali, au suruali nayo inavaliwa kutoka juu.
   
 15. W

  Wizzard Wweed Senior Member

  #15
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UMENENA vema,vizurilikifanyiwa kazi.
   
 16. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  wana CDM tujipange! tusitafute mchawi! wengi tulitalajia CDM kushinda kata nyingi zaidi ya CCM.
  Tukae chini tufanye tathmini ya kina!
  ila ukweli CCM na rushwa ni pete na kidole kama wenyewe kwa wenyewe wanachezeana faulo! unategemea nini wakiwa against CDM!
  CDM waangalie upande wa mawakala wake....uchawi wa mzungu ni pesa.

  BAWACHA nayo iangaliwe kwa jicho pana zaidi.....wapiga kura wengi wa CCM ni wanawake.
   
 17. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hao uliowataja hapo tatizo lao wanafuata upepo sana, utadhani boya la kuongozea ndege. Cdm wapo wengi humu na ushauri watauchukua kama wakiona unafaa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. C

  Concrete JF-Expert Member

  #18
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mkuu soma vizuri post yangu ndio utanielewa.

  Kwa mambo uliyosema humo siamini kama umeshiriki operation za M4C, au kama umeshiriki uchaguzi huu mdogo kwa karibu kwa namna yoyote ile.

  Ninauhakika kama ungeshiriki kuna mambo usingeyaandika ama ungeyaandika kabla ya uchaguzi na sio baada ya matokeo.

  In short you wrote goodly but you mixed pure and impurities!!!

  Nilikuwa Ground Field nina uhakika na nilicho kitafiti.
   
 19. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hakuna jibu moja linalotumika kwa mambo yote, nakubalina na ww kabisa yapo mambo mengine zaidi ya haya lakini hatupaswi kutupa lawama hizi kwa wapinzani wetu kisiasa bila kutazama matatizo ya ndani ya chama. Ni vyema ungechangia ambacho na ww umekitafiti kuliko kukivumbika.

  Binafsi nimeshiriki kwenye kampeni za juzi za udiwani na nimeshiriki kabla ya hapo kwenye kampeni na mikutano mablimbali ya chama na sio mara yangu ya kwanza kuzungumza haya.
   
 20. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #20
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mbelwa Germano achana na wasoma maandishi wasiojali kupata mantiki wala maudhui ya maandishi yenyewe. Katika vitu ambavo vinaigharimu CHADEMA kikubwa kabisa ni mfumo wake uliowekwa na Katiba pamoja na utendaji wa watu wa Makao Makuu dhidi ya viongozi wa ngazi za chini kabisa kwenye chama!

  Hebu fikiria Mwenyekiti au Katibu wa CHADEMA taifa anafika wilayani au Mkoani haonani wala haonyeshi kama ana haja ya kufahamiana na viongozi waliopo kwenye eneo husika. Kiongozi huyo akimaliza mkutano wake anaingia kwenye gari na kutokomea kwenye wilaya au mkoa mwingine bila wakati mwingine ya kuagana na viongozi wa wilaya au mkoa aliokuwa anafanya kazi za uhamasishaji chama. Waulize viongozi wa Mkoa wa Morogoro kama tangu iondoke M4C Mkoani kwao mawasiliano na mahusiano yao na Makao Makuu yakoje!?

  Uhusiano kati ya Makao Makuu na Mikoa ni kama haupo na uuwezi amini lakini ndiyo ukweli wenyewe mpaka leo ukiwauliza watu wa CHADEMA Makao Makuu wana Viongozi wangapi wa ngazi ya Mkoa kwa upande wa BAVICHA,BAWACHA na chama chenyewe utaishia kushangaa. Huko kwenye wilaya na Majimbo hali ndiyo iko shaghalabagala kabisa!!
   
Loading...