Kosa kubwa alilofanya IGP Sirro katika tuhuma za ugaidi dhidi ya Mbowe, ambalo linaweza kuleta fedheha mbaya kwake binafsi, kwa Polisi na Tanzania

Ila hii timu..
20210917_182429.jpg
Screenshot_20210917-154032~3.jpg
 
nashauli tusiwe wepesi kutoa hukumu na kuanza kubagaza watu kabla kesi haijafika popote,

wapo mashahidi wa kutosha

tusubiri watoe ushahidi wao then tuupime.
Hamna kes hata wakihukumu ukweli ni kwamba kes imebubwa na niselikar imeaa mua kwa manufaa ya wachache.
 
kesi ya mbowe imetupa picha kuwa CPP VYUO VYA POLISI vinahitaji reformations sana!!yaani polisi hawana mafunzo ya uweledi zaidi ya kupiga watu tu!!
Naamini kule cpp from day one, nikufundisha kupiga tuu virunguu hadi wana maliza mafunzo
 
Naona hujui kwamba shahidi wa kwanza ndio anapangwa ambaye atatoa the highest impact (damage) kwenye kesi. Sasa kama the highest impact ya IGP Sirro ni ushahidi wa Ramadhani Kingai, basi IGP na jeshi lake wote ni watu wa kuhurumiwa sana - ndio hao wanafukuza bodaboda hadi Malawi!
Uongozi wa polisi na polisi wao wanafanana. Wanafukuza boda boda kuvuka mpaka, uongozi unawafukuzwa wote. Wamesahau jeshini mambo yanakwenda kwa amri. Hakuna waliotoa amri? Gari ipo kwenye mwendo, ulitegemea wakaidi wa amri waruke?
 
Uongozi wa polisi na polisi wao wanafanana. Wanafukuza boda boda kuvuka mpaka, uongozi unawafukuzwa wote. Wamesahau jeshini mambo yanakwenda kwa amri. Hakuna waliotoa amri? Gari ipo kwenye mwendo, ulitegemea wakaidi wa amri waruke?
Una point nzuri Mkuu. Labda walikubaliana wote. Lakini kihalisi Mkuu wa huu msafara (detail) ndio alipaswa kuwajibishwa. Point nzuri umetoa
 
Tatizo Chadema kila mtu ni mwanasheria.kila mtu ni Jaji na kila mtu ni mtetezi wa Mbowe!

Acheni kesi ifike mwisho basi.Sio
Nyinyi kila siku mnajadili.....

Lakini hamjiulizi mbona hamjabadilisha chochote kwenye mwenendo wa kesi hii?

Mna hofu ya nini?
Wakati kuvurunda kwa mashahidi wa serikali,ndio unafuu kwa Mbowe?

Ila mimi nauliza swali moja tu la kijinga.

Nalo ni kuhusu bastola waliyokutwa nayo kina Adamoo.

Je umiliki wake ulikuwa ni halali kisheria?

Na kama ni halali!

Je aliyekutwa nayo ndie mmiliki halali anaepaswa kuwa nayo kwa matumizi binafsi.
Kulingana na sheria za umiliki wa silaha binafsi za moto nchini?

Je kama sio halali,nini ndio hukumu ya mtu au kundi la watu wanaokutwa na silaha ya moto kinyume na sheria?

Tuanzie hapo.....haya mengine ni porojo za mawakili tu.

Ushahidi unaochukuliwa na mahakama,hautokani na mbwembwe za mawakili bali yale ya point muhimu.

Kutoka kwa shahidi alivyotoa maelezo ya awali kwenye maandishi.

Uamuzi hautokani na maoni kutoka Maria Space au Jamiiforums.
 
Back
Top Bottom