Jindal Singh
JF-Expert Member
- Sep 9, 2015
- 1,857
- 1,538
Hiki ndicho kilichonifanya nianze uzi bila salaam kutokana na vitendo visivyo vya kizalendo vya askari polisi kupiga na kuumiza raia ambao sisi tunasema kuwa hawana hatia.
Baada ya kutokea shambulizi la kijambazi lililoua askari kadha mkoani pwani sasa imekuwa ni chuki na kulipiza kisasi kwa jeshi la polisi dhidi ya raia yeyote yule atakaeonekana anakatiza katiza barabarani kwa hari yeyote ile, ikiwemo kupigwa virungu na mashuti na ngumi mfano wa mtu anayecheza boxer, hawaishii hapo tu! bali hadi kupora mali za watu katika vioksi.
Kibaya zaidi ni pale mtaji uliozuka kwa wana usalama barabarani kuzidisha kasi ya kukamata magari na kupora pikipiki za watu na kuzifungia.
Sasa hii si njia nzuri ya kuzuia matukio kama haya kuendelea sababu yanaongeza chuki baina ya serikali na raia kwa kupitia polisi.
Angalizo
Njia ya pwani kwa sasa si salama tena kuanzia Mkuranga hadi kibiti hivyo mnaetembea ambao ni wafanyakazi wa ummah basi mnatakiwa muwe na set of ID.