Kortini kwa madai ya kuiba Biblia za Kanisa la Malanasa

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
Kortini kwa madai ya kuiba Biblia za Kanisa la MalanasaNa Colletha Mwangamila

MKAZI wa Buguruni mwenye asili ya kiasia Hanif Fazal (40), jana alifikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Buguruni kwa tuhuma za kujifanya mlokole na kuiba Biblia 11 zenye thamani ya Sh 850,000 pamoja na kipaza sauti mali ya kanisa la Malanasa (Assembles of God).

Ilidaiwa na mwendesha mashtaka wa polisi ,Pc Mtesigwa, mbele ya Hakimu Emanuel Mbonamasabo kuwa, mtuhumiwa alifanya kitendo hicho Mei 24 mwaka huu, huko maeneo ya Buguruni ambako Fazal aliiba Biblia kumi na moja na kipaza sauti.

Hata hivyo mtuhumiwa alipoulizwa kuhusika na tuhuma hizo alikana shtaka na kesi iliahirishwa hadi Juni mosi, mwaka huu.

Katika tukio lingine Ayubu Said (19), mkazi wa Vingunguti Mtambani alifikishwa mahakamani hapo kwa tuhuma za kumtaja Zainabu Diwani kuwa ni mchawi.

Ilidaiwa mahakamani hapo kwamba Mei mosi, mwaka huu, huko Vingunguti Mtambani, Ayubu alimtuhumu mlalamikaji kuwa ni mchawi. Hata hivyo mtuhumiwa alipoulizwa kuhusika na tuhuma hizo alikana kuhusika na kesi iliahirishwa hadi Juni mosi mwaka huu itakaposikilizwa tena
 
Back
Top Bottom