Kortini kwa kuuza mikanda ya ngono | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kortini kwa kuuza mikanda ya ngono

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, May 28, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,127
  Likes Received: 5,567
  Trophy Points: 280
  Kortini kwa kuuza mikanda ya ngono
  [​IMG]
  Wednesday, May 27, 2009 11:39 AM
  MFANYABIASHARA Hamisi Hemed [40] mkazi wa Mbagala amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa kosa la kuuza mikanda ya video ya picha za ngono.Mtuhumiwa huyo alifikishwa Mahakamani hapo na kusomewa shtaka lake hilo na Wakili wa Serikali, Credo Lugaju mbele ya Hakimu Pamela Kalala wa Mahakama hiyo.

  Lugaju alidai kuwa, mtuhumiwa alikamatwa Mei 15, mwaka huu, huko katika maeneo ya Kariakoo akiwa anauza mikanda hiyo bila wasiwasi na bila kutambua ni uvunjaji wa sheria za nchi kwa mujibu wa katiba.

  Mshitakiwa alikana shtaka hilo na kudai hakuhusika na uuzaji wa mikanda hiyo na kupewa dhamana.

  Hata hivyo kesi hiyo iliahirishwa kwa kuwa lugalu alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado halijakamilika na kesi itarudi tena Juni 10, mwaka huu.

  Wakati huohuo Farida Hamisi [29] mkazi wa Buguruni amefikishwa Mahakamani hapo kwa tuhuma za kumshambulia kwa matusi ya nguoni mpangaji wake na kummwagia maji ya moto na kumsababishia maumivu makali hadi kupelekea kulazwa hospitalini.

  Ilidaiwa kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Mei 20, mwaka huu, majira ya jioni, alimmwagia Halima Saidi [25] maji ya moto kitendo ambacho ni kinyume na sheria.

  Hivyo kutokana na hali ya mlalamikaji wa kesi hiyo kuwa bado hairidhishi hakimu aliamuru kumnyima dhamana mshitakiwa huyo hadi hapo hali ya mlalamikaji itakaporidhisha.

  Mshitakiwa alikana shtaka na alikwenda
   
Loading...