korti yawaachia huru mwakalebela,mkewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

korti yawaachia huru mwakalebela,mkewe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mujumba, Mar 12, 2011.

 1. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Korti yawaachia huru Mwakalebela, mkewe

  Mahakama ya Mkoa wa Iringa imemwachia huru aliyekuwa mshindi wa kwanza katika kura za maoni nafasi ya ubunge wa Iringa Mjini (CCM),Frederick Mwakalebela (41), na mkewe Selina katika kesi namba nane ya kutoa hongo kwenye mchakato wa kura za maoni iliyokuwa inawakabili.
  Mwakalebela pia, aliachiwa huru Februari 25, 2011 na Hakimu Festo Lwila wa mahakama ya wilaya ya Iringa kwenye kesi namba 4 iliyokuwa inamkabili peke yake baada ya hakimu kujiridhisha kuwa upande wa mashtaka ulikuwa haujatenda haki kuchanganya makosa mawili kwenye shtaka moja na kusema kuwa upande wa mashtaka ulikuwa na hiari ya kumshtaki tena mahakamani kama wanaona inafaa kufanya hivyo, lakini kwa kutumia kosa moja na sheria moja kati ya mbili walizokuwa wametumia.
  Tofauti na kesi namba nne, Mahakama ya Mkoa wa Iringa chini ya Hakimu wa mahakama hiyo, Mary Senapee, amewaachia huru Mwakalebela na Selina baada ya kuridhika na hoja kuu mbili za utetezi uliokuwa unaongozwa na Basil Mkwatta wa Mkwatta Law Chambers.
  Hoja hizo ni kwamba upande wa mashtaka wakati wanapeleka hati ya mashtaka mahakamani ilipindi waonyeshe wazi kwamba Mwakalebela na mkewe walitoa hongo kwa ajili ya kutaka upendeleo au kupindisha utaratibu wa kawaida kwa niaba ya ofisi yao au mkubwa wao na kwamba waliopokea pia walifanya hivyo kwa niaba ya ofisi zao, biashara zao au mkubwa wao.
  Kwamba kifungu namba 15 (1) (b) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007 kinawahusu watumishi wa serikali au wanaoshikilia ofisi za umma hivyo ni lazima hati ya mashitaka ionyeshe waziwazi maneno hayo.
  Hoja ya pili ni upande wa mashtaka kutotenda haki kwa kuchanganya makosa mawili kwenye shtaka moja kwa kutumia Sheria mbili tofauti ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007 na Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010.
  Katika hoja ya kwanza, Mwendesha mashtaka wa Takukuru Mkoa wa Iringa, Imani Nitume, alisema maneno hayo siyo lazima yaonyeshwe kwenye hati ya mashtaka kwani yanaweza kusubiri wakati wa ushahidi.
  Hakimu Senapee alijiridhisha kuwa hoja hizo zina nguvu kisheria na kwamba kuchanganya makosa mawili kwenye shtaka moja si haki hivyo akawaachia huru watuhumiwa na kueleza kuwa upande wa mashtaka wanayo haki ya kukata rufaa kama hawajaridhika na hukumu hiyo.
  Mwakalebela na Selina wanadaiwa kuwa Juni mwaka jana, katika kijiji cha Mkoga Manispaa ya Iringa, walitoa hongo ya Sh.100,000 kwa Mwenyekiti wa kijiji hicho, Hamisi Luhanga, ili azigawe kwa wapiga kura 30 wa CCM ili wampigie kura za maoni zilizofanyika Agosti mosi, 2010.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Moja ya majivuno ya PCCB ni kukamata wala rushwa wakati wa uchaguzi...au ilikuwa ni kuwapunguza kasi waliowatishia wale waliowataka nini???
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Teh teh. Good. Na baada ya hapa waje mbele ya press waeleze jinsi walivyoshindwa si kujitangaza tu wanavyokamata kwa upendeleo!
   
Loading...