Korti yaamuru Nabii Mwingira akamatwe

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
863
na Irene Mark

MAHAKAMA Kuu kitengo cha Ardhi, Dar es Salaam, imetoa amri ya kukamatwa kwa Mtume na Nabii, Josephat Mwingira, ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Watumishi wa Ephata, kwa madai ya kupuuza amri ya mahakama.

Amri ya kukamatwa nabii huyo ilitolewa juzi mahakamani hapo na Jaji Alise Chingwile, baada ya upande wa mlalamikaji kudai kuvunjwa kwa amri ya mahakama iliyozuia kubomolewa kwa ukuta wa eneo linalogombaniwa kati ya Mwingira na Kiwanda cha Plastiki cha Soza.

Eneo linalogombaniwa lipo Mwenge sehemu lilipo Kanisa la Ephata, ambapo licha ya kuwepo kwa kiwanda hicho, awali palikuwa na wafanyabiashara wa vibanda na gereji.

Katika shauri hilo ambalo ni pingamizi namba 24/2006; lililofunguliwa na wamiliki wa kiwanda, mahakama ilitoa amri ya eneo hilo kutobomolewa na kuruhusu wenye Kiwanda cha Soza kuendelea na shughuli zao wakisubiri kukamilika kwa kesi ya msingi.

Licha ya kutolewa kwa amri hiyo, Nabii Mwingira alikaidi na kuwaondoa kwa nguvu baadhi ya wafanyabiashara waliozunguka eneo hilo na wahusika wa kiwanda hicho cha plastiki, Mei 26, mwaka 2007 alipobomoa.

Aidha, Nabii Mwingira alihamia katika kiwanja hicho cha Mwenge kitalu namba 90, na kudai kuwa amenunua kihalali eneo hilo kutoka kwa Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC) mwaka 2001.

Huyu ni kiongozi wa dini amepuuza amri ya mahamakama.Wengine wasio viongozi wa dini watafanyaje?
h.sep3.gif
 
Huyu ni kiongozi wa dini amepuuza amri ya mahamakama.Wengine wasio viongozi wa dini watafanyaje?
h.sep3.gif
amepuuza mahakama wala hajampuuza Mungu wake, acha unafiki, cha msingi tuangalie sababu zilizomfanya aipuuze mahakama, pengine alikuwa na ratiba ya maombi
 
amepuuza mahakama wala hajampuuza Mungu wake, acha unafiki, cha msingi tuangalie sababu zilizomfanya aipuuze mahakama, pengine alikuwa na ratiba ya maombi

Hey,ndugu yangu mbona unanitusi bure?unajua maana ya unafiki?mimi nilichosema ni kwamba kama kiongozi wa dini anatakiwa kuwa mfano..Kuupuza mahakama sio mafano mzuri hata kama angekuwa na sababu za muhimu.Biblia iansema tuheshimu mamlaka zilizowekwa....acha hasira ndugu yangu,jenga hoja.Pole kama nimekuudhi sio lemgo langu..
 
Huyu ni kiongozi wa dini amepuuza amri ya mahamakama.Wengine wasio viongozi wa dini watafanyaje?

mahakama inajishushia hadhi yenyewe, ikipuuzwa na serikali inilmaba miguu, watu binafsi ndio nasikia amri ya kukamatwa inatolewa. kama inataka kuheshimiwa ithibitishe kwanza kwa matendo yake, itoe haki kwa watu masikini, sio ikubali kutumiwa kuwatupa magerezani............
 
Ni kweli kabisa lakini sio hoja hapa.hapa hoja ni kiongozi wa dini kukuoa utii.Biblia inasema Utii ni Bora kuliko dhabihu(Sadaka)
 
Hey,ndugu yangu mbona unanitusi bure?unajua maana ya unafiki?mimi nilichosema ni kwamba kama kiongozi wa dini anatakiwa kuwa mfano..Kuupuza mahakama sio mafano mzuri hata kama angekuwa na sababu za muhimu.Biblia iansema tuheshimu mamlaka zilizowekwa....acha hasira ndugu yangu,jenga hoja.Pole kama nimekuudhi sio lemgo langu..
no usijari sina nia mbaya sorry kama nimekukwaza hiyo ni kwa ya huyo mwana habari isipokuwa imepitia kwako kwa vile wewe ndo umeleta hii habari
 
Ni kweli kabisa lakini sio hoja hapa.hapa hoja ni kiongozi wa dini kukuoa utii.Biblia inasema Utii ni Bora kuliko dhabihu(Sadaka)
ni kweli kabisa lakini si kwa mahakama za kinafiki, utii kwa Mungu ni bora kuliko dhabihu, unataka hata kumtii mganga wa kienyeji ni bora kuliko dhabihu? ndugu usiinukuu Biblia kwa kuisaidia uelekeo
 
Ngoja tusubiri tuone nini kinatokea na nani kakosea kati ya mahakama na mtumishi huyo wa Mungu.
 
amepuuza mahakama wala hajampuuza Mungu wake, acha unafiki, cha msingi tuangalie sababu zilizomfanya aipuuze mahakama, pengine alikuwa na ratiba ya maombi
kuvunja miundombinu ya watu ni ratiba ya maombi?
Bible inaamrisha kuitiii mamlaka na serikali kwa kuwa huwezi kumtii Mungu usiyemwona ilhali watu wanaoonekana hauwatii
 
Huyu ni kiongozi wa dini amepuuza amri ya mahamakama.Wengine wasio viongozi wa dini watafanyaje?

kwa wanaoijua mwenge na kujua fitna ya ardhi mwenge lazma watakubaliana na mimi kwamba the only way mwenge itaendelea ni kwa kutumia nguvu tu!!! hayo ya mahakama ni kitu kingine ila nina wasiwasi sana na sheria zetu siku hizi hasa kutokana na baadhi ya maamuzi

labda niulize swali, inakuaje mtu aliye kwenye open space kama gereji bubu awe na haki mbele ya sheria? nauliza ili nijue na si kwamba napinga mahakama
 
The Disciples of today who owns Bank, why dont he ask the short man Lazarus "the tax collector" OH GOD open their eyes!
 
Knisa kwenye godauni!
Kwanza:
Kanisa linatakiwa kuwa na mipango ya maendeleo kutokana na hali halisi ya nchi,
Kama wananchi hawana basic social services, kama zahanati au maji,
Linatakiwa kufocus huko kwanza. Sasa huyu mwingira guy anaanzisha business oriented miradi itawasaidiaje waumini masikini hawa?
Benki!? Mashamba huko sumbawanga?!

This is shait men. For real. I dare to sa that right here and now.
 
Mie hawa watu wananiacha hoi,but kuna kipegele fulani ndani ya biblia kinasisitiza MUUMINI kutii mamlaka zilizo juu yake,sasa huyu sijui kafanyaje!!

Na ndio hoja yangu kuu.Yeye kama kiongozi wa dini anapaswa kutii and then mengine yatafuata baadaye.Huu ni utii gani wa kuchagua wa kumtii?
 
Ni kweli kabisa lakini sio hoja hapa.hapa hoja ni kiongozi wa dini kukuoa utii.Biblia inasema Utii ni Bora kuliko dhabihu(Sadaka)
tatizo lako unakariri kifungu badala ya kukielewa, utii huo, unajua unahusu nini? maana sadaka twatoa kwa Mungu, hivyo sadaka, kama Mungu humtii sadaka yako ataitaka ya nini, inamaanisha kwa Mungu utii ni bora kuliko dhabihu yaani sadaka, na si pahari pengine panapohusisha akili za mwanadamu
 
Na ndio hoja yangu kuu.Yeye kama kiongozi wa dini anapaswa kutii and then mengine yatafuata baadaye.Huu ni utii gani wa kuchagua wa kumtii?
kuchagua wa kumtii ni jambo la muhimu kwa mtu anayejitambua na kuwa na akili timamu, huwezi ukawa unatii kila kitu, we labda uwe mlevi anayeamua kutukana kila mtu au kusalimia kila mtu, iweje ufundishwe namna ya kuutumia utii? usipochagua pa kupeleka utii wako, utawatii hata wachawi, walawiti, wafiraji, na waongo, harafu unategemea nini ukiwatii watu hao? Mahama za Tanzania nyingi zimekuwa hazitendi haki, kama hazitendi haki maana yake zinaongozwa kishetani, Kwa sababu Mungu ni wa haki hivyo hazikutoka kwake, kwa hiyo kuzipuuza ni kumpuza shetani nba mahakama zake
 
amepuuza mahakama wala hajampuuza Mungu wake, acha unafiki, cha msingi tuangalie sababu zilizomfanya aipuuze mahakama, pengine alikuwa na ratiba ya maombi

Hata biblia inasema "Tiini mamlaka zilizoko ulimwenguni" hapa huyu mfanyabiashara wa neno la Mungu hajatii anayofundisha.

Ni kweli kabisa lakini sio hoja hapa.hapa hoja ni kiongozi wa dini kukuoa utii.Biblia inasema Utii ni Bora kuliko dhabihu(Sadaka)

Fungukeni macho jamani...sio wote wamwitao bwana!bwana wataurithi ufalme wa Mungu.

Ngoja tusubiri tuone nini kinatokea na nani kakosea kati ya mahakama na mtumishi huyo wa Mungu.

Huyu ni tajiri mkubwa anamiliki Bank na Mashamba ya mifugo huko mikoani aliyonunua kwa bilion plus na ni mfadhili wa serikali maya uchaguzi je unafikiri nani atashinda?
 
amepuuza mahakama wala hajampuuza Mungu wake, acha unafiki, cha msingi tuangalie sababu zilizomfanya aipuuze mahakama, pengine alikuwa na ratiba ya maombi

Mungu naye anataka tutii mamlaka halali za hapa duniani..... Mahakama ya Tanzania ni mamlaka halali na ilitoa amri halali kabisa.
 
Mie hawa watu wananiacha hoi,but kuna kipegele fulani ndani ya biblia kinasisitiza MUUMINI kutii mamlaka zilizo juu yake,sasa huyu sijui kafanyaje!!
unapokisoma iulkize Biblie ni mamlaka gani zilizo juu? siyo unasoma then imetosha utapotea, kuidadisi Biblie ni kumdadisi Mungu, na ye kasema Mwanadamu hata eseme uongo....endelea utapata maarifa zaidi
 
Back
Top Bottom