Regia Mtema
R I P
- Nov 21, 2009
- 2,970
- 863
na Irene Mark
MAHAKAMA Kuu kitengo cha Ardhi, Dar es Salaam, imetoa amri ya kukamatwa kwa Mtume na Nabii, Josephat Mwingira, ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Watumishi wa Ephata, kwa madai ya kupuuza amri ya mahakama.
Amri ya kukamatwa nabii huyo ilitolewa juzi mahakamani hapo na Jaji Alise Chingwile, baada ya upande wa mlalamikaji kudai kuvunjwa kwa amri ya mahakama iliyozuia kubomolewa kwa ukuta wa eneo linalogombaniwa kati ya Mwingira na Kiwanda cha Plastiki cha Soza.
Eneo linalogombaniwa lipo Mwenge sehemu lilipo Kanisa la Ephata, ambapo licha ya kuwepo kwa kiwanda hicho, awali palikuwa na wafanyabiashara wa vibanda na gereji.
Katika shauri hilo ambalo ni pingamizi namba 24/2006; lililofunguliwa na wamiliki wa kiwanda, mahakama ilitoa amri ya eneo hilo kutobomolewa na kuruhusu wenye Kiwanda cha Soza kuendelea na shughuli zao wakisubiri kukamilika kwa kesi ya msingi.
Licha ya kutolewa kwa amri hiyo, Nabii Mwingira alikaidi na kuwaondoa kwa nguvu baadhi ya wafanyabiashara waliozunguka eneo hilo na wahusika wa kiwanda hicho cha plastiki, Mei 26, mwaka 2007 alipobomoa.
Aidha, Nabii Mwingira alihamia katika kiwanja hicho cha Mwenge kitalu namba 90, na kudai kuwa amenunua kihalali eneo hilo kutoka kwa Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC) mwaka 2001.
Huyu ni kiongozi wa dini amepuuza amri ya mahamakama.Wengine wasio viongozi wa dini watafanyaje?