Korti yaamuru Mzungu kucharazwa viboko kumi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Korti yaamuru Mzungu kucharazwa viboko kumi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 20, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MAHAKAMA ya Wilaya ya Bukoba, imemhukumu Robert Maintland (42), raia wa Ugiriki kutumikia kifungo cha miaka miwili jela na kucharazwa viboko kumi, baada ya kupatikana na hatia ya kuingia nchini kinyume cha sheria.
  Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Peter Matete.

  Hukumu hiyo inaweza kuwa faraja kwa wananchi wapatao 100 wa kitongoji cha Bujenjeke, Kijiji cha Ruhija, Kata ya Ijumbi mkoani Kagera ambao walikuwa wakivutana na Mgiriki huyo ambaye alikuwa akituhumiwa kuwanyanyasa akishirikiana na polisi.

  Polisi mkoani Kagera walikuwa wakilalamikiwa kwamba wanamkingia kifua raia huyo wa kigeni ambaye manyanyaso yake dhidi ya raia yaliwafanya baadhi yao kukimbia nyumba zao na kulala vichakani.

  Wakazi wa Bujenjeke waliwahi kuwaambia waandishi wa habari kuwa walikuwa wakilala na kushinda porini, kukwepa kupigwa na askari polisi na mgambo ambao walikuwa wakivaa mavazi ya kufunika nyuso zao maarufu kama mavazi ya kininja.

  Lakini juzi, Mahakama ya Bukoba iliridhika na ushahidi uliotolewa dhidi ya mtuhumiwa, hivyo hakimu Matete alimtia hatiani kwa kosa la kuwepo nchini bila kibali na kumhukumu kwenda jela miaka miwili na viboko kumi au kulipa faini ya Sh80,000.

  Hata hivyo, Maintland alilipa faini ambayo haikumuondolea adhabu ya kuchapwa viboko ambayo ilikuwa itekelezwe jana.
  Mapema hati ya mashtaka iliyowasilishwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka wa Idara ya Uhamiaji, Gerald Mardai ilidai kuwa, raia huyo alikamatwa Februari 23, mwaka jana, akiwa Kituo cha Polisi Bukoba bila kibali halali cha kuingia nchini.

  Pia ilidaiwa kuwa, Maintland alikuwa na hati tatu za kusafiria zikiwa na majina tofauti, ambazo alizitumia kuingia nchini isivyo halali.

  Katika ushahidi uliowasilishwa mahakamani, hati za Uingereza na Afrika Kusini zilikuwa na jina la Robert John Rubeinstein, huku vielelezo vingine vya Ugiriki vikionyesha kwamba alikuwa akitumia majina ya John Robert Penesis na Robert John Maintland.

  Maintland amekuwa na mgogoro wa muda mrefu na wanakijiji wa Ruhija wilayani Muleba, mwaka jana aliripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwachapa viboko wananchi waliodaiwa kuingia katika ardhi yake.

  Baadhi ya familia kijijini hapo na Bujenjeke waliondolewa kwa kuvunjiwa nyumba zao kwa madai ya kuvamia eneo la “Buguma Estate” ambalo mzungu huyo alidaiwa kumiliki kihalali kwa shughuli za uwekezaji.

  Miongoni mwa wakazi wa Kijiji cha Bujenjeke waliomlalamikia mzungu huyo, ni Leonida Pancras (54), aliyemtuhumu kufukua kaburi la marehemu mume wake na kubomoa nyumba akimshinikiza kuhama eneo hilo.

  Pia, miongoni mwa waliomtuhumu mzungu huyo kwa kuwacharaza viboko ni Geniva Romward (30), aliyedai Novemba 2, 2008 alichapwa kwa ushirikiano wa mgambo na polisi wa Muleba.

  Mmoja wa walinzi wa mzungu huyo, Joas Kyatuka, anadaiwa kushiriki matukio ya kubomoa nyumba na kufukuza wananchi waliojenga karibu na eneo hilo, Romward ni miongoni mwa wananchi wengi waliofunguliwa mashtaka ya kuvamia eneo la mwekezaji huyo.

  Akizungumza mwaka jana kujibu malalamiko ya wananchi hao, Maintland alisisitiza kuwa eneo hilo analimiliki kisheria na kudai kuwa, mgogoro huo ulikuwa unakuzwa na wanasiasa wilayani Muleba.

  Kwa mujibu wa wananchi hao, Maintland alifika kijijini hapo mwaka 2003 na kuanza kuweka uzio katika eneo mojawapo la kijiji hicho bila kuishirikisha jamii husika, lakini baadaye aliondoka kurudi kwao.

  Mwaka 2008 Maintland alirejea tena nchini na hapo ndipo mgogoro ulipoanza kwani aliwaamuru wananchi hao kuondoka katika eneo hilo, huku akijigamba kwamba alikuwa tayari kuwalipa fidia kati ya Sh100,000 na Sh350,000, malipo ambayo hata hivyo wananchi hao waliyakataa.
   
 2. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Dawa ya moto ni moto
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hv sheria zao huko kwao hawa wagiriki huwa wanachapwa viboko?na anaechapa huwa ni hakim au polisi?
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Habari njema hii, Amen to that.
   
 5. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mmmmh,yawezekana tunaishi na magaidi hapa au wezi walioshindikana!!!majina yote hayo yanini interchangeably???
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Uekezaji uekezaji, my a$$ ..
   
 7. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  wapo ila lawama kwa wananchi na serikali mtu ataingiaje bila kibali na mnamuona tu mpaka anawanyanyasa mnamwangalia tu walitakiwa kuandamana mpaka kunakohusika
   
 8. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Je adhabu hii ni halali kweli, Immigration Act kifungu 31(2) kinasema ni faini isiyozidi laki moja au kifungo ksichozidi miaka mitatu.

  Sijaona adhabu ya viboko, wandugu au hakimu alikuwa overzelous?
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kama hukumu ya Chenge
  Ameshindwa kulipa faini hiyo ya sh. 80,000/=?
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kaka adhabu ya viboko ndio inanifanya niapate butterflies tumboni. hihihihi

  Kama ameipata hiyo itakuwa pouwa sana...lazima akasimulie kwa mkewe.
   
 11. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  inadepend anachapwa na nani maana kuna watu wanachapa lakini haziingii mwilini
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  I hope Mnali (yule DC aliyewachapa walimu katerero) atakua na kazi sana tukianza kucharaza wageni

  hahahaaaaaaaa
   
 13. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Adhabu ya viboko labda kwa kuwa na yeye alifanyia ukatili kwa kuchapa viboko jirani zake au? Manake kuingia nchini bila vibali kweli wastahili viboko?
   
 14. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  mnali hakuhapa bali alimtuma polisi mie nadhani mahakama ziajili wachapaji ili kupunguza pengo la vijana wanaokosa ajira
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Jan 20, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  sijakuelewa hapa mkuu
   
 16. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kaka adhabu za polisi ni standard. Unapewa kipimo sahihi.
   
 17. K

  Kenge (Eng) JF-Expert Member

  #17
  Jan 20, 2011
  Joined: Dec 7, 2006
  Messages: 502
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Huyu hakimu ni mlevi sana
   
 18. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #18
  Jan 20, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  sorry acid keybord ina kigugumizi mnali hakuchapa bali alimtuma polisi
   
 19. D

  DOCTORMO Member

  #19
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hivi kweli kunauhuwiano gani kati ya kufungwa miaka miwili na kulipa 80,000? hivi sheria zetu ziko weak au? nisawa umemwambia mumfunge au awanunulie soda, kiukweli atachagua kuwapa hela ya soda. Kweli inabidi tufanye mabadiliko makubwa sana ili kujiondoa kwenye manyanyaso haya.
   
 20. N

  Ndevu mbili JF-Expert Member

  #20
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 382
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kivipi?
  Yaani mtu ananyanyasa raia,hadi rai wanahama makazi yao....
  Eti anakutwa na kosa la kuingia nchini bila kibali?
  Tena anadaiwa faini elf80/- wanasheria mtusaidie!!!.
   
Loading...