Korti ya Uingereza yakataa ombi la Marekani la kumuhamisha Assange

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Mahakama ya Uingereza imekataa ombi la Marekani la kumkabidhi kwake mwanzilishi wa mtandao wa WikiLeaks Julian Assange ili akabiliwe na mashtaka ya ujasusi. Mahakama imeamua kuwa hatua ya kumhamisha Assange, ni "ukandamizaji" kutokana na afya yake ya kiakili. Jaji Vanessa Baraitser amesema Assange huenda akajiua iwapo atahamishwa hadi Marekani.

Hata hivyo, serikali ya Marekani imesema itakata rufaa juu ya uamuzi huo.Waendesha mashtaka wa Marekani wanamshtumu Assange kwa makosa 17 ya ujasusi na utumizi mabaya wa Kompyuta kwa kuchapisha mtandaoni nyaraka za siri juu ya oparesheni za jeshi la Marekani nchini Iraq na Afghanistan muongo uliopita. Iwapo atapatikana na hatia, Assange huenda akapewa kifungo cha miaka 175 jela.
 
Huyo Assange kama angekuwa ktk nchi zetu hizi ,nina uhakika US angempa hifadhi na angetupiga mkwara tunabana uhuru wakujieleza.

Hapo ndipo uone US ni mnafiki na Ndumilakuwili.
Mi sidhani kama kuna nchi duniani inayoruhusu SIRI zake za jeshi kuchapishwa hovyo hovyo; tusichanganye madesa wakuu. Hata enzi hizo bongo ikiwa inao uhuru mkubwa wa habari but hakuna mwandishi wa habari aliyewahi kuandika SIRI za jeshi au za kijeshi za Tanzania.

Idadi ya silaha, idadi ya wanajeshi hilo laweza kua sio siri but sio zile SIRI za ki operations za jeshi; hilo hapana.
 
Back
Top Bottom