Kort yataka upelelezi kesi ya Mdee na wenzake

Shindu Namwaka

JF-Expert Member
Sep 22, 2014
4,911
3,082
Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi haraka ili kesi inayowakabili wabunge watatu wanaotokana na Ukawa na madiwani wao ianze kusikilizwa.

Washtakiwa hao ni pamoja na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mwita Waitara (Ukonga) na Saed Kubenea (Ubungo).

Madiwani wanaoshtakiwa katika kesi hiyo ni Ephrein Kinyafu (Kimara), Manase Njema (Kimanga, Tabata) na kada wa chama hicho, Rafii Juma.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alitoa kauli hiyo jana baada ya Wakili wa Serikali, Mbunito Aloyce kudai kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa kwa kuwa upelelezi wake haujakamilika na kuomba ipangiwe tarehe nyingine.

Wakili Peter Kibatala anayewatetea washtakiwa hao, aliuomba upande wa mashtaka kuanza kuisikiliza kesi hiyo kwa sababu washtakiwa walikamatwa haraka haraka na usikilizaji wake uwe vivyo hivyo.

Washtakiwa hao wanaodaiwa kumjeruhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresa Mmbando katika vurugu zilizotokea Februari 27,2016 Ukumbi wa Karimjee kwenye Uchaguzi wa meya na naibu meya wa jiji la Dar es Salaam, wanatetewa na Mawakili Peter Kibatala na John Malya. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 18.


Chanzo: Mwananchi
 
kuna haja ofisi ya DPP ijitathmini na ijihukumu kama ipo huru au inaendeshwa na Ofisi Ndogo ya Chama Lumumba na kama haipo huru iombe reformation. Wanaamrishwa kufungua kesi na CCM, kesi zisizo na mashiko ya kisheria na gharama inakuwa kwetu walipa kodi maskini wa nchi hii. Huyo aliyeamuru kesi zifunguliwe anakula tu uroda na vimada wake. Mfano hii kesi, anaachwaje aliyefoji hati ya mahakama na kuleta taharuki na kutosikilizana ndani ya kikao siku ile ya uchaguzi badala yake eti wanakamatwa waliokuwa wanahoji hiyo hali na kutetea demokrasia. Hata JPM afanye kazi vipi, mambo kama haya ya chama chake yakiachwa yaendelee, yanaleta hasara kubwa kwa taifa in terms of time and money. Hao mawakili wa serikali, huo muda wa kushughulikia shauri la kingese kama hili si wangekuwa wanashughulikia mashauri muhimu ya kijinai mfano ubakaji, ujambazi nk
 
Back
Top Bottom