Korosho zinachomwa tena. Hali hii imerudi tena. ili wahi kutokea miaka ya themanini.

MZIMU

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
4,066
1,225
Katika hali ya mshangao mkubwa ukipita mitaani siku hizi utakuta idadi kubwa ya watu wanauza korosho za kuchoma na sio za kubanguliwa kama kawaida yake. Hali hiyo ilinistusha kwa sababu nakumbuka nilipokua mdogo njia pekee ya wakulima kuuza zao la korosho ili kuzichoma kwa kiwango kikubwa na kuziuza kama karanga. Kulikoni? inamaana serekali imeshindwa kuwatafutia wakulima wetu wa korosho masoko ya zao hilo au wananchi wamekasirika juu ya bei wanayo pewa.

Nilibahatika kuumuliza mzee mmoja pale maeneo ya ferry, Kulikoni mbona korosho mnazichoma? Kwa masikitiko akanijibu hakuna soko.

jeeee! Hali hii inatokeaje. Naona kama kunawatu wanatakiwa kujiuzulu hapa. Maana hata mananasi yamesha anza, na Bakhresa sidhani anaweza kuyanunua yote.
 

MZIMU

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
4,066
1,225
kilimo kwanza korosho zinaunguzwa, wakulima wamechanganyikiwa?
 

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
13,999
2,000
Unategemea ukimpa uenyekiti wa bodi ya korosho mtu kama anna abdallah ufanisi na mwelekeo wa zao hilo utapatikana??

Jeikei kuna vitu vingne lawama unajitakia wewe mwenyewe,,anna abdallah na mudhihir mudhihiri ni hopless,na wanadidimiza zao hilo,,

hili pia unasubiri cdm waje walipigie kelele??
 

Endangered

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
924
195
Huwa nasikitishwa sana na haya mambo ya Korosho. Mara utasikia sijui tani elfu kadhaa zimepote, mara tani elfu kadhaa hazijulikani zilipo. Kuna wapumb*** wachache wanachezea akili za wengi, lakini kila lenye mwanzo lina mwisho. Wasipotubu kwa waathirika wa matendo yao, watakuja pata aibu mbaya sana, wamesahau kwamba hakuna atakayeishi milele duniani.
 
Top Bottom