KOROSHO ZA KIASILI ZENYE MAMILIONI YA VITAMINI NA UJENZI WA AFYA YAKO-Kwa ufupi pitia hapa

yassin alluy

Member
Feb 4, 2017
30
225
FAIDA ZA KULA KOROSHO KWA AFYA YAKO.

Ni zao dogo, lakini maarufu duniani. Kwa mtizamo wa kawaida, una weza kulidharau zao hili. Wengi wetu hatuli korosho na hata pale tunapokula, hula kama kitafunwa cha kuchangamsha mdomo tu, na wala siyo kitu muhimu sana kuliwa.
Utafiti uliofanywa kuhusu zao la korosho, umeonesha kuwa korosho ina faida nyingi sana kiafya, hasa katika magonjwa yenye uhusiano na magonjwa ya moyo, kama ambavyo tutaweza kuona katika makala ya leo, na bila shaka kuanzia leo utaanza kuziangalia korosho kwa jichotofauti.

KINGA DHIDI YA UGONJWA WA MOYO
Siyo tu kwamba korosho zina kiwango kidogo cha mafuta (fat), lakini pia zina aina ya mafuta (Monounsaturated Fats) ambayo hutoa kinga kwenye moyo, aina ambayo huweza pia kupatikana kwenye Olive Oil.
Aidha, ndani ya korosho, kuna kirutubisho aina ya Oleic Acid ambacho utafiti unaonesha kuwa kirutubisho hicho huimarisha afya njema ya moyo na huwafaa hata wagonjwa wa kisukari.
Kama kweli unajali sana afya ya moyo wako, basi pendelea kula korosho za kila aina. Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa kwenye jarida la masuala ya virutubisho nchini Uingereza (British Journal of Nutrition), umeonesha kuwa watu waliopendelea kula korosho na bidhaa zake, kama butter, idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa moyo vilipungua kati ya asilimia 11 na 19.
Utafiti huo umeenda mbali zaidi na kubainisha kuwa watu wanaotumia korosho angalau mara nne kwa wiki, walionesha kuondokewa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo (coronary disease) kwa asilimia 37! Na iwapo mtu atakula sana korosho, hatari ya kupatwa na magonjwa huendelea kupungua zaidi.
Dondoo moja ya ulaji korosho na kujiepusha na magonjwa ya moyo yote mawili (coronary na cardiovascular), inasema kuwa chukua kiganja kimoja cha korosho tafuna au kijiko kimoja cha chakula kilicho jaa ‘nut butter’, kula hivyo mara nne kwa wiki.

MADINI YA COPPER, UIMARISHAJI MIFUPA, NISHATI
Licha ya kutoa kinga dhidi ya magonjwa ya moyo, korosho pia ni chanzo kizuri cha madini aina ya copper ambayo ni muhimu sana katika mwili wa binadamu. Halikadhalika, korosho ina madini yanayoimarisha mifupa na kinga ya mwili.

KOROSHO NA UZITO
Kuna imani potofu kuwa kwa kuwa korosho ina mafuta, ukipenda kuzila basi mlaji huenda akanenepa. Imani hiyo si ya kweli kwani utafiti unaonesha kuwa watu wanaopenda kula korosho, angalau mara mbili kwa wiki, hakuna uwezekano wa kuongezeka uzito na badala yake wanaweza kupungua.
Hivyo inashauriwa kupenda kula korosho kwa afya zetu na wala hakuna haja ya kuhofia kuongezeka uzito, badala yaje mlaji ndiye atakaepungua uzito. Elewa kwamba korosho kwa ujumla, ni chanzo kizuri cha madini ya copper, magnesium na phosphorus.

KILO MOJA TUNAUZA 24,000/= Kwa Dar na Kibaha tunakuletea kwenye vituo vya mwendokasi

MIKOANI NI- 29,000/= na usafiri ndani yake

Karibu sana,

Namba zetu ni
0625 50 43 16
0712 58 31 57
0689 55 44 38 whatsapp

Tupo KIBAHA Karibu sana ujipatie huduma bora, Dar tunasambaza mikoani tunatuma kwa uaminifu wa hali ya juu
IMG_20190208_201851_635.jpeg
Screenshot_20190203-223137.jpeg
IMG_20190104_1022081.jpeg
IMG_20190104_1008218.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom