KOROSHO: Wamedanganya tena, mara hii Majaliwa

Safari hii ni Kasim Majaliwa ambaye aliahidi kuwa pesa italipwa mwezi huu. Duh!!
kumbe kasema majaliwa? hukumbuki ile ziara ya April kule mtwara kichaa alisema ameagiza bl50 ziletwe wakulima walipwe na majina ya waliyolipwa yabandikwe? yalibandikwa? walilipwa? sasa kuna kongonjera za kongamano la korosho.atawaita watu ataongeaaaaa. hamna kitu kipya
 
Hadi Leo sijalipwa kilo zisizozidi 500 eti wanaenda ktk kongamano la korosho mbona sijaalikwa ili niwaulize pesa zetu tutalipwa lini?
 
kumbe kasema majaliwa? hukumbuki ile ziara ya April kule mtwara kichaa alisema ameagiza bl50 ziletwe wakulima walipwe na majina ya waliyolipwa yabandikwe? yalibandikwa? walilipwa? sasa kuna kongonjera za kongamano la korosho.atawaita watu ataongeaaaaa. hamna kitu kipya
Kwanza alisema wote wamelipwa atakayeswma hajalipwa mkuu WA mkoa amweke ndani
 
Hili la koro-show! kwa nchi ambazo viongozi ni kwa ajili ya maslahi ya wananchi, wengi wangeisha achia ngazi! imagine jengo kuanguka tuu, gavana kajivua gamba/gwanda
 
Kimyakimya ndio kuzulumiwa kwenyewe huko, bora wadanganywe danganywe huku wabunge wao wakiitwa "Nongwa" ili nao waamke iwapo kusini yote itapigia kura Upinzani nyanda za juu nazo zikipigia kura upinzani kaskazini nayo ikipigia kura upinzani ccm watabakia na Kanda pendwa tu kanda ya ziwa.
Chadema inatakiwa kukomaa na hii kanda ya korosho na iwatumie wabunge nongwa kufanikisha hii oparesheni koro show.
 
Waziri alliyetumbuliwa karibuni ambaye amedumu Kwa siku zisizozidi 206 alidanya kuwa kuna makampuni 6 ambayo yako tayari kununua lakini hatayaweka hadharani kwa sababu anahofia husuda. Lakini ukweli ni kwamba korosho za mwaka jana hazina mnunuzi na za msimu huu pia hazina mnunuzi lakini pia mavuno yatashuka sana Kwa sababu 1. Wakulima wengi wameshindwa kuyaanda mashamba mapema Kwa maana ya palizi, 2. Wakulima wengi wameshindwa kununua pembejeo Kwa maana ya viuwatilivu kwa sababu ya kutokulipwa pesa zao za msimu uliopita
 
Mashamba mengi sana hayajapaliliwa kutokana na ukosefu wa pesa za palizi.

Kwa wilaya ya Masasi Mjini kuna fomu zimetolewa kwa wakulima wote wenye mikorosho waijaze kwa elfu 20 ndipo atauza korosho zake msimu huu. Bila kutoa pesa hupewi fomu na kama huchukui fomu utahesabiwa umeiba korosho .

Yajayo hayafurahishi
Ndio tumefikia hapo?
 
Very sad! 😳😳😳😳

Mashamba mengi sana hayajapaliliwa kutokana na ukosefu wa pesa za palizi.

Kwa wilaya ya Masasi Mjini kuna fomu zimetolewa kwa wakulima wote wenye mikorosho waijaze kwa elfu 20 ndipo atauza korosho zake msimu huu. Bila kutoa pesa hupewi fomu na kama huchukui fomu utahesabiwa umeiba korosho .

Yajayo hayafurahishi
 
tunaingia msimu mwingine wa korosho bila kulipwa pesa zangu za korosho, serikali imenizurumu kilo chache sana sina hata pesa ya kununulia sumu kwa kilimo cha msim huu na sasa tunajiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa
 
Unaanza lini huo uchaguzi?
 
Back
Top Bottom