KOROSHO NGOMA NZITO: Wakulima Watinga ofisini kwa Mkuu wa Wilaya kudai malipo yao

Halafu jiwe sijui anawazaga nini?
Mkulima umemwambia utampa 3300tsh kitu ambacho hata soko halitoi. Kuanzia hapo tu umekula loss.
Bado unatimu ya ukaguzi, nayo hii inahitaji usafiri, chakula, malazi na malipo- hii nayo itabidi ukatoe tu hazina uwape.
Kuna hao wanajeshi waliopiga pilika, posho zao na mafuta ya magari na meli + chakula- hapa napo inabidi ukachomoe hazina.
Bado Korosho hiyohiyo inamtembeza waziri mkuu na mawaziri wengine kila uchao- nao wanahitaji posho + usafiri + malazi.

Mwisho wa siku unanunua kilo kwa 8,000/=tsh
halafu uweke gharama za kugrade maana nadhani wanajeshi wamechanganya grade A, B, C na D pamoja.
Kisha ubangue.
Halafu uendenazo sokoni, sasa sijui utaenda India utandike mkeka chini uuze au sijui itakuwaje!
Jiwe....

Sent using Jamii Forums mobile app
Jiwe halisikii wala kufikiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui kusini kuna mikosi gani, gesi tuliumizwa na sasa koroshow ni utata!!
Kutokufikiri kwa kina kunawaponza .......hili la korosho mwanzoni kabisa mliambiwa soko la dunia bei sio nzuri .....ule mnada wa 2700 mngekubali kuuza korosho watu wasingejinyonga Leo...hakuna ambae angedhurumiwa korosho zake kwa kutaifishwa na kila kitu kingekua sawa ila kiki za wanasiasa zimewapeleka kibra poleni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawajalipwa hata wale wasiohitaji kukaguliwa…. Leo hii unamwita mfanyabishara akae mezani ajadili na wewe namna ya kununua na kubangua korosho...wakati Ulimtoa baruti mara ya kwanza tena kwa kejeli na "madedilaini" kibao… Unasahau kuwa wakati unamtoa baruti...
1. Alikuwa keshakodi ghara huko Mtwara kwa ajili ya kuhifadhia korosho atakazozinunua
2. Alikodi Meli kuleta makontena ya kusafirishia korosho
3. Akalipia kuyashusha bandarini na kuyasafirisha hadi eneo la ghara
4. Anaingia mikataba na wapakiaji, walinzi etc

MARA GHAFRA UNAMPIGA STOP...THEN
1. Anasafirisha makontena matupu kurudi bandarini
2. Anakodi Meli tena kurudisha makontena alikoyatoa
3. Anarudisha ghara alilokodi
4. Anavunja mikataba na wote alioingia nao mikataba ya kazi mbalimbalia.. ulinzi, upakiaji etc

THEN UNAMWITA TENA MTU ULIYEMPITISHA KWENYE HAYO HAPO JUU MKAE MEZANI MJADILI JAMBO LILELILE...!!!!!

YEYE ANGEWEZA?
Tatizo jamaa yetu anaroho mbaya mmno..anapenda na kufurahi wafanyabiashara wakipata hasara.
Sijui ananufaika na nini. Inasikitisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ss Ngozi nyeusi tuna matatizo gani? Hawa wapuuzi ndiyo waliochoma yale mashamba yanayo daiwa kuwa ni ya Zitto, wakidai kuwa anashirikiana na mabeberu?

Na juzi waliandamana wakimpongeza raisi kwa kununua korosho zote? Yaani kuna idadi ndogo sana ya raia wanaosababisha kucheleweshwa kwa ukombozi
 
“Ukaguzi wa mashamba ya wakulima tunashindwa kuuelewa kwanini umekuwa ukifanywa kwa kusuasua, tukiuliza tunajibiwa eti magari hayana mafuta, mimi niko tayari kutoa mafuta na gari langu litumike kufanya ukaguzi kwenye shamba langu na kwa sababu korosho kwangu ndiyo msingi wa kuendesha maisha na sasa sina hela" alisema Khata

Hii inaonyesha ni jinsi gani serikali imefeli
 
Kikao cha wakulima wa koroshow na Mkuu wa wilaya +kamat ya ulinzi na usalama, je mwenyekit wa ccm anaingiaje apo? Kwanin wasiwe wenyeviti wa vyama vyote? Ujinga km huu ndo maana ccm inachukiwa afu tunaona km inahusika iviiii ktk hili la kucheleweshwa kwa malipo ya wakulima wa korosho.
Poor ccm
 
Mimi Ni Mkereketwa wa CCM na sikuunga Mkono uamuzi huo wa Serikal Na humu tumeandika Sana kupinga jambo hili

Mr Lumumba tunaomba ushahidi wa unachosema (hukuunga mkono na ulipoandika), usije kuwa Bendera umeelekea upepo unapoelekea.

Ili wana Lumumba wenzako wajue kuwa Nchi haiendi kwa mihemko
 
Back
Top Bottom