KOROSHO NGOMA NZITO: Wakulima Watinga ofisini kwa Mkuu wa Wilaya kudai malipo yao

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
889
1,000
BAADHI ya wakulima wa korosho, makatibu na wenyeviti wa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) wilayani Masasi mkoani Mtwara, jana walikusanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Selemani Mzee na kupiga kambi nje ya ofisi hiyo kwa zaidi ya saa saba wakishinikiza serikali kulipa fedha za korosho.

Walichukua hatua hiyo kutokana na serikali kutowalipa fedha za korosho, huku baadhi yao wakidai kuwa walipewa ahadi ya kufanyika ukaguzi wa mashamba yao baada ya kubainika korosho walizouza ni zaidi ya kilo 1,500.

Taratibu za malipo kwa walikuma wa zao hilo zinataka mkulima yeyote mwenye kilo zaidi ya 1,500 lazima akaguliwe shamba lake kabla ya malipo kufanyika.

Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Wilaya hiyo, (Mzee) aliamua kufanya kikao maalum cha dharura na wakulima hao akiwa na wajumbe wengine wa Kamati yake ya Ulinzi na Usalama na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Masasi, Eduward Mmavele, ili kwa pamoja kusikiliza malalamiko ya wakulima hao.

Katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano uliopo ofisi ya Mkuu wa Wilaya, mmoja wa wakulima hao ambaye ameuza korosho zake kwenye Chama cha Msingi Tuaminiane (AMCOS), Saidi Khatau, alisema ni miongoni mwa wakulima wanaotakiwa kufanyiwa ukaguzi wa mashamba yao. Alisema wanashangaa kuona ahadi ya serikali ya kukagua mashamba yao haitekelezwi licha ya kuuza korosho.

Alisema wakulima hawajui ni lini serikali itawalipa fedha zao na hawafahamu lini jopo linalofanya ukaguzi wa mashamba ya wakulima litafika shambani kwake, ili aingizwe kwenye orodha ya majina ya wakulima ambao watalipwa fedha zao.

“Ukaguzi wa mashamba ya wakulima tunashindwa kuuelewa kwanini umekuwa ukifanywa kwa kusuasua, tukiuliza tunajibiwa eti magari hayana mafuta, mimi niko tayari kutoa mafuta na gari langu litumike kufanya ukaguzi kwenye shamba langu na kwa sababu korosho kwangu ndiyo msingi wa kuendesha maisha na sasa sina hela, nategemea fedha hizi za korosho ili hata watoto wangu niwaandae kwenda shuleni," alisema Khatau.

Mkulima mwingine wa korosho, Jacob Hokororo, alidai kuuza kilo 1,563 za korosho kwa chama cha Tuaminiane, alidai kuna kundi kubwa la wakulima hajalipwa fedha za mauzo ya zao hilo.

Alisema haoni haja kwa sasa serikali kutumia muda mwingi kukagua mashamba ya korosho kwa kuwa zipo takwimu za miaka ya nyuma kuhusu ukaguzi wa mashamba hayo. Everina Kambulage, mkulima aliyeuza kilo 470 za korosho, alisema kiwango alichouza hakihitaji ukaguzi wa shamba lake, lakini hajalipwa hata senti moja.

Alisema anaiomba serikali kuharakisha mchakato wa wakulima, hasa wenye kiwango kidogo cha korosho, kulipwa fedha zao.

Alisema hali ya wakulima ambao hadi sasa hawajalipwa fedha zao ni mbaya, akidai wanashindwa kuendesha maisha yao kutokana na kukosa fedha.

Kiongozi wa Chama cha Msingi Lulindi AMCOS, Shiraji Athuman, alisema wamepata faraja kukutana na Mkuu wa Wilaya kwa kuwa chama chao ni miongoni mwa vyama ambavyo wakulima bado hawajalipwa fedha zao na hawajaelezwa sababu za kutofanyika kwa malipo hayo.

“Sisi viongozi wa AMCOS kwa sasa tunashindwa kuishi vizuri na familia zetu huko vijijini kwa sababu ya wakulima kutolipwa fedha zao, wanahitaji kufahamu kwanini serikali bado haijawalipa fedha zao hadi sasa na kila siku wanasikia serikali ikisema wakulima wamelipwa. Kwa kweli usalama wa maisha yetu ni mdogo, tunaomba kulipwa," alisema.

Akijibu maombi yao, Mkuu wa Wilaya ya Masasi (Mzee) alisema amesikiliza kwa umakini malalamiko ya wakulima na akasisitiza serikali bado inaendelea kuwalipa wakulima, hivyo kuwataka wawe wavumilivu.

“Nawaomba muwe wavumilivu kwa kuwa kila mkulima ambaye ni mkulima halali, lazima atalipwa fedha zake," alisema.

"Kuhusu suala la ukaguzi wa mashamba, hili nitakaa na wahusika kujua tatizo liko wapi, lakini ni lazima serikali inawalipa wakulima kupitia taratibu zake ambazo zinalenga kuhakikisha anayelipwa ni mkulima halali."

Watinga ofisini kwa DC kudai malipo ya korosho
 

Zesh

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
14,635
2,000
Halafu jiwe sijui anawazaga nini?
Mkulima umemwambia utampa 3300tsh kitu ambacho hata soko halitoi. Kuanzia hapo tu umekula loss.
Bado unatimu ya ukaguzi, nayo hii inahitaji usafiri, chakula, malazi na malipo- hii nayo itabidi ukatoe tu hazina uwape.
Kuna hao wanajeshi waliopiga pilika, posho zao na mafuta ya magari na meli + chakula- hapa napo inabidi ukachomoe hazina.
Bado Korosho hiyohiyo inamtembeza waziri mkuu na mawaziri wengine kila uchao- nao wanahitaji posho + usafiri + malazi.

Mwisho wa siku unanunua kilo kwa 8,000/=tsh
halafu uweke gharama za kugrade maana nadhani wanajeshi wamechanganya grade A, B, C na D pamoja.
Kisha ubangue.
Halafu uendenazo sokoni, sasa sijui utaenda India utandike mkeka chini uuze au sijui itakuwaje!
Jiwe....

Sent using Jamii Forums mobile app
Jiwe halisikii wala kufikiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Zesh

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
14,635
2,000
Sijui kusini kuna mikosi gani, gesi tuliumizwa na sasa koroshow ni utata!!
Kutokufikiri kwa kina kunawaponza .......hili la korosho mwanzoni kabisa mliambiwa soko la dunia bei sio nzuri .....ule mnada wa 2700 mngekubali kuuza korosho watu wasingejinyonga Leo...hakuna ambae angedhurumiwa korosho zake kwa kutaifishwa na kila kitu kingekua sawa ila kiki za wanasiasa zimewapeleka kibra poleni

Sent using Jamii Forums mobile app
 

dabluz

JF-Expert Member
Feb 28, 2013
2,406
2,000
Hawajalipwa hata wale wasiohitaji kukaguliwa…. Leo hii unamwita mfanyabishara akae mezani ajadili na wewe namna ya kununua na kubangua korosho...wakati Ulimtoa baruti mara ya kwanza tena kwa kejeli na "madedilaini" kibao… Unasahau kuwa wakati unamtoa baruti...
1. Alikuwa keshakodi ghara huko Mtwara kwa ajili ya kuhifadhia korosho atakazozinunua
2. Alikodi Meli kuleta makontena ya kusafirishia korosho
3. Akalipia kuyashusha bandarini na kuyasafirisha hadi eneo la ghara
4. Anaingia mikataba na wapakiaji, walinzi etc

MARA GHAFRA UNAMPIGA STOP...THEN
1. Anasafirisha makontena matupu kurudi bandarini
2. Anakodi Meli tena kurudisha makontena alikoyatoa
3. Anarudisha ghara alilokodi
4. Anavunja mikataba na wote alioingia nao mikataba ya kazi mbalimbalia.. ulinzi, upakiaji etc

THEN UNAMWITA TENA MTU ULIYEMPITISHA KWENYE HAYO HAPO JUU MKAE MEZANI MJADILI JAMBO LILELILE...!!!!!

YEYE ANGEWEZA?
Tatizo jamaa yetu anaroho mbaya mmno..anapenda na kufurahi wafanyabiashara wakipata hasara.
Sijui ananufaika na nini. Inasikitisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Waziri wa Kaskazini

JF-Expert Member
Dec 12, 2015
6,118
2,000
Hivi ss Ngozi nyeusi tuna matatizo gani? Hawa wapuuzi ndiyo waliochoma yale mashamba yanayo daiwa kuwa ni ya Zitto, wakidai kuwa anashirikiana na mabeberu?

Na juzi waliandamana wakimpongeza raisi kwa kununua korosho zote? Yaani kuna idadi ndogo sana ya raia wanaosababisha kucheleweshwa kwa ukombozi
 

Nas Jr

JF-Expert Member
May 15, 2018
3,592
2,000
“Ukaguzi wa mashamba ya wakulima tunashindwa kuuelewa kwanini umekuwa ukifanywa kwa kusuasua, tukiuliza tunajibiwa eti magari hayana mafuta, mimi niko tayari kutoa mafuta na gari langu litumike kufanya ukaguzi kwenye shamba langu na kwa sababu korosho kwangu ndiyo msingi wa kuendesha maisha na sasa sina hela" alisema Khata
Hii inaonyesha ni jinsi gani serikali imefeli
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom