KOROSHO NGOMA NZITO: Wakulima Watinga ofisini kwa Mkuu wa Wilaya kudai malipo yao

Hawa Jamaa wa Kusini si Waliandamana Kupongeza Juhudi za Serikali KUNUNUA KOROSHO ZAO kwa 3,300

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio maana hicho kikao cha DC kamuita Mwenyekiti wa CCM wilaya. Unajiuliza wa nini katika kikao cha utendaji? lakini jubu ni kuwa CCM ndio wanatumika kuhadaa watu waandamane kupongeza juhudi (koko) mbele ya kamera na vipaza sauti.
Sasa juhudi koko zimewatokea puani wamakonde wamechacha, ukitema nchale ukimeza nchale.
Labda watumie tena wanajeshi kuwakong'ota kama wakati wa gas. Ila nao wacha wapigwe tuu, walikuwa na sababu gani kumrudisha Mkuchika na Ghasia bungeni? najua wanaiba sana kura, lakini kama kwenye kura elfu 40 anaambulia 300 za ukoo wake tuu wataibaje?
 
Hakuna kushindwa kitu. Mlisema ndege haziji mpaka sasa tuna ndege tano mpyaaa!! Mradi wa Umeme wa Maji wa Rufiji mlisema hautaanza tayari umeanza! SGR mlisema haiwezekani Novemba 2019 train ya umeme inaanza kati ya Dar na Moro just to mention few projects!! Hapa Kazi Tu ukitaka umbeya na usaliti nenda Chadomo!!
Akili kama hizi za huyu Jamaa anaejiita UCD

Ni hatari sana kwa Afya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Ndo Maana Hata JPM mwenyewe kuna kipindi huwa ana wadharau baadhi ya wanaCCM wenye akili kama za UCD.

Wenzio wanaCCM kindakindaki humu kina jingalao, Pohamba na wengineo huwa wanatulia kwanza

Wanasoma na kupangua hoja kimkakati, wakiona hoja imekaa hovyo wanaamua tu kupita kimya kimya.

Na sio kukurupuka tu na kuleta Majibu kichefuchefu ili uonekane wewe ni mwanaCCM mzalendo sana.

Na Ndo Maana skuhizi JPM kaamua, Anachukua tu Watu kutoka Upinzani na Kuwapa Vyeo.

watu kama nyie hamfai kwa Afya ya chama.

Mambo ya msingi&Maendeleo kwa ujenzi wa Taifa letu,

Wewe unajitoa tu ufahamu eti ili uonekane unauchungu sana na KUKIPIGANIA CHAMA.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akili kama hizi za huyu Jamaa anaejiita UCD

Ni hatari sana kwa Afya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Ndo Maana Hata JPM mwenyewe kuna kipindi huwa ana wadharau baadhi ya wanaCCM wenye akili kama za UCD.

Wenzio wanaCCM kindakindaki humu kina jingalao, Pohamba na wengineo huwa wanatulia kwanza

Wanasoma na kupangua hoja kimkakati, wakiona hoja imekaa hovyo wanaamua tu kupita kimya kimya.

Na sio kukurupuka tu na kuleta Majibu kichefuchefu ili uonekane wewe ni mwanaCCM mzalendo sana.

Na Ndo Maana skuhizi JPM kaamua, Anachukua tu Watu kutoka Upinzani na Kuwapa Vyeo.

watu kama nyie hamfai kwa Afya ya chama.

Mambo ya msingi&Maendeleo kwa ujenzi wa Taifa letu,

Wewe unajitoa tu ufahamu eti ili uonekane unajua sana KUKIPIGANIA CHAMA.



Sent using Jamii Forums mobile app
Kabisa wengi tu wakiona hii imewakaria kooni,wanapita kimya kimya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BAADHI ya wakulima wa korosho, makatibu na wenyeviti wa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) wilayani Masasi mkoani Mtwara, jana walikusanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Selemani Mzee na kupiga kambi nje ya ofisi hiyo kwa zaidi ya saa saba wakishinikiza serikali kulipa fedha za korosho.

Walichukua hatua hiyo kutokana na serikali kutowalipa fedha za korosho, huku baadhi yao wakidai kuwa walipewa ahadi ya kufanyika ukaguzi wa mashamba yao baada ya kubainika korosho walizouza ni zaidi ya kilo 1,500.

Taratibu za malipo kwa walikuma wa zao hilo zinataka mkulima yeyote mwenye kilo zaidi ya 1,500 lazima akaguliwe shamba lake kabla ya malipo kufanyika.

Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Wilaya hiyo, (Mzee) aliamua kufanya kikao maalum cha dharura na wakulima hao akiwa na wajumbe wengine wa Kamati yake ya Ulinzi na Usalama na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Masasi, Eduward Mmavele, ili kwa pamoja kusikiliza malalamiko ya wakulima hao.

Katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano uliopo ofisi ya Mkuu wa Wilaya, mmoja wa wakulima hao ambaye ameuza korosho zake kwenye Chama cha Msingi Tuaminiane (AMCOS), Saidi Khatau, alisema ni miongoni mwa wakulima wanaotakiwa kufanyiwa ukaguzi wa mashamba yao. Alisema wanashangaa kuona ahadi ya serikali ya kukagua mashamba yao haitekelezwi licha ya kuuza korosho.

Alisema wakulima hawajui ni lini serikali itawalipa fedha zao na hawafahamu lini jopo linalofanya ukaguzi wa mashamba ya wakulima litafika shambani kwake, ili aingizwe kwenye orodha ya majina ya wakulima ambao watalipwa fedha zao.

“Ukaguzi wa mashamba ya wakulima tunashindwa kuuelewa kwanini umekuwa ukifanywa kwa kusuasua, tukiuliza tunajibiwa eti magari hayana mafuta, mimi niko tayari kutoa mafuta na gari langu litumike kufanya ukaguzi kwenye shamba langu na kwa sababu korosho kwangu ndiyo msingi wa kuendesha maisha na sasa sina hela, nategemea fedha hizi za korosho ili hata watoto wangu niwaandae kwenda shuleni," alisema Khatau.

Mkulima mwingine wa korosho, Jacob Hokororo, alidai kuuza kilo 1,563 za korosho kwa chama cha Tuaminiane, alidai kuna kundi kubwa la wakulima hajalipwa fedha za mauzo ya zao hilo.

Alisema haoni haja kwa sasa serikali kutumia muda mwingi kukagua mashamba ya korosho kwa kuwa zipo takwimu za miaka ya nyuma kuhusu ukaguzi wa mashamba hayo. Everina Kambulage, mkulima aliyeuza kilo 470 za korosho, alisema kiwango alichouza hakihitaji ukaguzi wa shamba lake, lakini hajalipwa hata senti moja.

Alisema anaiomba serikali kuharakisha mchakato wa wakulima, hasa wenye kiwango kidogo cha korosho, kulipwa fedha zao.

Alisema hali ya wakulima ambao hadi sasa hawajalipwa fedha zao ni mbaya, akidai wanashindwa kuendesha maisha yao kutokana na kukosa fedha.

Kiongozi wa Chama cha Msingi Lulindi AMCOS, Shiraji Athuman, alisema wamepata faraja kukutana na Mkuu wa Wilaya kwa kuwa chama chao ni miongoni mwa vyama ambavyo wakulima bado hawajalipwa fedha zao na hawajaelezwa sababu za kutofanyika kwa malipo hayo.

“Sisi viongozi wa AMCOS kwa sasa tunashindwa kuishi vizuri na familia zetu huko vijijini kwa sababu ya wakulima kutolipwa fedha zao, wanahitaji kufahamu kwanini serikali bado haijawalipa fedha zao hadi sasa na kila siku wanasikia serikali ikisema wakulima wamelipwa. Kwa kweli usalama wa maisha yetu ni mdogo, tunaomba kulipwa," alisema.

Akijibu maombi yao, Mkuu wa Wilaya ya Masasi (Mzee) alisema amesikiliza kwa umakini malalamiko ya wakulima na akasisitiza serikali bado inaendelea kuwalipa wakulima, hivyo kuwataka wawe wavumilivu.

“Nawaomba muwe wavumilivu kwa kuwa kila mkulima ambaye ni mkulima halali, lazima atalipwa fedha zake," alisema.

"Kuhusu suala la ukaguzi wa mashamba, hili nitakaa na wahusika kujua tatizo liko wapi, lakini ni lazima serikali inawalipa wakulima kupitia taratibu zake ambazo zinalenga kuhakikisha anayelipwa ni mkulima halali."

Watinga ofisini kwa DC kudai malipo ya korosho
huyu mnyapara na wasaidizi wake ni wamechoka na kuishiwa maarifa hivi hizo gharama za mafuta ya kukagulia mashamba yote hayo na magari watapata wapi? na hapo wapo mkoa mmoja tu mwezi wa tatu huu sasa? shule zinafunguliwa wiki ijayo. kisha jitu mwakani linapiga kura
 
Hakuna kushindwa kitu. Mlisema ndege haziji mpaka sasa tuna ndege tano mpyaaa!! Mradi wa Umeme wa Maji wa Rufiji mlisema hautaanza tayari umeanza! SGR mlisema haiwezekani Novemba 2019 train ya umeme inaanza kati ya Dar na Moro just to mention few projects!! Hapa Kazi Tu ukitaka umbeya na usaliti nenda Chadomo!!
Q.uma wa uwanja wa fisi
 
Korosho halali ilinunuliwa, hiyo yenye mashaka kuna ulazima wa kuthibitisha mashaka hayo.Wajanja wengi pia walijitokeza namaanisha walanguzi wanyonya wakulima.Kama mkulima alilima korosho yake hakika atalipwa. subira inahitajika
 
Kabisa wengi tu wakiona hii imewakaria kooni,wanapita kimya kimya

Sent using Jamii Forums mobile app
Afu teuzi zikitoka, JPM kateua waliotoka upinzani.

Utaskia jitu linalalamika,

"Kwanini amteue aliekua mpinzani.
Hii sio halali, anatuacha sisi tuliokipigania chama na Kulala maporini kwa ajili ya CCM"

Anasahau kua,
Kwa uwezo wake mdogo kichwani ndo Uliommyima chance.

JPM nae ni binadamu,
Ndo Maana nae sometimes huwa anakubali kua Kuna vitu Haviko FAIR.

Mfano;
Kama lile LA KIKOKOTOZI,
Alikubali kabisa kua Serikali yake nayo imechangia kuifilisi mifuko.

Lakini akatuliza akili na KUONA HALIJAKAA SAWA, kua Kustaafu sio dhambi na Mstaafu asibebeshwe zigo hilo.

Na Dada Irene alivyoshupaza Shingo, AKALIWA KICHWA.

KWAHYO;
Hizo pumba wanazojibu humu kwenye mitandao ili waonekane kwenye mbele ya JPM kua wanakipigania chama.

Na yeye mwenyewe huwa anachekecha na KUGUNDUA KUA ANA BAADHI YA WANACCM Vilaza.

Na tunakoelekea,
Naamini wengi wa wanaCCM watakuja kuvuliwa Uanachama kwa makosa kama haya ya KUONGEA PUMBA kwenye mitandao ya kijamii kama huyu UCD

MAANA,
Wanakidhalilisha sana
Chama Tawala Kikubwa cha Pili DUNIANI.

Wanakidhalilisha sana,
Chama cha Mzalendo Nambari Moja Tanzania, Raisi wetu Mpendwa JPM.

Wanakidhalilisha sana,
Chama cha Mapinduzi CCM





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani amekuambia mimi najibu hapa kama CCM? CCM inamsemaji wake halafu umequote hiyo comment yangu bila kujua kuwa hiyo ni mwendelezo wa comments nyingi tulizokuwa tunajibishana na Mmawia sasa wewe unadandia tu katikati ya comments. Ukitaka kujua what transpired rudi nyuma ujue yaliyojiri la sivyo piti kimyakimya mkuu.
Jinga ww
 
Jpm alikuwa na yupo sahihi maana suala kama hili lazima ingetokea changamoto, na nahisi serikali sikivu imeshaona ilo changamoto,kwaiyo msimu mwingine malalamiko yataisha kabisa. Mlitegemea changamoto za hapa na pale hazitotokea?



Sent using Jamii Forums mobile app
ACHA BASI KUHISI.. WEKA FACT ZINAZOKUPA HISIA HIZO..!!!
 
Back
Top Bottom