Korogwe: Watu 6 wafariki Dunia, 19 wajeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka

Katika nchi za Africa mashariki Tanzania inaongoza Kwa ajili hii inatokana na barabara zetu za hovyo na miundombinu ya kijinga
Mara nyingi baadhi ya madereva Wana kimbiza sana magar hasa hiz Costa Zina kimbiaga sana Hata huki Kanda ya kaskazin Arusha moshi Costa Zina ongoza Kwa speed sana ,na uendeshaji wa hao madereva ni WA hovyo sana
 
Katika nchi za Africa mashariki Tanzania inaongoza Kwa ajili hii inatokana na barabara zetu za hovyo na miundombinu ya kijinga
Poleni sana ndugu wa wafiwa na walioumia, Tuwaombee.
Pamoja na mwendo kasi, lakini pia barabara zina kasoro kwenye kona. Kama kuna kona kali lazima barabara itengenezwe kwa kuinamia ndani ya mzunguko, lakini utakuta pawe na kona pasiwe na kona barabara iko vile vile.
Road construction should consider centripetal force
1649772689543.png
 
Na spidi 180 kazi yake ni nini? Ziondolewe.
Kuna muda wa kuitumia na muda wa kutoitumia, full light unaweza usione mashimo mbele yako.
umesema full light inakufanya usione barabara

sasa ni wakati gani inatumika ambapo huhitaji kuangalia barabara, ni pale unapoangalia mawingu kwenye sun roof?
 
Chanzo cha ajali: Mwendokasi kwenye kona.

Je inahusiana vipi na sababu uliotoa hapo juu
Ni kweli kuna uzembe mwingi Kwa baadhi ya madereva hasa kwenye mwendokasi lkn pia miundombinu yetu wabongo sio rafiki....Kwa mfano barabara ya kwenda mtwara jaribu kupita utaona jinsi ulivyokuwa nyembamba alafu ina viraka kutoka hapa DAR mpaka unafika MTWARA
 
SITA WAFARIKI KWA AJALI TANGA.

Kutoka Tanga.

Watu sita wamefariki Dunia na wengine 19 wamejeruhiwa baada ya gari waliokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Akithibitisha kutokea Kwa ajali hiyo kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Safia Jongo amesema ajali hiyo imetokea eneo la Kwamdulu ambapo gari aina ya Coastal yenye namba za usajili T833 DMH kuacha njia na kupinduka.

Kamanda Jongo amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospital ya wilaya ya Magunga Korogwe.Na majeruhi wanaendelea kupata matibabu hospitalini hapo.

Aidha chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa kuwa ni mwendo kasi aliokuwa nao dereva hivyo kushindwa kukata kona na gari kutelezaa kisha kupinduka na wito Kwa watumiaji wa vyombo vya Moto barabarani kufuata sheria ili kuzuiya ajali zinazoweza kuepukika.

Kwa upande wake mganga Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Dk Salma Swedi amethibitisha kupokea miili 6 na majaruhi 19 na kwamba majeruhi wawili hali zao nii mbaya na wanatarajiwa kupelekwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo.

Endelea kuwa karibu nasi kwa taarifa zaidi.

Korogwe once again
 
Back
Top Bottom