Korogwe, Tanga: TANESCO wanawaibia wananchi wa hali ya chini

Steph JK

Senior Member
Sep 14, 2018
103
106
Habari

Bei ya umeme ipo katika viwango tofauti tofauti na kiwango Cha chini ni kinatambulika kwa D1 ambapo katika kiwango hicho Kuna watumiaji wa majumbani wadogo ambao matumizi yao hayazidi unit 75 na wale wa zaidi ya 75.

Bei ya wasio zidi 75 ni sh. 100 bila kodi.

Aidha, TANESCO wilaya ya Korogwe mkoa wa Tanga wanawateja wa makundi hayo yote, miezi miwili iliyopita wameamua kuwapandishia bei watumiaji wadogo toka kiwango Cha sh.100 kwa unit moja Hadi sh. 250 kwa kwa unit kwa kigezo Cha kufanya uchunguzi Kama kweli ni mtumiaji mdogo. Jambo ambalo halina maana kwani kwenye mfumo wa TANESCO inaonesha matumizi ya mteja huyo jivyoni rahisi kujua Kama ni mdogo au mkubwa.

Uthibitisho kuwa ni wizi suala Hilo linafanyika Korogwe tu, na Wala sio Handeni au Muheza Wala Tanga mjini.

Kwa hili walifanyalo wanalipisha wateja gharama kubwa kuliko wanazo paswa, aidha nilijaribu kuwasiliana na TANESCO makao makuu hawajui suala Hilo.

Tunaomba wenye Mamlaka mshughulikie wizi huu ambao unaongeza hasira kwa wananchi dhidi ya Serikali yao.
 
Watumishi wengine wa mashirika ya serikali na kada zake ni wapinzani kwahiyo wanatumia kila aina ya mbinu kuichafua serikali.

Rejea tukio la Egypt baada ya Muhammad Mursy kushinda uchaguzi.
 
Mkuu sijaelewa hapo kwenye units...mfano huku Dsm tsh 1000 unapata unit 2.9 maana ake unit moja ni tsh 345.

Wewe unaongelea unit moja tsh 100 au 250.
 
Sh. 100 bila kodi Wala REA ambapo sawa na sh. 120 na hiyo nyingine ni sh. 356
 
TANESCO wanamfumo ambao una control manunuzi ya umeme nchi nzima. Mteja kuwa D1 kunatakiwa kuwe na vigezo kwa mujibu wa miongozo ya Regulator ambaye ni EWURA. Pamoja na mteja kuwa matumizi chini ya Unit 75 hiyo haitoshi kuwa ni kigezo pekee. Naomba upitie miongozo ya EWURA utaelewa zaidi.
 
Back
Top Bottom