Korogwe: Mkurugenzi afunga ofisi na kuja jina la mgombea wa CCM. Mgombea wa CHADEMA nusura aporwe fomu

Ushauri mzuri lakini nina hakika uongozi unajua unachokifanya tatizo ni nyinyi wanachama mlio gizani hamjui kinachoendelea huko ndani!
 
Watanzania tuna matatizo ambayo ni vigumu kusaidika. Kama sio upinzani kuonyesha kwamba serikali inawakandamiza na kuwaonea wananchi, inawanyang'anya haki yao ya kuchagua wawakilishi sijui nani tena angewaonyesha.

Sio kweli kwamba wananchi wanahitaji kuelekezwa cha kufanya pale haki na demokrasia inapominywa, wanasema waje na plan B, chadema inaweza kuminywa kama institution isiwe na mgombea, but infact, wananchi ndio walionyang'anywa haki yao.
Wananchi/WaTz wanatakiwa kuamka na kukataa huu ujinga.
Hakuna anaejigusa, tunalaumu vyama vya upinzani kwamba hawafanyi kitu...sijui watu wanataka wabebwe mgongoni?

Wanaominya haki zenu si mnakaa nao huko mitaani? Need I say more....plan B hiyo. Tumeni ujumbe. Otherwise mnyamaze milele jwa kuwa nyie ni wacha mungu, mkipigwa kofi shavu la kulia mnageuza na shavu la kushoto nalo lipashwe joto.

Roger.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui cdm wamekumbwa na shida gani, wana ushahidi wa wazi lakini hawaendi mahakamani. watetezi utasikia huko mahakamani ni kupoteza muda. Sasa wanashiriki uchaguzi hiyo tume ndio inatenda haki?
Kwa sababu ni Jana tu ndo wamemwandikia mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wakilalamikia suala hili na kumuomba apokee fomu za mgombea wao, tunataraji hatua zaidi zitafuata baada kumtanganza mgombea wa CCM kupita bila kupingwa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ikiwa uchaguzi wa Korogwe mgombea wa CCM atapita bila ushindani hakika mnatengeneza anguko kubwa kwasababu sasa wapenzi wenu wataanza kukata tamaa jinsi mlivyo wazembe na msiochukua taadhari mapema.

Korogwe ni jimbo moja tu mnashindwa kurejesha fomu je majimbo 200 hali itakuwaje????
Kwani nawewe mlevi Kama waitara au magonywa ya utotoni yanaanza kukuludia?
 
Nijaribu tu kuwashauri wanachadema wote wakiongozwa na mgombea ubunge
kwa namna ingne naona ni sawa tu,kwani hata akithibitishwa huyo mgombea ccm watashinda tu!sasa kuokoa gharama acha apite bila kupingwa
 
Maelezo ya kilichotokea wakati wagombea wanarudisha form za uteuzi kwa msimamizi wa uchaguzi ambae ni Mkurugenzi wa Halmashauri huko Korogwe,yanapatikana katika account ya twitter ya Halima Mdee ambapo mtu aliemsindikiza mgombea wa CHADEMA anatoa ushuhuda wa kilichotokea.

Hakika awamu hii kuna mambo ya hovyo sana na civilisation hivi sasa ni zero kabisa katika siasa zetu.

Alafu kwa unafiki bila aibu utawasikia wakisema, "tumtangulize Mungu mbere!"

Ningeweza kukopi hiyo video na kuileta humu ila taratibu za JF ndio zinakwamisha.
Mzee acha kuruka ruka, weka hata link basi. Siku hizi sikuelewi kabisa mkuu wangu, umekuwa mtu wa kuandika kimajungumajungu
 
Ikiwa uchaguzi wa Korogwe mgombea wa CCM atapita bila ushindani hakika mnatengeneza anguko kubwa kwasababu sasa wapenzi wenu wataanza kukata tamaa jinsi mlivyo wazembe na msiochukua taadhari mapema.

Korogwe ni jimbo moja tu mnashindwa kurejesha fomu je majimbo 200 hali itakuwaje????
Spite bila kupingwa mara ngapi? Chama ambacho kinashindwa kufanya timing ni chama mfu kabisa. Chadema ni saccos tu n sio chama cha kisiasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maelezo ya kilichotokea wakati wagombea wanarudisha form za uteuzi kwa msimamizi wa uchaguzi ambae ni Mkurugenzi wa Halmashauri huko Korogwe,yanapatikana katika account ya twitter ya Halima Mdee ambapo mtu aliemsindikiza mgombea wa CHADEMA anatoa ushuhuda wa kilichotokea.

Hakika awamu hii kuna mambo ya hovyo sana na civilisation hivi sasa ni zero kabisa katika siasa zetu.

Alafu kwa unafiki bila aibu utawasikia wakisema, "tumtangulize Mungu mbere!"

Ningeweza kukopi hiyo video na kuileta humu ila taratibu za JF ndio zinakwamisha.

sasa kwanini hii taarifa umeileta huku??

si ungeiwacha huko huko tweeter
 
Si la Korogwe tu Mkuu, hadi Buyungu issue Ni the same.

Karatasi Za matokeo Buyungu zimewapa ushindi lakini hawaendi court, what's wrong with CDM
Wakienda mahakamani watageuziwa kesi.

Mahakama na nec wote wametumwa kufanya kazi moja.

Solution ni tume huru ya uchaguzi. Basi
 
Hili ni jambo linaloshangaza wengi, na kufanya watu waamini kwamba huenda hata hivi vyama vinavyojitambulisha kuwa ni vya upinzani vina njama tusiyoielewa wananchi.

Haiwezekani wawe wanalalamika tuuu kila mara kwamba wanaonewa, halafu hawataki angalao kufuatilia haki na kutoa ushahidi uliowazi kwamba kweli wanaonewa kila mahali, hadi mbele ya sheria mahakamani.

Wao walichojua ni kuwa maandamano na mikutano ilizuiwa, wakiandamana wanapigwa, wakifanya mikutano wanapigwa, lakini hawapo tayari kufuata taratibu za kutafuta haki zao ili wananchi wote waone haki hizo zinavyonyimwa katika ngazi zote, bungeni hadi mahakamani. Hawataki kabisa kujihangaisha tena. Sijui walishahitimisha kwamba wananchi wameona vya kutosha jinsi wanavyoonewa na hakuna lazima tena kuendelea kuonyesha jitihada zao katika kutafuta haki hizo na ushahidi zaidi! Hawalazimishwi, kama wamechoka waachane kabisa na siasa? Inafaa kitu gani kuendelea kuwatia watu matumaini ya kuwepo mabadiliko huku watu wanaotegemewa kuongoza mabadiliko hayo hawana msisimko nayo. Hili linafanya tuwafikirie kuwa watafuta riziki tu mwanya ukipatikana. Usipopatikana, wanaendelea tu na maisha ya kubangaiza, mradi mkono uende kinywani.

Sasa chukulia jambo kama hili, la mtu tu anaamua kukiuka taratibu maksudi kabisa na kiburi. Wapinzani wanataka wananchi wajue tu kuwa wameonewa na huyu mtumishi, basi liishie hapo? Wanataka kutuambia "sasa tufanye nini kwa vile haturuhusiwi kuandamana kumzuia huyo mtu asituonee. Yangekuwa maandamano yanaruhusiwa leo pasingetosha, kama mlivyokuwa mnaona wenyewe enzi zile"?
Kuna kiasi cha kuonyesha huruma, ikizidi kiasi hicho hata wananchi wataona kuwa hawa hawastahili kuonewa huruma.

Tatizo letu Watanzania tunaongea Na kulaumu vyama vya upinzani kama hayatuhusu vilee..

Hayo mashinikizo hayawezi kuleta matunda kama Sisi Wananchi hatutaamua kushiriki moja kwa moja kwenye kudai haki.

Tukumbuke vyama vya upinzani sio viongozi wake, vinajengwa Na Sisi Wananchi tunaochukizwa Na hali hii ya uminywaji wa haki na demokrasia...Ambao wengi wetu ni waoga wakujitokeza waziwazi Na kuunganisha nguvu zetu kupambana Na utawala huu. Badala yake tunataka jukumu hilo lifanywe Na watu wengine huku Sisi tukinyoosha miguu majumbani mwetu tukisubiri matunda. Ni uzwazwa.

Ni ama tukae kimya tusulubiwe ama tutoke majumbani mwetu tukapambane....tuache unafiki.
 
Mzee acha kuruka ruka, weka hata link basi. Siku hizi sikuelewi kabisa mkuu wangu, umekuwa mtu wa kuandika kimajungumajungu
Kama unaweza kuingia JF,unashindwa nini kuingia katika twitter?

Nikiweka hiyo link address hapa italeta tweet nzima(video na comments za watu) kitu ambacho JF hawaruhusu(hotliking).
 
Ikiwa uchaguzi wa Korogwe mgombea wa CCM atapita bila ushindani hakika mnatengeneza anguko kubwa kwasababu sasa wapenzi wenu wataanza kukata tamaa jinsi mlivyo wazembe na msiochukua taadhari mapema.

Korogwe ni jimbo moja tu mnashindwa kurejesha fomu je majimbo 200 hali itakuwaje????

Mkuu ule uzi uliotundikwa humu Siku ya tarehe 20,August,2018,kwenye majira ya saa tano na dakika kadhaa(siku ya urejeshwaji wa fomu) uliuona?

Utafute humu.... Ndo Majibu ya hilo Swali na lawama zako Kwa CHADEMA.
 
kwa sasa Tanzania inaongozwa na Mfumo wa chama kimoja kwa Pesa inayotumika kudhoofisha upinzani ni pesa nyingi sana ni pesa ambazo zingeweza kuleta maendeleo makubwa Tanzania yote ikiwemo kujenga nyumba za watumishi wa umma kule Dodoma na wote wangeweza kuishi kwenye makazi salama, lakini badala ya maendeleo CCM wanatumia pato la Taifa kukandamiza demokrasia kwa kuwabambikia kesi wapinzani, kuwapora ushahidi kwenye chaguzi mbalimbali kwa kutumia Polisi ni aibu kubwa kwa Nchi ya amani kama Tanzania kuendelea kupandikiza Chuki kwa wananchi.
Mtaishia kulalama,yabayofanyika leo hayakuwa mageni toka enzi hizo, tena yalikuwa zaidi kipindi chadema inawika kama jogoo...Ila walibanana...
 
inawezekana pesa ya kugharamia haya manunuzi imeanza kukata, hivyo jiwe ametoa maagizo zitumike 'short-cut'
 
Maelezo ya kilichotokea wakati wagombea wanarudisha form za uteuzi kwa msimamizi wa uchaguzi ambae ni Mkurugenzi wa Halmashauri huko Korogwe,yanapatikana katika account ya twitter ya Halima Mdee ambapo mtu aliemsindikiza mgombea wa CHADEMA anatoa ushuhuda wa kilichotokea.

Hakika awamu hii kuna mambo ya hovyo sana na civilisation hivi sasa ni zero kabisa katika siasa zetu.

Alafu kwa unafiki bila aibu utawasikia wakisema, "tumtangulize Mungu mbere!"

Ningeweza kukopi hiyo video na kuileta humu ila taratibu za JF ndio zinakwamisha.

Ktk himaya (lusipher)ya shetani wasaidizi wote lazima wawe mashetani.kwenye ngome ya shetani huwezimkuta malaika na ikiwa malaika atapenya basi vita itakuwa kubwa ndani ya ngome na mwisho lucipher atawatimua wote walozembea na kusababisha malaika aingie katika ngome yao.Ili kuwa na amani lazima kizazi cha Lucipher kifyekwe chote na Lucipher akose nguvu na kujitakasa.
 
Tumechoka na blah blah,wekeni ushahdi kuwa mkurugenzi kakimbia
simu mnazo hata kupiga picha mnashindwa
Dawa hapa ni electronic form submissions. Maana hii tabia imekuwa too much sasa, hata kama ukipewa picha; mtaleta hadithi kama za Mnyeti wakati ni mkuu wa wilaya. Rubbish
 
Back
Top Bottom