Korea yavutiwa uwekezaji umeme Zanzibar

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Umesema mazingira hayo yanawapa moyo wa kuanzisha mradi wao unaokuwa ndani ya bahari masafa ya mita 100, umbali wa ardhi unaoambatana na mita 10 chini ya bahari.

Mwakilishi wa kampuni hiyo, Profesa Injoon Suh, alisema hayo wakati timu yake ikitangaza nia yao ya kutaka kuwekeza mradi wao mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, Vuga Mjini Zanzibar.

Prof. Injoon Suh, alisema, umeme unaozalishwa na kampuni hiyo unaweza kabisa kutumia gesi asilia inayozalishwa nchini Tanzania kwa kuongezea na ile inayopatikana kutoka Mashariki ya Kati.

Alisema kiwango cha umeme utakaozalishwa na kampuni hiyo yenye uzoefu na utaalamu wa masuala ya nishati ya gesi unafikia megawatts 215 kiwango ambacho ni kikubwa kwa Zanzibar kinachoweza kutosheleza mahitaji yote ya huduma hiyo.

Mwakilishi huyo alisema, mradi huo una garentii ya kufanya kazi katika kipindi cha miaka 25 na baadaye kukabidhiwa kwa serikali.

Alieleza kwamba kampuni ya FCCPP ni moja miongoni mwa kampuni 15 zinazofanya kazi kimataifa ndani ya mwamvuli wa kampuni ya kitaifa ya Korea ya VOE Group.

Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, alisema mradi wa uzalishaji wa umeme wa kutumia gesi asilia ni muhimu kwa vile umeonyesha mwelekeo kupungua kwa gharama za matumizi ya huduma hiyo.

Balozi Iddi alisema, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar bado ina nia ya kuwa na chanzo kingine cha umeme utakaokuwa mbadala endapo kutatokea hitilafu kwenye chanzo kimoja otumika hivi sasa Visiwani Zanzibar uri uongozi wa kampuni ya FCCPPa mradi

Chanzo:Nipashe
 
Ifike hatua sasa Zanzibar ijitegemee kwa nishati ya Umeme.
Sidhani kama mahitaji ni makubwa kiasi kwamba Serikali haina uwezo wa kuwekeza katika nishati hii.
 
Umesema mazingira hayo yanawapa moyo wa kuanzisha mradi wao unaokuwa ndani ya bahari masafa ya mita 100, umbali wa ardhi unaoambatana na mita 10 chini ya bahari.

Mwakilishi wa kampuni hiyo, Profesa Injoon Suh, alisema hayo wakati timu yake ikitangaza nia yao ya kutaka kuwekeza mradi wao mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, Vuga Mjini Zanzibar.

Prof. Injoon Suh, alisema, umeme unaozalishwa na kampuni hiyo unaweza kabisa kutumia gesi asilia inayozalishwa nchini Tanzania kwa kuongezea na ile inayopatikana kutoka Mashariki ya Kati.

Alisema kiwango cha umeme utakaozalishwa na kampuni hiyo yenye uzoefu na utaalamu wa masuala ya nishati ya gesi unafikia megawatts 215 kiwango ambacho ni kikubwa kwa Zanzibar kinachoweza kutosheleza mahitaji yote ya huduma hiyo.

Mwakilishi huyo alisema, mradi huo una garentii ya kufanya kazi katika kipindi cha miaka 25 na baadaye kukabidhiwa kwa serikali.

Alieleza kwamba kampuni ya FCCPP ni moja miongoni mwa kampuni 15 zinazofanya kazi kimataifa ndani ya mwamvuli wa kampuni ya kitaifa ya Korea ya VOE Group.

Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, alisema mradi wa uzalishaji wa umeme wa kutumia gesi asilia ni muhimu kwa vile umeonyesha mwelekeo kupungua kwa gharama za matumizi ya huduma hiyo.

Balozi Iddi alisema, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar bado ina nia ya kuwa na chanzo kingine cha umeme utakaokuwa mbadala endapo kutatokea hitilafu kwenye chanzo kimoja otumika hivi sasa Visiwani Zanzibar uri uongozi wa kampuni ya FCCPPa mradi

Chanzo:Nipashe
Hivi balozi Seif Alisema lddi anacheo gani hapo Zanzibar ukitoa uo umakamo wa urais wa zamani
 
Back
Top Bottom