Korea ya Kaskazini na Tanzania:Picha haiko sahihi!

Wako tayari kuwashambulia kwa sababu North na South Korea bado vipo kwenye vita hadi leo. South Korea wala Marekani hawezi kuvamia North Korea unless alete ukorofi kwanza. Ni waste of resources kurusha Rockets wakati chakula hakuna, wamarekani sidhani kama wana shida ya chakula.

Ninachosema mimi ni kuwa North Korea sio mfano wa kuigwa na wala sio mfano mzuri kwa Tanzania, tutapelekana pabaya sana.
Kama tunataka kuiga kwanini tusiige South Korea, Japan etc?

Unauhakika kuwa hawawezi kushambuliwa na Marekani au Korea kusini? Kwanini Mmarekani amlebel kuwa ni Axis of Envil? wanafanya majaribio ya makombola wao, marekani na korea ya kusini yanawahusu nini? Mbona wao wamehifadhi mashehena kibao ya makombola nani anawauliza? Halafu wanakimbilia umoja wa mataifa kuwa iwekewe vikwazo, hivi wamerekani wameambiwa kuwa wao ndio kilanja mkuu wa dunia? Korea sio ya kuigwa lakini tunaweza kuiga moyo wa kufanya kazi kwa ajili ya kuleta maendeleo. Chakula watanunuwa wapi wakati wamewekea vikwazo? Si wanataka wawanyenyekee na kuwalamba miguu ndipo watoe chakula?
 
Sasa adui yako ambaye unapigana nae vita akiwa anatafuta nuclear kivipi isikuhusu?
Moyo wa kufanya kazi au kulazimishwa na kuwekwa kwenye giza na madikteta?
Waache kutengeneza mabomu waendeleze kilimo mambo yatakaa sawa, pia sidhani kama kuna vikwazo kwenye chakula.
 
Na marekani nae aache kuwauzia zana nzito korea kusini. Kwa alliance ya Marekani na Korea kusini ilivyo ni kuwa Silaha za Nuclear za marekani zinaweza kutumika kwa ajili ya kuilinda korea kusini. Sasa kwa nini kaskazini isijihami?

Kilimo wanalima sana tena kuliko sisi watanzania. Hali ya hewa ndio imewaendea vibaya na usije ukakuta nako kwenye hali ya hewa kuna mkono wa marekani maana wanaweza wakafanya chochote ili watimize malengo yao. Si unajua mambo ya Sep. 11 walivyowafanya raia wao ili tu wapate kisingizio cha kwenda kupiga Afghanistani na Iraki?
 
Korea Tambarare?

3089_explorer_inside_north_korea-3_04700300.jpg

Kuna sehemu yoyote bongo kama hiyo?
 
Kuna sehemu yoyote bongo kama hiyo?

Elewa ya kwamba: uzuri wa hiyo picha ni sawa na kaburi lililojengewa kwa nakshi za dhahabu na ndani yake kuna uozo.

Mwananchi wa kawaida wa Korea afaidi hayo majengo ndiyo maana kila kukicha wanatoroka nchi yao. Uchumi na hali bora za maisha ya mwananchi haipimwi kwa majengo marefu peke yake. Umeshaonyeshwa upande wa pili wa shilingi au hicho kipande cha Pyonyang kimekuchanganya.

Ni kheri kuishi kama mtumwa kwenye nchi huru lakini ninayo my concious and dignity kuliko kuishi kama nguruwe aliyenona katika mazingira hayo.
 
shadow.. kuna watu wanataka tuamini kwa vile kuna majengo marefu katikati ya Jiji la Dar na ya kuwa kuna majengo ya zamani yanabomolewa basi "Bongo tambarare"!
 
Nchi ya North Korea kwa miongo mingi sasa imekuwa ikitengwa katika mambo mengi ya jumuiya ya Kimataifa nakuwekewa vikwazo vya kila aina. Na yenyewe ikiwe imejitenga kwa mambo mengi inashangaza kuona kuwa nchi hii ambayo imetajwa kwa kila namna mbaya na nchi za magharibi iko mbele kimaendeleo kuliko Tanzania nchi yenye idadi mara mbili ya watu wa Korea Kaskazini, demokrasia ya vyama vingi, mahusiano mazuri na mataifa ya magharibi n.k

Hata Cuba, Vietnam, China, Venezuela, Uhispania nchi zenye mrengo wa kisoshalisti zinapiga maendeleo mbele kuliko nchi ya kibepari kama ya kwetu. Tatizo ni nini hasa? NI mfumo wa kisiasa, ni mwelekeo wa uongozi, au kitu gani hasa?

Lakini hasa ni North Korea inawezekanaje kataifa kama North Korea kuwawekea ngumu Obama na washirika wake na kuendelea kufanya utafiti wa mambo ya kiteknolojia bila ya kuabudu au kufuata kitabu cha maelekezo kutoka Ulaya na Marekani?

Je na sisi tuwawekee ngumu kina Obama, Brown na wenzake na tuone kama tunaweza kupita hatua za maendeleo mbele? Je kwa kuamua kufanya mambo bila kuwatilia maanani wakubwa hawa yawezekana tukachochea ubununifu wetu wenyewe?

Fikiria kwa nchi kama Tanzania inayopokea misaada mingi, ina marafiki wengi bla bla bla GDP (nominal) = 16.691 Billions USD na Per Capita income ya 428USD. Population yake karibu milioni 40 Literacy level ya tanzan ni 69.4 wakati makadirio ya uhai ni miaka 50 kwa wanaume na 53 kwa wanawake.

North Korea kwa upande wake, pamoja na matatizo yake na kutengwa na jumuiya ya kimataifa GDP yake ni 26.2 Billions USD; Per capita ni 1800USD; population yake ni watu milioni 23 hivi na life expectancy ni miaka 69 kwa wanaume na 75 kwa wanawake. Literacy level ni asilimia 99!! (Hata Marekani haijafika hapo!)

So, why this picture don't make any sense!? Yawezekana uongozi wa kidikteta una manufaa kwa watu wengi zaidi kuliko uongozi wa kina mjomba?

Wee unafikiri misaada ile ni ya bure? lazima ufate mrengo!
 
Jamani.. kama tunapima hali yao mbaya kwa sababu ya wananchi wao kukosa chakula au kutumia resources vibaya.. wana tofauti gani na Tanzania? MBona sisi pamoja na urafiki wetu na magharibi hatujaweza kujitosheleza kwa chakula wala umeme? Hatujaweza hata kurusha kibatari angani!? Kwamba, tunapinga propaganda za DPRK wakati zile za magharibi ndizo tunazikubali?

DPRK wameweza kufanya mengi, mfumo wao wenyewe wa uchumi, siasa zao za Juche n.k labda tunachokosa sisi ni kiongozi mwenye nguvu na hisia za kidikteta hivi maana kama Udikteta unaweza kujenga na kwenda mbali katika teknolojia, miundombinu n.k basi utawala wa demokrasia una matatizo!

Siku zote huwa napata taabu kuelewa hoja ya huyu bwana kuwa ili tuendelee basi ni lazima tuvunje uhusiano na nchi za magharibi [na kukataa misaada]. Ninashindwa kuelewa msingi wa hoja hii. Wakati watu wanajitahidi kupanua mahusiano [from Doha Development Agenda to myriads of PTAs], hoja hii inatueleza tufanye tofauti. Is this based on economic theory? or ni mtizamo tu. I think you are aiming at the wrong target. Ili tuweze kuendelea, ushirikiano na nchi za magharibi ni muhimu mno. They have technology and capital, which we are lacking. Only that, tunahitaji kujua ni nini tunataka.

Nchi zote zilizoendelea ni kwa sababu watu walifanya na wanafanya kazi, na si vinginevyo. Hakuna nchi iliyoendelea kwa sababu ya kuwa isolated. Hata North Korea unayoizungumzia, kama ni kweli wanafanya vizuri kiuchumi [of which I doubt!] ni kwa sababu watu wanafanya kazi, si kwa sababu wako isolated [causal effect!]. Whether tunashirikiana na nchi za magharibi au la, maendeleo yataletwa kwa kufanya kazi, period!
 
shadow.. kuna watu wanataka tuamini kwa vile kuna majengo marefu katikati ya Jiji la Dar na ya kuwa kuna majengo ya zamani yanabomolewa basi "Bongo tambarare"!

MWKJJ tunayo safari ndefu ya kuundoa hayo mawazo kwamba majengo marefu ndo 'utambare' wakati jiji letu halina maji safi ya huakika toka uhuru. Nilikuwa nasoma report ya mtaalamu wa uchumi [De Soto] Anasema Tanzania uchumi wake asilimia 98 huko kwenye sekta isiyo rasmi. Ni asilimia mbili tu ndo hiko kwenye mfumo rasmi. Anasema uchumi huo usiyo rasmi unazarisha zaidi ya mara mbili ya msaada tunaoupokeea kutoka huko Ulaya.

Lakini hakuna kiongozi hata mmoja aliwaza na kufikiria namna gani ya kuuingiza mfumo huo unaoperate nje ya mfumo wa kisasa na kuuoanisha na ule ulio rasmi.
 
Nafikiri serikali inatekeleza mradi mkubwa specifically addressing this issue. Unaitwa MKURABITA. Again, hautafanikiwa sana kwa sababu we are naturally not serious. A well designed policy/project can easily fail due to poor implementation. On the contrary, effective implementation can overshadow a poorly designed policy. So, implementation is the key.
 
Siku zote huwa napata taabu kuelewa hoja ya huyu bwana kuwa ili tuendelee basi ni lazima tuvunje uhusiano na nchi za magharibi [na kukataa misaada]. Ninashindwa kuelewa msingi wa hoja hii. Wakati watu wanajitahidi kupanua mahusiano [from Doha Development Agenda to myriads of PTAs], hoja hii inatueleza tufanye tofauti. Is this based on economic theory? or ni mtizamo tu. I think you are aiming at the wrong target. Ili tuweze kuendelea, ushirikiano na nchi za magharibi ni muhimu mno. They have technology and capital, which we are lacking. Only that, tunahitaji kujua ni nini tunataka.

Nchi zote zilizoendelea ni kwa sababu watu walifanya na wanafanya kazi, na si vinginevyo. Hakuna nchi iliyoendelea kwa sababu ya kuwa isolated. Hata North Korea unayoizungumzia, kama ni kweli wanafanya vizuri kiuchumi [of which I doubt!] ni kwa sababu watu wanafanya kazi, si kwa sababu wako isolated [causal effect!]. Whether tunashirikiana na nchi za magharibi au la, maendeleo yataletwa kwa kufanya kazi, period!

In 46 years you have no "Technology and Capital" do you expect that you will have it in the current situation where people think like you? Mwanakijiji never said we shall stop our relationship with the West, he just asked: Why we have a very good relationship with the west "who have Technology and Capital" and we are still backward and Korean have such bad relations and are better than us? Answer that question first.
 
Sisi Tanzania naona tunakosa vitu vifuatavyo: Uzalendo, Uwajibikaji, na Uadilifu.
Viongozi wetu, hakuna mwenye uchungu na nchi yake. Hakuna anayeshtuka na kuumia pale anapoona nchi nyingine na hata za jirani zinapiga hatua kimaendeleo. Viongozi wetu ndio wanaopata fursa ya kutembelea nchi nyingine hasa zile zilizoendelea., tulitegemea ziara zao zitusaidie katika kuleta maendeleo lakini kinyume chake ziara hizo zinatumika kutafuta BANK ambazo zitawasaidia kuficha fedha za umma walizochota. Tuangalie nchi kama Rwanda ambayo juzi tu wametoka kuchinjana, lakini leo eti unaambiwa nchi hiyo inafanya maajabu katika kuunda na kuboresha miundo mbinu, Technolojia ya habari na mengine chungu nzima. Nchi kama Sudan, ambayo haikupata misaada ya kimaendeleo na kitechnolojia kutoka magharibi, nchi hii inatengeneza siraha za kisasa, wao vifaru, magari ya kivita na mizinga ya kisasa wanajitengenezea, kilimo cha umwagiliaji kimeshamiri kwa kutumia mto nile ambao umeanzia kwetu. Kama kweli viongozi wetu wanauzalendo na nchi yao kwa nini hawashituki pale tunapopitwa na nchi zenye dhiki ya kimaumbile? Nasema viongozi wetu hawana uzalendo. Korea kaskazini, Kiongozi wao ni mzalendo, achilia mbali misaada waliyoipata kutoka kwa washirika wao China na Urusi ambayo ilipunguzwa kutoka na mabadiliko yaliyotokea katika nchi hizo. Hata tukisema Korea kaskazini ilikuwa na msingi mzuri tangu huko nyuma, ni sawa, lakini uzalendo wa viongozi wao wa kupenda nchi yao, kuilinda na maadui wa nje, na kutambua kwamba wao wametengwa ndiko kumepelekea kukaa chini, na kutumia raslimali zao na watalaam wao wenyewe kubuni na kupanga mikakati yenye kuleta maendeleo katika taifa hilo.

Uwajibikaji kwa viongozi wetu haupo. Kinachoonekana kwa sasa viongozi wetu wanatumia muda mwingi kufanya mambo yao binafsi. Kwa wale waliokabidhiwa madaraka ya kuongoza taasisi za serikali, hawashtuki wanapoona taasisi wanazoongoza hazifanyi vizuri na wala hawafikirii kutafuta mbinu mbadala za kumaliza matatizo hayo. Hili naweza kulioanisha na namna viongozi hao waandamizi wanavyopatikana, wanateuliwa, vigezo vya kuteuliwa kwao vimezungukwa na mashaka matupu, mara utasikia huyo amepata nafasi hiyo kwa vile ni mwanamtandao, au walikuwa pamoja jeshini, au amemsadia Mhe. wakati wa kampeni au wanatoka pamoja. Hali kama hii, usitegemee uwajibikaji, zaidi akishindwa kuwajibika na vyombo husika vikambana utaona nyundo kubwa ikitokea juu na wote mnakaa kimyaaaaaaa.

Uadilifu, hapa ndio haswa kumeoza. Hakuna kiongozi anayetumikia taifa mbali na kujishibisha na kuneemesha familia zao. Ushahidi ni matumizi makubwa ya fedha za serikali kwa vitu vya anasa. Naita vya anasa kwa sababu kuna mbadala wa hivyo, magari ya kifahari ya nini wakati taifa linaangamia, posho kubwa kubwa za nini wakati wananchi hawana huduma za kijamii kwenye maeneo yao. Mali za serikali zinatumika kutajirisha baadhi ya viongozi. Angalia ni kiongozi gani anayeishi maisha ya kitanzania? utasikia hekalu hili ni la waziri, au Katibu Mkuu, au mkurugenzi wa Idara ya serikali au duka kubwa/kampuni/au biashara kubwa ni ya mtumishi wa serikali. Kampuni za kigeni nyingi zina mikono ya vigogo. Sasa iweje tuishangae North Korea? au Rwanda? au Botswana?

Mchawi wa maendeleo yetu ni sisi wenyewe kwa kukosa uzalendo, uwajibikaji na uadilifu. Mwizi wa mali ya umma ndiye significant figure katika jamii yetu ya sasa ya kitanzania, sheria za nchi hazimhusu, na wale watakaodiriki kufunua anaponeemekea tindikali za uso ni halali kwako. Tunahitaji mwendawazimu kuiokoa nchi yetu ili tujifananishe na nchi kama china na North korea
 
Lakini hasa ni North Korea inawezekanaje kataifa kama North Korea kuwawekea ngumu Obama na washirika wake na kuendelea kufanya utafiti wa mambo ya kiteknolojia bila ya kuabudu au kufuata kitabu cha maelekezo kutoka Ulaya na Marekani?

Je na sisi tuwawekee ngumu kina Obama, Brown na wenzake na tuone kama tunaweza kupita hatua za maendeleo mbele? Je kwa kuamua kufanya mambo bila kuwatilia maanani wakubwa hawa yawezekana tukachochea ubununifu wetu wenyewe?
Mkuu

North Korea is a Chinese/Russian protégé

BE
 
Mbona na sisi tunauhusiano mzuri tu na Wachina na Warusi, Wamarekani, Waswedi, Waingereza n.k? Tena China tulikuwa kama mtoto wao tulipotoea wapi?
 
Kikubwa ninachowasifu North Korea ni ku maintain national identity. Hawajabadilika kufuatana na matakwa ya IMF or Worl Bank na ndugu zao west. Ili kupata maendeleo ya kweli, watanzania lazima tukubadili kuwa bila kutoa jasho letu wenyewe na kuwa na uongozi makini hatutaweza.
Inatia aibu jinsi
 
Elewa ya kwamba: uzuri wa hiyo picha ni sawa na kaburi lililojengewa kwa nakshi za dhahabu na ndani yake kuna uozo.

Tunalinganisha Korea ya Kaskazini na Tanzania. Je, unataka kunambia uozo uliopo Tanzania ni sawa na uliopo Korea ya Kaskazini?

Mwananchi wa kawaida wa Korea afaidi hayo majengo ndiyo maana kila kukicha wanatoroka nchi yao.

Na wabongo wengi wangepata fursa ya kuondoka nchini mwao wangeondoka pia. Tatizo ni kwamba wengi wao hawana jinsi.

Uchumi na hali bora za maisha ya mwananchi haipimwi kwa majengo marefu peke yake. Umeshaonyeshwa upande wa pili wa shilingi au hicho kipande cha Pyonyang kimekuchanganya.

Ni kweli hali bora za maisha hazipimwi na majengo peke yake lakini majengo ni sehemu ya miundo mbinu ambayo ni essential katika kuleta maisha bora. Sasa tukilinganisha hizi nchi mbili, unataka kunambia sisi (Watanzania) tuna maisha bora kuliko wao (Korea ya Kaskazini)? Ni nani kati ya hizi nchi mbili ambayo imewahi au inaisadia nchi nyenzake katika misaada ya kimaendeleo?

Ni kheri kuishi kama mtumwa kwenye nchi huru lakini ninayo my concious and dignity kuliko kuishi kama nguruwe aliyenona katika mazingira hayo.

Kweli, lakini Watanzania wengi wanaishi maisha duni kuliko hata hao Nguruwe. Usikute hao Nguruwe wanapata milo zaidi ya mitatu kwa siku wakati Watanzania wanaishia kupata mlo mmoja kwa siku.

Hata uspin vipi, kiwango cha maendeleo cha Korea ya Kaskazini kimezidi cha Tanzania tena kwa mbali licha ya vikwazo vyote walivyonavyo. Now can you imagine kama wasingekuwa na hivyo vikwazo vyote walivyonavyo wangekuwa wapi sasa hivi na imagine sisi ndo tungekuwa na hivyo vikwazo tungekuwa wapi sasa hivi.
 
Asante Mwanakijiji,
Hatuhitaji kutengwa na wala kutokutengwa ili tuweze kuendelea. Sisi Tanzania tunakosa kitu kimoja tu, viongozi wetu hawatujui kwanini Tanzania ni masikini, japokuwa baadhi ya Watanzania wanajua kwanini bado hii nchi masikini SANA. Viongozi wetu wao sio masikini, ila watanzania wengi mno (>90%) ni masikini wa kutupa, nadhani hii ndio sababu hawajui kwanini bado Tanzania ni masikini.

Kwa hakika Tanzania tulichokikosa ni uongozi bora tu, uongozi unaotawala kwa mujibu wa sheria, uongozi usiokuwa na viwango viwili vya sheria, utendaji na utoaji wa haki. HAKI YA CHENGE SIO SAWA NA HAKI YA KUBENEA hapa Tanzania!. Wenzetu kama nchina ambao ni mfano mzuri ulioutaja, hakuna mchezo kabisa linapokuja suala la masilahi ya umma. Wote wanaotuhumiwa na kupatikana na hati za rushwa, ufisadi, waliouwa mashirika ya umma, walioingiza vyakula vibovu nchini wangekuwa tayari kesi zao zishamalika siku nyingi na wengi wao kunyonwa tayari. Kumbuka ni juzi tu waliohusika na maziwa ya watoto yenye sumu walihukumiwa kunyongwa nao hawakawizi, sisi bado tunaendelea kulumbana na EPA n.k! Hapa Tanzania ukiharibu TTCL unapelekwa NSSF, ukizamisha BOT unapelekwa Tanesco, bandari, nasaco n.k, sasa tuendelee je wakati hao wahusika tayari wanakuwa wameshaeendelea kwa niaba ya taifa!

Tunahitaji mwendawazimu Tanzania, lakini sio kupokezana kijiti kama Kikwete alivyopokea kutoka kwa Mkapa, kwani anapokea pamoja na mikoba yake!

Viongozi wetu wanafurahia Tanzania kama ilivyo kwa DRC kuendelea tu kuwa sehemu ya kujipatia malighafi kwa mambwana wet wa amerikana na china!

Tres Bien!!........Nono............nina imani wanakusikia
 
Back
Top Bottom