Korea ya Kaskazini na Tanzania:Picha haiko sahihi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Korea ya Kaskazini na Tanzania:Picha haiko sahihi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 5, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 5, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nchi ya North Korea kwa miongo mingi sasa imekuwa ikitengwa katika mambo mengi ya jumuiya ya Kimataifa nakuwekewa vikwazo vya kila aina. Na yenyewe ikiwe imejitenga kwa mambo mengi inashangaza kuona kuwa nchi hii ambayo imetajwa kwa kila namna mbaya na nchi za magharibi iko mbele kimaendeleo kuliko Tanzania nchi yenye idadi mara mbili ya watu wa Korea Kaskazini, demokrasia ya vyama vingi, mahusiano mazuri na mataifa ya magharibi n.k

  Hata Cuba, Vietnam, China, Venezuela, Uhispania nchi zenye mrengo wa kisoshalisti zinapiga maendeleo mbele kuliko nchi ya kibepari kama ya kwetu. Tatizo ni nini hasa? NI mfumo wa kisiasa, ni mwelekeo wa uongozi, au kitu gani hasa?

  Lakini hasa ni North Korea inawezekanaje kataifa kama North Korea kuwawekea ngumu Obama na washirika wake na kuendelea kufanya utafiti wa mambo ya kiteknolojia bila ya kuabudu au kufuata kitabu cha maelekezo kutoka Ulaya na Marekani?

  Je na sisi tuwawekee ngumu kina Obama, Brown na wenzake na tuone kama tunaweza kupita hatua za maendeleo mbele? Je kwa kuamua kufanya mambo bila kuwatilia maanani wakubwa hawa yawezekana tukachochea ubununifu wetu wenyewe?

  Fikiria kwa nchi kama Tanzania inayopokea misaada mingi, ina marafiki wengi bla bla bla GDP (nominal) = 16.691 Billions USD na Per Capita income ya 428USD. Population yake karibu milioni 40 Literacy level ya tanzan ni 69.4 wakati makadirio ya uhai ni miaka 50 kwa wanaume na 53 kwa wanawake.

  North Korea kwa upande wake, pamoja na matatizo yake na kutengwa na jumuiya ya kimataifa GDP yake ni 26.2 Billions USD; Per capita ni 1800USD; population yake ni watu milioni 23 hivi na life expectancy ni miaka 69 kwa wanaume na 75 kwa wanawake. Literacy level ni asilimia 99!! (Hata Marekani haijafika hapo!)

  So, why this picture don't make any sense!? Yawezekana uongozi wa kidikteta una manufaa kwa watu wengi zaidi kuliko uongozi wa kina mjomba?
   
 2. B

  Bontowar JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 524
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Tatizo letu Mfumo mbaya wa maendeleo unao ongozwa na wakubwa wa nchi
  sisi kama TZ hatuna haja yakuwa kama ombaomba tuna kila kitu tatizo mikono ya watu.

  Tuangalie nchi kama suda mpaka inafikia kufukuza watoa msaada ni kwamba haiogopi yeyote. TZ haki hakuna - wizi umekithiri- rushwa. kila kiongozi wa juu wanatajirika wakiwa madarakani kwanza wanajivunia wenyewe,hata Uganda na Kenya wanatushinda.
   
 3. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145

  Kulinganisha utawa wa kiimla wa Korea ya Kaskazini na Tanzania ni sawa na kufananisha mbingu na ardhi.

  Mosi, Korea kaskazini imefika hapo ilipo kutokana na vita baridi kati ya kundi la 'warsaw' na lile la NATO.

  Pili, Urusi na Uchina waliwekeza sana katika utawala huu hasa katika nyanja ya teknolojia ya ulinzi na usalama na kupuuza masuala muhimu ya usalama.

  Tatu, kuendeleza sehemu hiyo ya pili hapo juu, korean peninsular ni eneo lililokuwa maalum kwa usalama wa USSR na PRC kwa hiyo walimwaga kila aina ya msaada kulinda eneo hilo lisitwaliwe na USA.

  Nne, wananchi wake wanakufanya njaa kwani serikali yenyewe imekalia kulimbikiza silaha na kufanya mauzo ya silaha kwenye 'lack makert'

  Takwimu zinaonyesha ya kwamba pamoja na kuwa na teknolojia ya kisasa na kutambia mataifa makubwa lakini ukiondoa pazia utaona ya kwamba ni mrusi na mchina ndiyo wako nyuma ya move zote za Korea Kaskani. PRC wanauwezo wa kuruhusu mapinduzi na mabadiliko ya China.

  Mwisho, Kim Jong Il anawatesa wananchi wake kwa njaa na wananchi wake wanaishi katika karne ya 18 kimaisha.

  Hitimisho: Dikteta ni dikteta hata ukimpaka rangi za namna gani bado atabaki kuwa dikteta na hawana nafasi katika ulimwengu huru wa kidemokrasia. Unategemea Tanzania itaendelea ukiacha siasa mbovu , sera zisizo na manufaa kwa mwananchi wa kawaida na sasa UTAWALA ULIOPO MADARAKANI NI SAWA NA TIMU YA MPIRA WA MIGUU YA CHEKECHEA AMBAYO UFANYA KAZI YA KUKIMBIZA MPIRA KILA KONA YA UWANJA BADALA YA KUWA PROFESSIONAL KWENYE HIYO KANDANDA YA KISIASA.

  mwisho kabisa unategemea nini kama uchumi wa Tanzania asilimia 98 huko mikononi mwa sekta isiyo rasmi[DE SOTO 2005]? kisa: mifumo mibovu na uongozi usio na 'road map' au ukiwa na road mapo haujui kuweka vipaumbele.

  Mungu Ibariki Tanzania
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Data za nchi kama North Korea saa ingine ni fabricated!

  Ikumbikwe a rosy picture should not be potrayed as kuna njaa kali na wananchi wengi kufa kwa njaa na baridi ya ajabu!
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Apr 6, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,417
  Trophy Points: 280
  Heheheheheee...mtakuna vichwa weeeee...mtajiuliza weeeee...mwisho wa siku ukweli utabaki palepale tu!
   
 6. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #6
  Apr 6, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180

  Mwjj:

  Misaada tu inatuua. Tukiacha kuombaomba nina imani tutafanikiwa.
   
 7. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #7
  Apr 6, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Asante Mwanakijiji,
  Hatuhitaji kutengwa na wala kutokutengwa ili tuweze kuendelea. Sisi Tanzania tunakosa kitu kimoja tu, viongozi wetu hawatujui kwanini Tanzania ni masikini, japokuwa baadhi ya Watanzania wanajua kwanini bado hii nchi masikini SANA. Viongozi wetu wao sio masikini, ila watanzania wengi mno (>90%) ni masikini wa kutupa, nadhani hii ndio sababu hawajui kwanini bado Tanzania ni masikini.

  Kwa hakika Tanzania tulichokikosa ni uongozi bora tu, uongozi unaotawala kwa mujibu wa sheria, uongozi usiokuwa na viwango viwili vya sheria, utendaji na utoaji wa haki. HAKI YA CHENGE SIO SAWA NA HAKI YA KUBENEA hapa Tanzania!. Wenzetu kama nchina ambao ni mfano mzuri ulioutaja, hakuna mchezo kabisa linapokuja suala la masilahi ya umma. Wote wanaotuhumiwa na kupatikana na hati za rushwa, ufisadi, waliouwa mashirika ya umma, walioingiza vyakula vibovu nchini wangekuwa tayari kesi zao zishamalika siku nyingi na wengi wao kunyonwa tayari. Kumbuka ni juzi tu waliohusika na maziwa ya watoto yenye sumu walihukumiwa kunyongwa nao hawakawizi, sisi bado tunaendelea kulumbana na EPA n.k! Hapa Tanzania ukiharibu TTCL unapelekwa NSSF, ukizamisha BOT unapelekwa Tanesco, bandari, nasaco n.k, sasa tuendelee je wakati hao wahusika tayari wanakuwa wameshaeendelea kwa niaba ya taifa!

  Tunahitaji mwendawazimu Tanzania, lakini sio kupokezana kijiti kama Kikwete alivyopokea kutoka kwa Mkapa, kwani anapokea pamoja na mikoba yake!

  Viongozi wetu wanafurahia Tanzania kama ilivyo kwa DRC kuendelea tu kuwa sehemu ya kujipatia malighafi kwa mambwana wet wa amerikana na china!
   
 8. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #8
  Apr 6, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ikumbukwe kuwa wakati Korea ilipogawanyika sehemu ya kaskazini (Korea Kaskazini ndio ilikuwa imeendelea kiviwanda kuliko korea kusini. Hivyo basi uwezo walikuwa nao tayari wa kuendeleza hiyo technologia ya kiviwanda. Lakini kutokana na kutengwa, technologia yao haikuweza kukua kwa haraka kama wenzao wa kusini ambao walipata msaada mkubwa kutoka nchi za ulaya ya magharibi na Marekani. Ukirejea Tanzania, hali ya maendeleo ya kiviwanda tulikuwa tupo chini kabisa. Hatukuwa na watanzania wakutosha waliobobea katika technologia za kiviwanda hivyo ikawa kama ndio tumeanza from the scratch. Kwa hiyo wakati sisi tunaangaika kujenga miundombinu ya viviwanda na kutrain manpower wenzetu walikuwa wanaboresha na kuongezea vipya. Pia tabaka la wafanyakazi wenye nidhamu ya hali ya juu na moyo wa kufanya kazi liliwasaidia korea kaskaz kusonga mbele wakati Tanzania wafanyakazi wetu wakati wote walikuwa wanafikiria motisha kwanza halafu ndio wafanye kazi. Na pale motisha haikupatikana, hujuma mahali pa kazi kuanzi kwa wa kurugenzi maka wafanya kazi wa kawaida zilikuwa kubwa na kusababisha uzalishaji kupungua.

  Pia ushindani wa kimaendeleo kati ya Korea mbili, Kaskazi na kusini. Zote zilikuwa zinajitahidi kuhakikisha zinaboresha maisha ya wananchi wake ili wauone mfumo wa utawala wa sehemu fulani ndio unafaa. Bahati mbaya Korea kaskazini toka kuparaganyinga kwa nchi za kikomnist, ikajikuta imebaki peke yake na misaada ya kigeni kupungua. Tanzania hatukuwa tunashindana na nchi yoyote, sanasana tuliamua kusubirisha maendeleo yetu ili tukomboe nchi nyingine zilizokuwa chini ya ukoloni

  Kingine ni hali ya hewa. Korea hali ya hewa ni very harsh. Mazingira yao yanawafanya wajitume kutatua kero za maisha lasivyo wanaweza kupoteza maisha. mfano, kutokana na kuwa katika eneo ambalo lina baridi kali, nishati ya umeme ni kitu cha muhimu sana kwa ajili ya kupasha joto majengo ili watu wasije wakafreeze. Pia kwa kuzalisha nishati ya kutosha, imesaidia kuendesha shughuli zingine za maendeleo bila matatizo ama viwanda. Ukija Tanzania, nishati ya umeme sio jambo la muhimu sana kwa sababu hakuna mtu atakaye kufa kwa kukosa umeme, nyumba haziitaji kupashwa joto nk. Hivyo uwekezaji katika chi yetu haujaweza kuweka kipaumbele kuhakikisha kuwa kila mtanzania ana access umeme wa gharama nafuu na wakutosha kuendeshea shughuli zao za kila siku. Na hii imesababisha kutumaa kwa shughuli za maendeleo kwa kua nishart ya kutosha, ya bei nafuu na ya uhakika hakuna.

  Jingine ni Ufisadi (uhujumu uchumi) hili watu wamelizungumzia sana na litanifanya liangushe machozi bure kwa kulielezea. Naishia hapa

  Nawaachia wa JF wengine waendelee kuunga tela
   
 9. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #9
  Apr 6, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,122
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Korea ya kaskazini iko kwenye hali mbaya sana, oil asilimia 80% wanapewa na china chakula nacho asilimia nyingi ni misaada, so sidhani kama ni mfano mzuri.
   
 10. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #10
  Apr 6, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Imepelekwa kwenye hali mbaya kwa sababu ya dunia fedhuli (ikiongozwa na......) inayotaka kulambwa miguu yao ndipo wakukubali kuwa wewe ni mtoto mtiifu.
  Other wise they are better off. si umesikia kuwa wametengeneza satellite wanataka kuituma anga za juu pamoja na matatizo yao yote?
   
 11. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #11
  Apr 6, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,122
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Wameituma jana, imeanguka baharini nadhani.
  Ninachosema ni kuwa wanatumia resources zao vibaya, hakuna haja ya kurusha satelite/nuclear weapon kama chakula hamjaweka freshi bado.
   
 12. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #12
  Apr 6, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  badala ya kungangania kusoma looong articles za JJ MNYIKA na wenzie siku zingine soma vitabu kama hivi then njoo tujadili Economics

  [​IMG]


  ukienda to your local Barnes and Noble au hata ukiagiza Amazon utakipata hiki kitabu
   
 13. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Tanzania tunahitaji elimu ya siasa kwa sisi wananchi wapiga kura, mpaka siku tutakapoelimika na kuweza kuona ukweli, tutaendelea kujichagua wenyewe tu na kulalamika as if tuliowachagua wametoka Mars, kumbe ni sisi wenyewe kwa wenyewe tunaofanyiana uhuni. Korea na sisi ni sawa sawa tu ila tofauti tu ni kwamba wao wanatengwa na dunia sisi hapana, tunaweza kuomba omba wao hawawezi.

  Respect.

  FMES!
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Apr 6, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Korea Tambarare?

  [​IMG]
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Apr 6, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Jamani.. kama tunapima hali yao mbaya kwa sababu ya wananchi wao kukosa chakula au kutumia resources vibaya.. wana tofauti gani na Tanzania? MBona sisi pamoja na urafiki wetu na magharibi hatujaweza kujitosheleza kwa chakula wala umeme? Hatujaweza hata kurusha kibatari angani!? Kwamba, tunapinga propaganda za DPRK wakati zile za magharibi ndizo tunazikubali?

  DPRK wameweza kufanya mengi, mfumo wao wenyewe wa uchumi, siasa zao za Juche n.k labda tunachokosa sisi ni kiongozi mwenye nguvu na hisia za kidikteta hivi maana kama Udikteta unaweza kujenga na kwenda mbali katika teknolojia, miundombinu n.k basi utawala wa demokrasia una matatizo!
   
 16. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #16
  Apr 6, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wasijihami kwa sababu gani wakati Marekani na Korea Kusini wameweka majeshi yao tayari kwa ajili ya kuishambulia? Hata kama imeangukia baharini, wanaelekea kuzuri. Kwani mara ngapi marekani vyombo vyao vimeshindwa kupaa na kulipuka?
   
 17. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #17
  Apr 6, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Our so called leaders have no vision for the country. That's the main reason. Their main vision is themselves and their big tummies.
   
 18. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #18
  Apr 6, 2009
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  they have a nuclear bomb... thts how u get the white pigs to listen to u.. Angekuwa hana wangemchapa...lol Saddam kaleta ubishi akapewa kubwa.... Mugabe kaleta ubishi kapewa kubwa (china na russia wangekuwa wana interest yamaana kule asingemalizwa akaisha kabisa mzee Bob)...
   
 19. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #19
  Apr 6, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,122
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Wako tayari kuwashambulia kwa sababu North na South Korea bado vipo kwenye vita hadi leo. South Korea wala Marekani hawezi kuvamia North Korea unless alete ukorofi kwanza. Ni waste of resources kurusha Rockets wakati chakula hakuna, wamarekani sidhani kama wana shida ya chakula.

  Ninachosema mimi ni kuwa North Korea sio mfano wa kuigwa na wala sio mfano mzuri kwa Tanzania, tutapelekana pabaya sana.
  Kama tunataka kuiga kwanini tusiige South Korea, Japan etc?
   
 20. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #20
  Apr 6, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu angalieni picha ya Uwanja wa ndege wa Dar es salaam na wa Pyongyang. Nimetumia scale (ukubwa) karibu sawa na ndipo mlingalishe ulipo sisi na walipo wao
   

  Attached Files:

Loading...