Korea ya Kaskazini kuandaa silaha za kuifuta USA duniani

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,839
17,437
Gazeti rasmi la Korea Kaskazini la Minchu Chosun limeandika kuwa, hivi sasa Pyongyang inaendelea na maandalizi ya kuunda silaha yenye uwezo wa kuifuta kabisa Marekani kwenye uso wa dunia kutokana na Washington kuendelea kujizatiti katika eneo la Peninsula ya Korea.

Taarifa ya gazeti hilo imewanukuu makamanda wa kijeshi wa nchi hiyo wakisema kuwa, hivi sasa Marekani inajiandaa kufanya shambulizi dhidi ya Korea Kaskazini kupitia utumaji wa meli yenye uwezo wa kubeba ndege za kivita ya USS Nimitz katika pwani ya Korea.

Limeongeza kuwa, hatua hiyo ya Washington, inaifanya idadi ya meli kubwa za kijeshi za nchi hiyo zilizotia nanga katika pwani hiyo ya Korea kufikia tatu ikiwemo ya USS Ronald Reagan na USS Carl, suala ambalo linaifanya Pyongyang nayo ijiandae kukabiliana na hatari yoyote tarajiwa.

Wakati huo huo, nyambizi ya Marekani yenye kubeba silaha za nyuklia pia imetia naga katika pwani ya Korea baada ya kumaliza kushiriki maneva ya kijeshi na Japan. Gazeti rasmi la nchi hiyo la Minchu Chosun limebainisha kwamba, Pyongyang inaendelea kulifanyia marekebisho kombora lenye uwezo wa kuisambaratisha Marekani iwapo Washington itajaribu kutekeleza hujuma yoyote dhidi yake.

Weledi wa masuala ya kijeshi eneo la Peninsula ya Korea wanaamini kuwa, maandalizi ya Marekani katika eneo hilo yanabainisha kwamba Washington imepanga kufanya mashambulizi dhidi ya Pyongyang. Hayo yanajiri katika hali ambayo Marekani imeiwekea Pyongyang vikwazo zaidi kwa sababu ya miradi yake ya nyuklia na makombora ya balestiki.

Parstoday.sw
 
KOREA BANA WANASHANGAZA SANA TECHNOLOGY WANAYOPATA WAO WENZAO WALIKUWA NAYO MIAKA YA SABINI.ACHA WAPIGWE TU MAANA WANAONGEA SANA.
Huwa nawashangaa sana watu wanaobabaika na Korea ya Kaskazini. Watu wanajidanganya kusema eti Marekani inamuogopa Mkorea lakini ukweli ni kwamba North Korea Hana uwezo wa hata robo wa kupigana na Marekani. Wanachojivunia ni uwezo wao wa kuipiga Korea ya Kusini na Japan ambazo zimeendelea sana kiuchumi lakini hazijishughulishi na umiliki wa silaha za hatari. Mnajua historia ya Japan ni sawa na Ujerumani ambazo ziliwekewa vikwazo via kutomiliki silaha za maangamizi baada ya nchi hizo kuichachafya dunia mwaka 1939 - 1945 kwa namna ambazo haijawahi kutokea tena duniani.
Kwa hiyo ni hofu dhidi ya madhara yanayoweza kuwapata washirika wa Marekani na si vinginevyo. Kumbuka tambo za Cuba, Libya na Iraq mtaelewa kuwa Vinchi vidogo vinavyotawaliwa na madikteta vina tabia gani. Kama Russia na China wako nyuma kwa Marekani, sembuse North Korea ambayo kwa Mashariki ya Mbali ndiyo nchi masikini ambayo watu wake wanakufa eti kwa njaa kama huku kwetu Bongoland.
 
Huwa nawashangaa sana watu wanaobabaika na Korea ya Kaskazini. Watu wanajidanganya kusema eti Marekani inamuogopa Mkorea lakini ukweli ni kwamba North Korea Hana uwezo wa hata robo wa kupigana na Marekani. Wanachojivunia ni uwezo wao wa kuipiga Korea ya Kusini na Japan ambazo zimeendelea sana kiuchumi lakini hazijishughulishi na umiliki wa silaha za hatari. Mnajua historia ya Japan ni sawa na Ujerumani ambazo ziliwekewa vikwazo via kutomiliki silaha za maangamizi badala ya nchiizo kuichachafya dunia mwaka 1939 - 1945 kwa namna ambazo haijaahi kutokea tena duniani.
Kwa hiyo hour iko kwa mad hata yanayoweza kuwapata washirika wa Marekani na si vinginevyo. Kumbuka tambo za Cuba, Libya na Iraq mtaelewa kuwa Vinchi vidogo vinavyotawaliwa na madikteta vina tabia gain. Kama Russia na China wako nyuma kwa Marekani, sembuse North Korea ambayo kwa Mashariki ya Mbali ndiyo nchi masikini ambayo watu wake wanakufa eti kwa njaa kama huku kwetu Bongoland.

Ur right man.Keep.reading uzidi kupata madini adimu
 
Korea kaskikazini hata kama wanafanya utani na marekani lakini huo utani umepitiliza.

Watu wanasema usije ukacheza na simba ukamtia mkono kinywani.
 
Npo huku north korea U.S.A atapgwa saa 4 asbhi hawawez jamaa
Acha kabisa kukidanganya kichwa chako. N. Korae hana uwezo wa kiteknologia au kiuchumi wa kupigana na marekani hata kwa muda wa robo mwaka. Tena kama kweli upo huko mshauri bonge nyanya asije akajaribu kujitutumua ata-perish abaki kwenye vitabu vya historia.
 
KOREA BANA WANASHANGAZA SANA TECHNOLOGY WANAYOPATA WAO WENZAO WALIKUWA NAYO MIAKA YA SABINI.ACHA WAPIGWE TU MAANA WANAONGEA SANA.
hapo mgomvi sio mkorea ila marekani wanamuogopa na kutaka kumzuia huyo mkorea aache kutengeza nyuklia maana marekani wanataka wao ndio wawe juu siku zote wacha mkorea aonyeshe uwezo
 
Acha kabisa kukidanganya kichwa chako. N. Korae hana uwezo wa kiteknologia au kiuchumi wa kupigana na marekani hata kwa muda wa robo mwaka. Tena kama kweli upo huko mshauri bonge nyanya asije akajaribu kujitutumua ata-perish abaki kwenye vitabu vya historia.
Kama waarabu tu anaowaoneage mf syria, ni mwaka watano huu bado hawajafanikiwa kumtoa /kumuua bashar, sembuse north korea!. USA kwa sasa hadhi ya ufupa pawa interm of millurary umepungua sana. 김 종 은 /Kim jong un/ alishasemaga kuwa yeye si mwarabu.
 
KOREA BANA WANASHANGAZA SANA TECHNOLOGY WANAYOPATA WAO WENZAO WALIKUWA NAYO MIAKA YA SABINI.ACHA WAPIGWE TU MAANA WANAONGEA SANA.
Kama ni kweli kwa unayosasema, usa wasingefanya majalibio ya kujalibu kudugua makombola ya NK kwa destroyer zao ambazo zina uwezo wa kutungua makombola yao wenyewe. Wao wanasema kuwa NK hana kombola la kufika mainland ya marekani, destroyer za nini?
 
Acha kabisa kukidanganya kichwa chako. N. Korae hana uwezo wa kiteknologia au kiuchumi wa kupigana na marekani hata kwa muda wa robo mwaka. Tena kama kweli upo huko mshauri bonge nyanya asije akajaribu kujitutumua ata-perish abaki kwenye vitabu vya historia.
Subir sisi huwa hatuimbi taarabu kma Trump
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom