Korea Kusini na Kaskazini ilikuwaje wakatengana

komunisti

JF-Expert Member
Jan 5, 2015
1,047
1,379
Habari wakuu,nasikia korea kusini na kaskazini ilikuwa taifa moja yaani korea.Sasa sababu gani ilsababisha taifa hili la korea kumeguka na kuzaliwa Korea mbili?mwenye data tafadhali
 
Waligawanyika kwa mifumo ya kiujamaa na kibepari, kaskazini wakipewa sapoti na china na urusi na kusini wakisapotiwa na marekani na umoja wa mataifa, yakagawanywa kua mataifa mawili,.... Google Korean War au tafuta movie inaitwa Operation Chromite ya Liam Neeson
 
Nitaeleza historia ya korea kwa ufupi mpaka ikaja kuanguka.

Baada ya utawala wa Joseon baadae wakaita Korean Empire kuanguka nchi iliungwa(annexed) na kuwa sehemu ya japan hivyo ufalme wa korea ulianguka rasmi mwaka 1910 na kuwa koloni la japan.

Kuiibuka kwa vita ya pili ya dunia kukapelekea nchi ya Japan kushuhudia kipigo kitakatifu, USSR (urusi) ilitangaza vita na Japan wakitokea Manchuria eneo ambalo Japan waliliteka kwa kuipiga urusi vita ya 1905, hivyo aliyekuwa mwakilishi wa Japan kwa upande wa korea kaskazini aliamua ku-withdraw,

Urusi ikaingia ardhi ya korea upande wa kaskazini wakielekea upande wa kusini, kutokana na USA kuhofia kuenea kwa siasa za ukomunisti na wao wakavamia korea upande wa kusini na wakaja wakaseti mpaka ambao kila nchi haukupswa kuvuka.

Mpaka huu uliigawa nchi katika pande mbili yaani kusini na kaskazini, mwanzoni nchi zote zilizani ya kuwa mpaka huo utakuwa ni wa muda tu pindi mambo yatakaporekebishwa, lakini hali haikuwa hivyo kwani kila mmoja USA na USSR walitaka kutawala nchi kwa itikadi wanazotaka wao yaani ubepari au ukomunist kitu ambacho kilishindikana.
 
Mkuu ungeanza kuelezea kuanzia enzi za wafalme eg. Jumong, Gwan gaeto, yuri, Gunchogo etc..
Pia uelezee kuzaliwa kwa jumong hadi kuipata guguryeo
 
Huu ulimwengu wa kidigitali hauna msaada kabisa enhee? Maana hivyo vitu viko wazi sana na resources zipo kibao kwa google na youtube! Tujifunze kuwa independent kidogo....
 
Waligawanyika kwa mifumo ya kiujamaa na kibepari, kaskazini wakipewa sapoti na china na urusi na kusini wakisapotiwa na marekani na umoja wa mataifa, yakagawanywa kua mataifa mawili,.... Google Korean War au tafuta movie inaitwa Operation Chromite ya Liam Neeson
Asante sana kaka
 
Huu ulimwengu wa kidigitali hauna msaada kabisa enhee? Maana hivyo vitu viko wazi sana na resources zipo kibao kwa google na youtube! Tujifunze kuwa independent kidogo....
Tatizo kidhungu kk..wengine tulikwepa umande
 
Chimbuko la kuto elewana linatokea huko ni kama Israel na Palestina
Nimesoma kitabu cha SAMGUK YUSA na vitabu vingi vinavyoelezea historia ya korea sijaona correlation ya hiko unachodai, na ukumbuke tu ya kwamba waliounganisha korea ilikuwa ni dola ya later silla kabla ya hapo kulikuwa kuna na dolla nyingi zilizopo hayo maeneo, na dola ambayo iliunganisha kabisa kitaifa ilikuwa ni Koryo chini ya ukoo wa wang ambapo makao makuu yalikuwa pongyang ambapo baadae utawala wa familia ya Yi waliamishia mji na kuwa Hanyang(sasa ni soul), sasa hayo madai yako sijui umeyatoa wapi napenda facts kuliko speculation za kiimani.
 
Habari wakuu,nasikia korea kusini na kaskazini ilikuwa taifa moja yaani korea.Sasa sababu gani ilsababisha taifa hili la korea kumeguka na kuzaliwa Korea mbili?mwenye data tafadhali
Kipindi cha cold war kati ya USA na USSR, walikua wanachukua nchi mbalimbali kua upande wao. Ikatokea USA ikaichukua Southern part ya Korea na USSR ikaichukua Nothern part ya Korea.
Uadui wa socialists na capitalists ikapelekea nchi hiyo kujigawa.
 
Asante sana kwa ufafanuzi
 
Back
Top Bottom