Korea Kusini na Kaskazini ilikuwaje wakatengana

hemedans

Member
May 18, 2011
63
125
Kuna historia imefichwa kwa atakaetaka source nitampa zipo chache.

1.japan sio nchi ilioathirika zaidi na nyuklia ya marekani bali korea ndio iliathirika zaidi takriban watu milioni 8 waliuliwa na nyuklia hii ambayo ni kama theluthi ya nchi nzima na ardhi iliobakia asilimia 75% ikawa hailimiki. Kwa historia ya dunia iraq, afghanistan, vita ya vietnam zote hizi hazijauwa kama wananchi wa korea walivyouliwa.

2. Baada ya kuuliwa huko kuna watu wengi wakataka kuingia ujamaa lakini marekani akawa hakubaliani na hii mambo hivyo akaua wakorea wengi sana, kuna mauaji ya halaiki watu malaki waliuliwa, kama unadhani mauaji ya ubaguzi wa rangi ya south africa yalikuwa makubwa unahitaji kuangalia mauaji ya halaiki ya korea.

Mateso yote hayo ya nyukilia, ardhi isolimika, njaa, magonjwa nk ndio yalianzisha korea kaskazini, ambayo ni population ya korea iliojitenga na utawala wa kimabavu wa marekani, wakajiunga na china na urusi kutengeneza mataifa ya kijamaa.

South korea wao wakaendelea na marekani wakaukubali ubepari.

Hadi leo marekani analeta propaganda za kila namna ili ionekane korea ni nchi mbaya, na propaganda hizo 99% ni vitu vya uongo,

Nawasilisha, maswali zaidi uliza usiogope
 
Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
6,106
2,000
Mimi nachoelewa ni kwamba korea kusini na kaskazini ni matokeo ya vita kuu ya pili ya dunia. Kama ilivyokuwa kwa Ujerumani Magharibi na Mashariki. Kwa kifupi hizi korea zimeanza ku exist 1945 baada ya vita kuisha. Hapo mwanzo ilikuwa korea moja. Korea kaskazini ilibaki kuwa chini ya urusi na kusini wao wakabaki kuwa upande wa marekani.

Kwa ujerumani mashariki wao walibaki kuwa upande wa urusi (communist) na magharibi wao wakabaki upande wa marekani (mabepari)

Ww2 ilikuwa na faida zake
1. Kuanzishwa kwa umoja wa mataifa.
2. Kuanzishwa kwa nchi ya israel
3. Kuwepobkwa korea mbili na Germany mbili.

Hasara.

Vifo na uwaribifu wa mali na miundo mbinu.
 
medieval2april2021

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
249
500
Ifahamike ya kuwa hapo awali Rasi ya Korea ilikua chini ya Mamlaka moja, Nitaegemea zaidi kwenye Mgawanyo wa Korea.

Kuanzia miaka ya 1890 Korea (yote) Ilikua ikiitwa Korea Empire ilikua huru na ilijiendeshea mambo yake yenyewe, Mwaka 1905 Japan iliingia Mkataba na Korea Empire na wakaifanya kuwa 'Protectorate' kwa maana Korea Empire ilikua ikishughulika na mambo yake ya ndano tu huku masuala yote ya nje ikiwemo Ulinzi wake yalisimamiwa na Japan. Hapa ndipo Balaa kweli lilianza.

Miaka mitano baadae yaani 1910 Majeshi yenye nguvu ya Japan yakaisambaratisha rasmi Mamlaka za Korea Empire na hivyo kuitwaa rasi ya Korea kwa kuifanya kuwa Koloni lake.

Toka hapo Japan iliitawala Korea kama koloni lake huku ilifanyia Udhalimu wote ambao wakoloni walifanya Duniani kote, Wakorea walidhalilishwa, wakatengwa na wengine walilazimishwa kubadili majina yao na kubatizwa yale ya Kijapan, hili lilitamalaki zaidi kufikia 87% ya Wakorea waliyaacha Majina yao na kuchukua yale ya Kijapan.

Vita ya pili ya Dunia Ikazuka huko Ulaya, Ujerumani alikiwasha akawatetemesha wazungu wote akaungwa mkono na Musolini wa Italia na baadae na Japan.

Vita ya pili ya Dunia kwa upande wa Asia ilipiganwa kwa kuongozwa na Japan kama washirika wa Ujerumani na Italia huku U.S.S.R (urusi) alipigana kama Mshirika wa Uingereza na Marekani.

WaMarekani na U.S.S.R wakagawana Majukumu, U.S.S.R alikabidhiwa kumpiga Mjapan kutokea Kaskazini kushuka Rasi ya Korea mpaka Manchuria (hii ilikua ni kwa sababu U.S.S.R ilipakana na Rasi ya Korea)
Huku Marekani aliwajibika kumtandika Japan kutokea Kusini mwa Rasi ya Korea huku akikata 'Supply Chain' ya Japan kutokea Tokyo.

Walifanikiwa kumuweka Japan 'Ambakati' Walimfurusha mwishowe wakakutana kati katika eneo ambalo baadae waliliita 38th parallel.
Mwaka 1943 Maafisa wa Marekani wakapendekeza U.S.S.R kuunda Mfumo wa Utawala wa Kijeshi katika maeneo yote 'waliyoyakomboa' na Marekani wakifanya vivyo hivyo.

Eneo waliloliita 38th Parallel wakalifanya kuwa mpaka wa muda baina ya majeshi hayo.
Vita iliendelea mpaka Japan aliposalimu amri Katika ardhi yake ya nyumbani na hatimae ikatamatika mwaka 1945.

Katika Rasi ya Korea viliundwa 'vikundi' lakini vilikua na tofauti kwa maana kaskazini vilikua na Itikadi ya Kisoshalisti/Kijamaa huku Kusini vilikua na Itikadi ya Kibepari/Kiliberali.

Mwaka 1947/48 Marekani walipendekeza UN kuitishwa kwa uchaguzi ambao ungesimamiwa na kamati iliyoundwa wawakilishi wa Kimataifa, hatua hii ingepelekea kuundwa kwa Serikali ya Korea yote, Lakini U.S.S.R wakiwa miongoni mwa Taifa lenye Turufu Waligomea pendekezo hilo.

Mwaka 1948 K.Kusini chini ya Usimamizi wa kamati ya muda ya UN iliitisha Uchaguzi, Walichagua Rais wao kisha wakatangaza kuwa Taifa Huru na baadae mwaka huohuo K.Kaskazini waliitisha Uchaguzi kivyao walichagua Rais wao kisha wakajitangazia Uhuru chini ya Kim Il sung.
Muda mchache baadae Kiongozi wa K.Kaskazini Kim Il Sung alipendekeza kwa wakuu wa chama cha Kikomunisti juu ya 'kuikomboa' K.Kusini, Waliafikiana na baadae akaomba uungwaji mkono toka U.S.S.R na Uchina ambao alihakikishiwa na akajijengea kujiamini.

Mwaka 1950 Vikosi kadhaa vilivyokuwa na Askari takribani Laki moja toka Kaskazini vilivuka eneo la 38th Parallel kuelekea kusini vikiwa na lengo la kuikamata Seoul, baada ya mashambulizi kadhaa wakafanikiwa kuitwaa Seoul (Mji mkuu wa K. kusini) lakini baadae walikutana na Upinzani toka kwa vikosi vya Kusini vilivyokuwa tayari huku vikipewa Uungwaji mkono na Marekani, UN na Canada. ambavyo kwa pamoja walivifurusha vikosi vya K.Kaskazini na Uchina mpaka kufika K. Kaskazini.

Tokea hapo Mapigano hayakuwa na Mshindi, Vuta nikuvute zilikua nyingi vikosi vya upande mmoja vilivuka mpaka upande wa pili lakini kesho yake vilirudishwa kwao.

Mapigano yalidumu mpaka mwaka 1953, Maafisa wa Marekani waliona hatari ya kuzuka mapambano mapya dhidi ya U.S.S.R na Uchina au hata vita ya tatu ya Dunia. Kimsingi hakukua na Mshindi wa Jumla kwa muda wa Kipindi chote cha Vita hakuna Upande uliofanikiwa kutwaa Maeneo ambayo yangeamua nani Mshindi katika Vita ile.

Mwaka 1953 wakafikia Makubaliano ya kusitisha Mapigano huku 38th parallel ikabaki kuwa mpaka na ili kuzuia kuzuka kwa mapigano mengine wakaunda Ukanda huru yaani 'Demilitarized Zone' au 'DMZ' ambao una ukubwa wa walau Kilomita mbili kaskazini toka 38th parallel ma kilomita mbili kusini toka 38th parallel.

Mwaka huohuo 38th Parallel ikabaki kuwa kama mpaka baina ya Pande hizi mbili huku watu takribani milioni tano walipoteza maisha katika pande zote mbili.

Toka viita iishe hali imebaki hivyo mpaka hii leo.
Ama kwa ziada juu ya Ukuu wa K.Kaskazini katika Nyuklia tembelea hapa.
 
Gaddy Fazzy

Member
Jan 16, 2021
54
125
Ifahamike ya kuwa hapo awali Rasi ya Korea ilikua chini ya Mamlaka moja, Nitaegemea zaidi kwenye Mgawanyo wa Korea.

Kuanzia miaka ya 1890 Korea (yote) Ilikua ikiitwa Korea Empire ilikua huru na ilijiendeshea mambo yake yenyewe, Mwaka 1905 Japan iliingia Mkataba na Korea Empire na wakaifanya kuwa 'Protectorate' kwa maana Korea Empire ilikua ikishughulika na mambo yake ya ndano tu huku masuala yote ya nje ikiwemo Ulinzi wake yalisimamiwa na Japan. Hapa ndipo Balaa kweli lilianza.

Miaka mitano baadae yaani 1910 Majeshi yenye nguvu ya Japan yakaisambaratisha rasmi Mamlaka za Korea Empire na hivyo kuitwaa rasi ya Korea kwa kuifanya kuwa Koloni lake.

Toka hapo Japan iliitawala Korea kama koloni lake huku ilifanyia Udhalimu wote ambao wakoloni walifanya Duniani kote, Wakorea walidhalilishwa, wakatengwa na wengine walilazimishwa kubadili majina yao na kubatizwa yale ya Kijapan, hili lilitamalaki zaidi kufikia 87% ya Wakorea waliyaacha Majina yao na kuchukua yale ya Kijapan.

Vita ya pili ya Dunia Ikazuka huko Ulaya, Ujerumani alikiwasha akawatetemesha wazungu wote akaungwa mkono na Musolini wa Italia na baadae na Japan.

Vita ya pili ya Dunia kwa upande wa Asia ilipiganwa kwa kuongozwa na Japan kama washirika wa Ujerumani na Italia huku U.S.S.R (urusi) alipigana kama Mshirika wa Uingereza na Marekani.

WaMarekani na U.S.S.R wakagawana Majukumu, U.S.S.R alikabidhiwa kumpiga Mjapan kutokea Kaskazini kushuka Rasi ya Korea mpaka Manchuria (hii ilikua ni kwa sababu U.S.S.R ilipakana na Rasi ya Korea)
Huku Marekani aliwajibika kumtandika Japan kutokea Kusini mwa Rasi ya Korea huku akikata 'Supply Chain' ya Japan kutokea Tokyo.

Walifanikiwa kumuweka Japan 'Ambakati' Walimfurusha mwishowe wakakutana kati, Mwaka 1943 Maafisa wa Marekani wakapendekeza U.S.S.R kuunda Mfumo wa Utawala wa Kijeshi katika maeneo yote 'waliyoyakomboa' na Marekani wakifanya vivyo hivyo.

Eneo waliloliita 38th Parallel wakalifanya kuwa mpaka wa muda baina ya majeshi hayo.
Vita iliendelea mpaka Japan aliposalimu amri Katika ardhi yake ya nyumbani na hatimae ikatamatika mwaka 1945.

Katika Rasi ya Korea viliundwa 'vikundi' lakini vilikua na tofauti kwa maana kaskazini vilikua na Itikadi ya Kisoshalisti/Kijamaa huku Kusini vilikua na Itikadi ya Kibepari/Kiliberali.

Mwaka 1948 K.Kusini iliitisha Uchaguzi (kama ilivyopendekezwa na UN) kisha wakatangaza kuwa Taifa Huru na baadae mwaka huohuo K.Kaskazini wakajitangazia Uhuru pia chini ya Kim Il sung.

Mapema miaka kadhaa baadae Kiongozi wa K.Kaskazini Kim Il Sung alipendekeza kwa wakuu wa chama cha Kikomunisti juu ya 'kuikomboa' K.Kusini, Waliafikiana na baadae akaomba uungwaji mkono toka U.S.S.R na Uchina ambao alihakikishiwa na akajijengea kujiamini.

Mwaka 1950 Vikosi kadhaa vya Askari takribani Laki moja toka Kaskazini vilivuka eneo la 38th Parallel kuelekea kusini vikiwa na lengo la kuikamata Seoul, baada ya mashambulizi kadhaa wakafanikiwa kuitwaa Seoul (Mji mkuu wa K. kusini) lakini baadae walikutana na Upinzani toka kwa vikosi vya Kusini vilivyokuwa tayari huku vikipewa Uungwaji mkono na Marekani, UN na Canada. ambavyo kwa pamoja walivifurusha vikosi vya K.Kaskazini na Uchina mpaka kufika K. Kaskazini.

Tokea hapo Mapigano hayakuwa na Mshindi, Vuta nikuvute zilikua nyingi vikosi vya upande mmoja vilivuka mpaka upande wa pili lakini kesho yake vilirudishwa kwao.

Mapigano yalidumu mpaka mwaka 1953, Maafisa wa Marekani waliona hatari ya kuzuka mapambano mapya dhidi ya U.S.S.R na Uchina au hata vita ya tatu ya Dunia. Kimsingi hakukua na Mshindi wa Jumla kwa muda wa Kipindi chote cha Vita hakuna Upande uliofanikiwa kutwaa Maeneo ambayo yangeamua nani Mshindi.
Kufikia Mwaka 1953 38th Parallel ikabaki kuwa kama mpaka baina ya Pande hizi mbili huku watu takribani milioni tano walipoteza maisha katika pande zote mbili.

Mwaka huohuo wakafikia Makubaliano ya kusitisha Mapigano huku 38th parallel ikabaki kuwa mpaka na ili kuzuia kuzuka kwa mapigano mengine wakaunda Ukanda huru yaani 'Demilitarized Zone' au 'DMZ' ambao una ukubwa wa walau Kilomita mbili kaskazini toka 38th parallel ma kilomita mbili kusini toka 38th parallel.

Toka viita iishe hali imebaki hivyo mpaka hii leo.
ama kwa ziada juu ya Ukuu wa K.Kaskazini katika Nyuklia tembelea hapa.
Nimekupata
 
ZAK ZAK

JF-Expert Member
Mar 2, 2018
220
250
Jibu la swali ni kwanini USA Walivamia kusini(south korea) na Urusi(china) kasikazini. Jibu itikadi ya kusini ilikuwa ubepari na kasikazini ujamaa na ukomonist. Goguryeo ilijengwa na jumong kutoka la Buyeo(uchina na korea). Ndio maana Tang dynastry alichukua teo goguryeo. Baikije mke jumong alikuwa mbinafsi(capitalist) akawapa watoto ufalme.
 
Intelligent Electronics

JF-Expert Member
Jan 19, 2020
620
1,000
Jibu la swali ni kwanini USA Walivamia kusini(south korea) na Urusi(china) kasikazini. Jibu itikadi ya kusini ilikuwa ubepari na kasikazini ujamaa na ukomonist. Goguryeo ilijengwa na jumong kutoka la Buyeo(uchina na korea). Ndio maana Tang dynastry alichukua teo goguryeo. Baikije mke jumong alikuwa mbinafsi(capitalist) akawapa watoto ufalme.
Sababu kuu ya Korea ya sasa kugawanyika ni Siasa za Marekani na Urusi.

Ila hoja yako ya kuangalia Historia yao pia ina mashiko, kwa sababu Tangu miaka na Miaka, wamekuwa na Dola za Kaskazini na Kusini
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom