Jambazi
JF-Expert Member
- Jan 18, 2014
- 16,644
- 18,707
Waziri wa maswala ya Ulinzi nchini Korea Kusini amesema
kuwa mpango wa utengenezaji wa makombora wa Korea
Kaskazini unaendelea kwa kasi zaidi ya ilivyo dhaniwa. Han Min-koo pia aliliambia bunge mjini Seoul kwamba jaribio la kombora lililofanywa na Pyongyang siku ya
Jumapili liligunduliwa na kifaa cha kutibua makombora cha THAAD nchini Korea Kusini. Ni mara ya kwanza kwa kifaa hicho kilichotengezwa na Marekani kutumika tangu kipelekwe Korea
Kusini mwezi uliopita. China imepinga kupelekwa kwa
chombo hicho ikidai kuwa kinaweza kutumika kuchunguza eneo lake. Mjini New York, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya mkutano wa faragha kuzungumzia kuhusu
kuimarisha vikwazo dhidi ya Korea
Kaskazini.
Source; bbc