Korea Kuleta Walimu wa Sayansi na Hisabati ili Kupunguza Uhaba wa Walimu Nchini

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
1.jpg


SerikaliI ya Korea imepanga kuleta nchini walimu wa masomo ya hisabati na sayansi kwa shule za sekondari, kusaidia kupunguza uhaba wa walimu wa masomo hayo.

Itatekeleza azma hiyo kupitia Mpango wake wa Kusambaza Walimu wa Kikorea katika nchi Zinazoendelea (KTDP).

Akizungumza jana alipotembelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais wa Taasisi ya Elimu ya Kimataifa (NIIED), Kim Kwangho, alisema nchi yake imekuwa ikisambaza walimu.

Alisema mpaka sasa wamesambaza walimu 61 katika nchi mbalimbali zinazoendelea; na mwaka huu watasambaza walimu 140 kwa nchi 15.

“Tumeona katika kuunga mkono juhudi za serikali kuongeza walimu wa masomo ya sayansi na kwa mara ya kwanza mwaka huu taasisi yetu itasambaza walimu 10 hapa Tanzania kati yao watano watahusika katika masomo ya hisabati na wengine watano watahusika na masomo ya Sayansi,” alisema Kwang-ho.

Aidha alisema licha ya kusambaza walimu hao, Serikali ya Korea inatoa ufadhili kwa wanafunzi wenye vipaji kimataifa ili kuendeleza masomo yao katika taasisi za elimu ya juu nchini kwao, lengo likiwa ni kusaidia kukuza viongozi wa baadae wenye elimu.

Kwang-ho alisema waombaji wa ufadhili huo ni wale waliosoma tu Shahada ya kwanza na shahada ya Uzamili nchini; na haitawahusu wale wote ambao wamewahi kusoma Korea.

Katika hatua nyingine, Kwang-ho alisema Korea ina mpango wa kufungua kituo cha kutoa kozi ya lugha ya Kikorea katika chuo kikuu hapa nchini, lengo likiwa ni kupanua wigo wa fursa kwa wanafunzi wa Kitanzania kujifunza lugha hiyo.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Masuala ya Mahusiano Kimataifa, Opportuna Kweka alisema tayari rais huyo ameshakutana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala na kujadili uwezekano wa kuanzisha kituo hicho.
 
ni jambo jema sana kuona taifa la mbali linaonyesha kuumia na mapungufu yetu ila ni vyema kufikiri Mara mbili au zaidi kujua haswa nia njema hii na nyingine za namna hii nyuma yake kuna jambo gani haswa lililojificha ambalo kiuhalisia lazima litakuwa na faida upande wao?.......Mtindo wa dunia hii ya kisasa ni ule wa nipe NIKUPE ......tutafaidika kiasi gani na wao wao watanufaika nini hapo ndipo penye fumbo
 
nadhani tunao kdg ila kikwazo ni uwingi wa walimu hao maeneo ya mijini
Hapo sawa mkuu ila mo naona Serikali ingefanya jitihada za kuboresha mazingira ikiwemo miundombinu, maslahi na motosha ili ivutie waalimu kwenda maeneo ya vijijini
 
Sasa nchi hii kubwa, wanaleta walimu watano wa hesabu kweli! Na sisi tumekuwa wa misaada sana hadi tunaboa. Hapa itaandaliwa dhifa ya kupokea walimu kumi.
Ni mara mia wangefadhili wasomeshwe walimu wengine hata hao watano ambao wataendelea kuwepo maana hao wageni huja na huondoka
 
Kuna engineers wengi hawana ajira wapelekwe wakafundishe hesabu sekondari
Hapa ndo ujue taaluma ya ualimu haijaliwi unahitaju akili ya ukubwa wa 0.01kusolve hili tatizo. Hao jamaa ukiwatupia teaching methodology ya miezi 3 ukawalipa 1.5 take home hawawezi shindwa kwwnda ushekeni kupiga hayo masomo. Uchoyo tu umewajaa baadhi ya watu na kutaka kuona tuna shida saa kitubambacho si sawa
 
Hii nchi bana unashindwa hata kujua inakwendaje. Hapo utambiwa serikali iwawezeshe kuishi(makazi,chakula,usafiri na huduma za afya) halafu uone hiyo gharama yake sasa.

Kuna vijana wengi sana wanasoma hisabati na sayansi ila tu hawaingii kwenye kada ya kufundisha. Nchi ilitakiwa itafute suluhisho la kudumu la hizi changamoto badala yake unasikia vitu kama hivi.
 
Huwezi kuona uhaba wa walimu wahisabati & sayansi kwa vile shule ilikupita Pembeni sio kosa lako kwakuwa uwezo wako wa kuona unaishia hapo
Mkuu hakuna uhaba wa walimu wa Sayansi na Hesabu nchini, kilichopo nchini ni mazingira mabovu ya kuwawezesha hao walimu kufanya kazi na motisha.......Watu wanakimbia kufundisha masomo hayo kwa sababu ya mazingira.

Hawa walimu wa masomo ya art walio wengi mbona perfomance bado ni mbovu kulinganisha na idadi ya walimu
 
Hapo sawa mkuu ila mo naona Serikali ingefanya jitihada za kuboresha mazingira ikiwemo miundombinu, maslahi na motosha ili ivutie waalimu kwenda maeneo ya vijijini

Umetumia akili na umefikiria zaidi kuliko wale wenye majibu ya kukurupuka. Kuna walimu wengi hawapo mashuleni na wengi zaidi walio competent wanahangaika kutafuta njia na fursa ya kutoka kwenye mashule wanako fundisha. Jukumu la muhimu la la maana zaidi ilikuwa ni kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia, mazingira ya kuishi na kufanya kazi kwa walimu, kuondoa kero zinazowakabili walimu pamoja na kubwa zaidi, kuboresha maslahi yao. Hapo kuna walimu wengi watarejea darasani na wale wanaofikiria kutoka watazidi kufundisha kwa bidii. Hii ni sawa na mkeo kuwa na tatizo na kushika mimba ukaenda kukodisha mwanaume mwingine aje amtie mimba, siyo suluhisho. Na kwa ujumla, halina tofauti na mtu kutegemea cha nduguye
 
hii imenisikitisha kwa kweli, nawajua wadau kibao wapo nondo kwenye physics na maths ila wapo mtaani, sasa wanawaleta wa Korea? hii ni aibu
 
Korea ipi? make ziko mbili,isije kuwa walimu kutoka kwa mzee wa makombora na vitisho bwana kim jong un(korea kas)
 
Back
Top Bottom