Korea kujenga uwezo wa watumishi Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Korea kujenga uwezo wa watumishi Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BabuK, Mar 27, 2012.

 1. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2012
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  UJUMBE wa Taasisi ya Mafunzo kwa Viongozi Serikalini na Watumishi wa Serikali za Mitaa (LOGODI) kutoka Korea, wapo nchini kushirikiana na Serikali kujenga uwezo wa watumishi hao.

  Ujumbe wa watu sita upo nchini kwa mwaliko wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ili kusaidia kujenga uwezo kwa watumishi na kukijengea uwezo Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo kilichopo mkoani Dodoma.

  Akizungumza wakati wa kupokea ugeni huo katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk. Mary Nagu alisema ugeni huu utasaidia kukuza elimu kwa watumishi wa Serikali za Mitaa.

  Dk. Nagu alisema ziara ya wataalamu hao ni mwendelezo wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili ikiwa ni sehemu ya misaada ya Korea kwa Tanzania katika utoaji elimu ambapo awali walitoa msaada wa ujenzi wa vyuo vitatu vya ufundi katika mikoa ya Pwani, Manyara na Lindi.

  Alisema Watanzania zaidi ya 4,000 kutoka mikoa minane wamenufaika na mafunzo ya aina mbalimbali nchini humo kwa ufadhiri wa Kampuni ya Korea ya KOICA.

  "Baada ya kutujengea uwezo katika kutoa mafunzo kwa watumishi wa Serikali, itasaidia katika utoaji huduma kwa watu kuanzia ngazi ya chini hivyo kupunguza umasikini miongozi mwa jamii," alisisitiza Dk. Nagu.

  Naye Rais wa Taasisi hiyo, Jeong-Sam Kim alisema ziara hiyo ni kwa ajili ya kubadilishana uzoefu ili kuleta maendeleo ya kiuchumi pamoja na kukuza uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

  Alisema taasisi hiyo kuanzia mwaka 1997, imetoa mafunzo ya watumishi 2,000 katika nchi 80 wakiwamo watumishi 66 kutoka nchini ambao ni wengi kuliko nchi yoyote iliyopeleka watumishi wake.

  Naye Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Aggrey Mwanri alisema kuimarisha kwa elimu hiyo kutasaidia kukujenga uwezo kwa madiwani na watendaji wa mitaa na kata na kujenga utendaji kazi wa Serikali za Mitaa.

  Wageni hao leo watatembelea Chuo cha Hombolo.

  Chanzo: HabariLeo

  Zuru kwa kuielewa Koica na kwamba Tanzania ni mdau na 1 kwa misaada ya Korea kwa Africa.
  http://www.koica.go.kr/english/aid/education/index.html
   
Loading...