Korea Kaskazini yatoa ujumbe usioelewaka! Korea Kusini yashikwa kiwewe

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,166
2,000
Maafisa wa Korea Kusini wameushutumu utawala wa Korea Kaskazini wakisema umefufua vita baridi.

Wanatoa mfano wa hivi majuzi ambapo, kulikuwa na matangazo kutoka redio Pyongyang ya Korea Kazkazini.

Redio hiyo ilipeperusha msururu wa namba zisizoeleweka vyema ambazo Korea Kusini wanasema huenda ni mbinu ya kuwasiliana na majasusi wao ambao huenda wanajificha nchini Korea Kusini.

Msemaji wa wizara ya maswala ya utangamano huko Korea Kusini anasema hiyo ni mbinu mojawapo iliyokuwa ikitumika wakati wa enzi za vita baridi kuwasiliana na majasusi ambao huweza kubaini nambari hizo za siri, na kufahamu ujumbe unatolewa.

Tangazo mojawapo kama hilo lilifanywa usiku wa manane na sauti ya mtangazaji wa kike akitoa nambari hizi - "ukurasa 459 namba 35, ukurasa 913, namba 55, na kadhalika... tena hata akaendelea kutoa maelezo na kusema "Nawapa Kazi Namba 27, ma-ajenti wa utafiti."

Korea Kaskazini yatishia kuishambulia Marekani
Korea Kaskazini yakata mawasiliano na Marekani
Korea kusini imeitaka Korea Kazkazini kukomesha mara moja uchokozi huo.
Maafisa wa kijasusi wa Korea Kusini wanajikuna vichwa kujaribu kubaini maana ya ujumbe huo unaotolewa kwa vitendawili.

Lakini wachanganuzi wanashangaa ni kwa nini Korea Kazkazini watumie mbinu hiyo ya kizamani ilhali siku hizi ziko mbinu nyingi za kuwasilisha ujumbe kwa urahisi kupitia mitandao ya intaneti.

Au ni mbinu nyengineyo ya kutoa vitisho tu kama vile Korea Kaskazini inavyofanya kupitia majaribio ya makombora ya kinyuklia.

Mwezi huu Korea Kusini na Marekani waliamua kupeleka mitambo ya hali ya juu ya kujilinda dhidi ya makombora katika maeneo hayo ya Korea jambo lililoudhi sana utawala wa Pyongyang.
Utawala wa Korea Kaskazini pia umewahi kueneza uvumi na propaganda ya kusema wanaweza kutumia ndege zisizoonekana kwenye mitambo ya rada kushambulia uwanja wa ndege wa Seoul.

Kama hilo linawezekana au la ni suala la mjadala lakini ni mambo kama hayo yanayouongezea wasiwasi utawala wa Korea Kusini .

Chanzo: BBC
 

Bukyanagandi

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
9,066
2,000
Na hao viongozi wa Korea kusini wanaleta usanii tu, kwani wana uhakika gani kwamba kutajwa namba kwenye redio na TV za Korea kaskazini kunashilia kuhamusha sleeper cells zilizopo Korea kusini ili zifanye hujuma! Uongo mtupu.
 

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,166
2,000
japo kahakikishiwa ulinzi na Marekani bado South Korea haamini kama yupo salama
 

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
50,048
2,000
Vita ya tatu ya dunia itaanzia kati ya nashariki ya kati au korea kusini na kaskazini.
 

minuz

JF-Expert Member
May 8, 2014
624
225
Jamani mimi sielewi kabisa hivi ugomvi wa north na south korea ni nini si ni kila mtu ana kwake
 

hamfcb

JF-Expert Member
Dec 22, 2015
588
1,000
japo kahakikishiwa ulinzi na Marekani bado South Korea haamini kama yupo salama

Marekan siyo jitu la kuliamini asilimia 100%! Korea kusini kinaweza kikanuka Marekani akasema atatuma ndege za kuogeza mafuta tu hapo korea kusini akala kichapo cha mbwa!

Hata bila ya msaada wa marekani korea kusini anauwezo wa kutoa kichapo kikali kwa korea kaskazini. Korea kusini wapo juu kijeshi kuliko korea kaskazini tena kwa umbali mrefu tu. Wana silaha za kisasa zaidi, bajeti wao ya jeshi ni kubwa zaidi. Ni kati ya nchi 10 zenye uchumi imara duniani. Hata bila marekani Ikitokea vita kati ya hizi nchi mbili sidhani kama korea kaskazini anaweza ku survive labda asaidiwe na china
 

Mbojoz

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
578
1,000
Yaani hawa jamaa huwa wananichekesha sana, N. Korea yeye ni mkwara mara ahamishe makombora mara hivi hawaeleweki,wanakuwa kama kitoto wakitaka kupigana mtu anaanza kukunja mikono ya t-shirt wakati haihusiani
 
  • Thanks
Reactions: MC7

Washawasha

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
14,449
2,000
Sleeper agents kazi mmeshapewa namba 27 ndio habari ya mujini,napenda sana michezo hatari ya kipelelezi.
Nalog off
 
  • Thanks
Reactions: MC7

JustDoItNow

JF-Expert Member
Dec 3, 2013
2,970
2,000
Na hao viongozi wa Korea kusini wanaleta usanii tu, kwani wana uhakika gani kwamba kutajwa namba kwenye redio na TV za Korea kaskazini kunashilia kuhamusha sleeper cells zilizopo Korea kusini ili zifanye hujuma! Uongo mtupu.
Hilo ndilo tatizo la kufanyakazi kwa ajili ya benefits za mtu mwingine. Korea kusini ni vibaraka wa marekani. sasa wanahaha na kusubiri marekani awasaidie dhidi ya ubabe wa mjukuu wa kim IL Sung
 

JustDoItNow

JF-Expert Member
Dec 3, 2013
2,970
2,000
Hata bila ya msaada wa marekani korea kusini anauwezo wa kutoa kichapo kikali kwa korea kaskazini. Korea kusini wapo juu kijeshi kuliko korea kaskazini tena kwa umbali mrefu tu. Wana silaha za kisasa zaidi, bajeti wao ya jeshi ni kubwa zaidi. Ni kati ya nchi 10 zenye uchumi imara duniani. Hata bila marekani Ikitokea vita kati ya hizi nchi mbili sidhani kama korea kaskazini anaweza ku survive labda asaidiwe na china
Duu, mkuu mi ninavyojua k. kusini anategemea sana marekani. Lakini . kasikazini anaunda vitu vyake yeye mwenyewe kwa juhudi za kuiba teck kila kona ya dunia. Imagine huyu kijana ambaye sasa ni rais wa korea kasikazini, kasomea ulaya bila kujulikana tena ni mjukuu wa kim il sung ambaye ni adui mkubwa wa ulaya.
 

masatujr1985

JF-Expert Member
Oct 27, 2011
1,981
2,000
Ndugu hawa wachapane tu. Wanapiga mikwara kila siku...si warudie tu ile vita yao ya 1970s.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom