#COVID19 Korea Kaskazini yathibitisha kifo cha kwanza cha Covid-19. Kim Jong Un avaa barakoa kwa mara ya kwanza

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Shirika la Habari la Korea Kaskazini (KCNA), leo Ijumaa Mei 13, 2022 limethibitisha kifo cha kwanza cha mgonjwa wa Covid-19, ikiwa takwimu za kwanza kutolewa rasmi siku moja baada ya nchi hiyo kuthibitisha mlipuko wa kwanza wa Covid tangu janga hilo lianze.

Watu 187,800 hivi sasa wanapatiwa matibabu wakiwa wametengwa baada ya homa isiyojulikana kusambaa Nchini kote tangu mwezi Aprili, KCNA imeripoti.

Watu 350,000 walionyesha dalili za homa hiyo, 162,200 kati yao walitibiwa. Lakini KCNA haikufafanua ni wangapi waligundulika na maambukizi ya Covid-19.

Sita walioonyesha dalili za homa hiyo walifariki, ilithibitishwa kwamba mmoja kati yao aliambukizwa aina ya kirusi cha Omicron, KCNA imesema.

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong UN Alhamisi aliamuru kufungwa kwa shughuli zote kote nchini kama njia ya kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya Virusi vya Corona yanayosababishwa na Kirusi cha Omicron ambacho kinaambukiza kwa kasi.

Kugunduliwa kwa Kirusi cha Omicron kunatokea wakati Korea Kaskazini ndiyo nchi pekee duniani ambayo haijaanzisha zoezi la kuchanja raia wake milioni 26.

Kim Jong UN ameonekana kwa mara ya kwanza akiwa amevaa barakoa kwenye mkutano na maafisa wa Serikali, jana Alhamisi Mei 12, 2022

Source: VOA News
 
Watu wamekufa sana huko. Tena wameumwa sana. Tunaposema North Korea ni taifa mfu hamwamini. Hakuna uongozi hapo. Dunia nzima ilishakumbwa na hili tatizo, wao wanasema hawana corona labda wako sayari nyingine.Ubabaishaji mkubwa sana
 
Mamlaka za Korea Kaskazini zimetangaza vifo 21 vya watu kutokana na mlipuko wa ugonjwa gonjwa wa covid 19 Nchini humo.

Nchi hiyo imewekawa kwenye lock down Ili kukabiliana na maambukizi na vifo vinavyoongezeka vya virus vya omicron.

Hata hivyo imekataa chanjo kutoka Nje ya Nchi hiyo,haifahamiki ikiwa watatengeneza chanjo yao au laa.

My take;

Hadi kiduku kukiri Hadharani kwamba kuna Covidi 19 basi ujue Hali ni mbaya 👇

Screenshot_20220514-204427.png

Screenshot_20220512-211300.png
 
Mamlaka za Korea Kaskazini zimetangaza kifo cha kwanza cha mgonjwa wa covid 19 Nchini humo..

Nchi hiyo imewekawa kwenye lock down Ili kukabiliana na maambukizi yanayoongezeka..

Hata hivyo imekataa chanjo kutoka Nje ya Nchi hiyo,haifahamiki ikiwa watatengeneza chanjo yao au laa..

My take;

Hadi kiduku kukiri Hadharani kwamba kuna Covidi 19 basi ujue Hali ni mbaya 👇

View attachment 2223026

View attachment 2223031
Kiduku uwa anasemwa mara anaumwa kuna kipindi wakasema kuwa kafa dadake ndiye anaongoza nchi lakini jamaa kumbe yu hai. Hata haya wametangaza kafa watu 21 basi wasiopenda mema washasema hali bila shaka itakuwa ni mbaya. 🤣 Binadamu bwana. Hata afrika walisema maiti zitatapakaa ila tuko tunadunda tu like nobody's business
 
Haya sasa achukue ile mikombora yake ya Intercontinental ballistic missiles kupigana na virus.
Kajamaa kamesahau kwamba sio kila vita ni ya kibinadamu.
Kwahiyo nchi ibweteke bila kukuza teknolojia yake ya kivita kisa sio kila vita ni ya kibinadamu? Ni vile wamarekani hawakutangazii majaribio ya silaha zao ila walisha fanya majaribio ya makombora kama hayo na wanaendelea kufanya.
 
Kwahiyo nchi ibweteke bila kukuza teknolojia yake ya kivita kisa sio kila vita ni ya kibinadamu? Ni vile wamarekani hawakutangazii majaribio ya silaha zao ila walisha fanya majaribio ya makombora kama hayo na wanaendelea kufanya.
Teknolojia ya uzalishaji viwandani sio teknolojia ya silaha,wanauza silaha hao? Hofu yao ni ipi hasa?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom