ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,418
- 9,599
Korea Kaskazini imelaani kitendo Cha Marekani kutaka kuiwekea Naval Blockade nchi hiyo na kukiita ni kitendo haramu.
"Maritime Blockade inayotaka kufanywa na Marekani haikubaliki kabisa kwani Korea Kaskazini ni nchi huru,..Kitendo hicho kinachotaka kufanywa na Marekani na washirika wake tutakichukulia ni uchokozi pia ni kutaka vita rasmi,shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA pamoja gazeti maalumu la chama Cha wafanyakazi nchini Korea Kaskazini Rodong Sinmun vimeeleza.
Baada ya Korea Kaskazini kurusha kombora lake la masafa marefu mwishoni mwa mwezi November,waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson alieleza kwamba "Jamii ya kimataifa inatakiwa kuchukua hatua zaidi kuongeza ulinzi wa majini ikiwemo kudhibiti bidhaa zote ziingiazo na zitokazo Korea Kaskazini".
Shauri hilo la kufunga njia zote za majini na kudhibiti kila kiingiacho na kutoka Korea Kaskazini lilitolewa na Marekani ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lakini lilipingwa na China na Urusi ambao wana kura ya Veto.Marekani iliomba Baraza hilo (UNSC) ruhusa ya kukamata meli zote za Korea Kaskazini zilizopo baharini ili kuzuia usafirishaji wa bidhaa haramu iliwemo silaha,hii ni baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio lake la bomu la Hydrogen.
Njia hii pia ilitumiwa na Marekani kuizingira Cuba baada ya ndege ya upelelezi ya Marekani U-2 kugundua uwepo wa makombora ya nyuklia ya Usovieti nchini humo.
Marekani pia ilitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuiwekea nchi hiyo vikwazo vya mafuta,lakini baadhi ya nchi zinahofu kwamba kitendo hicho kitaleta janga la kibinaadamu hasa kwa raia wa Korea Kaskazini.
SPUTNIK NEWS & EXPRESS.CO.UK