Korea Kaskazini yaonya kuhusu Naval Blockade ya Marekani,yasema ni uhalifu wa kivita

ze kokuyo

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
6,748
2,000

Korea Kaskazini imelaani kitendo Cha Marekani kutaka kuiwekea Naval Blockade nchi hiyo na kukiita ni kitendo haramu."Maritime Blockade inayotaka kufanywa na Marekani haikubaliki kabisa kwani Korea Kaskazini ni nchi huru,..Kitendo hicho kinachotaka kufanywa na Marekani na washirika wake tutakichukulia ni uchokozi pia ni kutaka vita rasmi,shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA pamoja gazeti maalumu la chama Cha wafanyakazi nchini Korea Kaskazini Rodong Sinmun vimeeleza.

Baada ya Korea Kaskazini kurusha kombora lake la masafa marefu mwishoni mwa mwezi November,waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson alieleza kwamba "Jamii ya kimataifa inatakiwa kuchukua hatua zaidi kuongeza ulinzi wa majini ikiwemo kudhibiti bidhaa zote ziingiazo na zitokazo Korea Kaskazini".

Shauri hilo la kufunga njia zote za majini na kudhibiti kila kiingiacho na kutoka Korea Kaskazini lilitolewa na Marekani ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lakini lilipingwa na China na Urusi ambao wana kura ya Veto.Marekani iliomba Baraza hilo (UNSC) ruhusa ya kukamata meli zote za Korea Kaskazini zilizopo baharini ili kuzuia usafirishaji wa bidhaa haramu iliwemo silaha,hii ni baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio lake la bomu la Hydrogen.

Njia hii pia ilitumiwa na Marekani kuizingira Cuba baada ya ndege ya upelelezi ya Marekani U-2 kugundua uwepo wa makombora ya nyuklia ya Usovieti nchini humo.

Marekani pia ilitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuiwekea nchi hiyo vikwazo vya mafuta,lakini baadhi ya nchi zinahofu kwamba kitendo hicho kitaleta janga la kibinaadamu hasa kwa raia wa Korea Kaskazini.

SPUTNIK NEWS & EXPRESS.CO.UK
 
MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
16,791
2,000
Uhalifu wa kivita (War Crime) hauwezi kufanywa na nchi bali na mtu moja. Hivyo ndiyo sheria za kimataifa zinavyosema na hata mkataba wa Roma (Rome Statute) unaoanzisha mahakama ya uhalifu wa kivita ICC unasema.

Hivyo rekebisha hapo kutoka uhalifu wa kivita (war crime) kuelekea Vita Haramu (War of Aggression)...Hivi ni vitu viwili tofauti kabisa vyenye maana tofuati zisizoringana.
 
jimmyfoxxgongo

JF-Expert Member
Jan 23, 2013
5,375

Shikamoo mwalimu
 
Kilichosemwa kwenye article ni 'hideous war Criminal act' nikaona nikiweka 'War Crime' angalau kidogo inaeleweka kwa watu wengi.
Ila Asante kwa usahihisho mkuu Malcom Lumumba
 
MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
16,791
2,000
Kilichosemwa kwenye article ni 'hideous war Criminal act' nikaona nikiweka 'War Crime' angalau kidogo inaeleweka kwa watu wengi.
Ila Asante kwa usahihisho mkuu Malcom Lumumba

Ndiyo hata mimi nimeona hivyo mkuu.
Wamekosea sana hata wao, na kama kweli Korea Kaskazini wamesema basi wamepuyanga.
"Hideous War Criminal act" au "War Crime" ni kitu kimoja kisicho na tofauti kwasababu "A war Crime is a violation of rules and Customs of war" Contrary to the Geneva Conventions of 1949 and its Additional Protocols, The Hague Rules and Other various International Agreements.

Mifano ya War Crimes sasa ni kama:
1. Killing of prisoners of wars
2. Rape
3. Torture
4. Wanton destruction of civilian properties
5. Destruction of civilian objects necessary for survival like farms, water and electronic installations
6. Any Perfidious acts

Na mengineyo mengi. Kibaya ni kwamba haya makosa ili yaweze kuwa War Crimes ni lazima yafanywe na mtu "Natural Person" na siyo "Artificial Entity" kama nchi: Kikubwa ni kwamba ili kuwe na War Crime ni lazima kuwe na Vita lakini hapo ni mikwara na vita hakuna. Ndiyo maana basi nikasema kama wanaiita hiyo Pacific Blockade "Hideous War Criminal act" basi ni majuha sana na kesho wanaweza sema vile vikwazo (Economic Sanctions) navyo ni "Hideous War Criminal act"
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom