Korea Kaskazini yamuua afisa baada ya kushindwa mkutano wa Hanoi

Msaliti hayo ndio malipo yake, hata hapa kwetu tuna, dawa ni hiyo tu.

Safi sana Kim Jong Un
 
Vyombo vya habari vya Korea Kusini hii leo vimeripoti kwamba Korea Kaskazini imemuua mjumbe wake maalumu kwa ajili ya Marekani Kim Hyok Chol kufuatia kushindwa kwa mkutano wa pili wa kilele kati ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na rais Donald Trump.
Gazeti la Chosun Ilbo limeandika Chol aliyeuandaa mkutano huo wa Hanoi na kumsindikiza Kim kwenye treni yake binafsi ameuawa kwa kupigwa risasi kwa kile kinachotajwa kumsaliti kiongozi huyo wa juu baada ya kufanikiwa kuishawishi Marekani wakati wa majadiliano ya kabla ya mkutano huo wa kilele.
Gazeti hilo lililonukuu chanzo ambacho hakikutambulishwa limesema Chol, aliuawa mwezi Machi, katika uwanja wa ndege wa Mirim pamoja na maafisa wanne waandamizi wa wizara ya mambo ya nje baada ya uchunguzi.
Mkalimani wa Kim kwenye Umoja wa Mataifa naye ametiwa kizuizini baada ya kufanya makosa kwenye mkutano huo wa kilele.
Mmmh...sidhani. huu utakua ukatili su mtindo gsni wa uongozi? Huenda ni propaganda tu za wamarekani kuonesha dogo ni shetani.
 
Kim kushindwa kupata alichotaka unakua ni usaliti wa negotiators... This is insane.....!!!
Wewe ndezi huwezijua kitu, hizo nchi ukijichanganya Kama mfanyavyo haha ni kupewa safari ya jumla, hakuna ukuwadi huko, ukuwadi fanyeni hapa bongo
 
Nk wapo smart Sana, Kila marekani anachofanya kuwadhofisha wao wapo one step ahead. Ukute Wakati wa mazungumzo CIA somehow waliwatag na highly sophisticated GPS trackers na walipo fika Nk wakagundua nakuzideactivate Sasa wamarekani wanahaha kujua walipo na wanawasiwasi NK kagundua hiyo technologia hivyo chombo hicho Cha SK kina tumia propaganda ya namna hiyo kuwasaidia CIA kufanya intelligent guess 😄😄
 
Hao jamaa ni ndugu na wachina

Kuuwa Kwao sio tatizo

Ndio maana nawaogopa sana Wachina, hawaheshimu uhai, demokrasia wa utu wa mwanadamu
Ufyatukaji wa kuongelea haki na demokrasia ni janga .
 
Pumbavu kbx yaani mungu atumie gharama kubwa kuumba kiumbe chake alafu mwanadamu mwenye tamaa ya madaraka akinyonge kirahisi,,Kim atajuta maana dunia inamtizama,,,Tz tubaki maskini tu hatuhitaji mtu wa kumwaga damu za wananchi ili tufikie maendeleo huo upuuz uishie huko jehanam ya duniani N.korea, china, Russia na kwingineko
 
Screenshot_2019-06-03 'Purged' Kim Yong Chol's reappearance punches hole in sensationalist story.png
 
Back
Top Bottom