Korea Kaskazini yamuita 'mjinga' Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Afisa wa cheo cha juu wa Korea Kaskazini amemlaumu Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence kwa kuwa "mjinga" na kuonya kuwa kutakuwa na maonyeshano ya ubabe wa nyuklia ikiwa mazungumzo yatafeli.

Choe Son-hui alisema Pyongyang haitaweza kuibembeleza Marekani kwa mazungumzo.
Siku za hivi karibuni pande hizo mbili zimeonya kuwa mkutano wa Juni 12 unaweza kuharishwa au kufutwa kabisa.

Korea Kaskazini ilisema itafikiria tena iwapo itahudhuria mkutano ikiwa Marekani itaendelea kusisitiza kuwa iachane na mpango wa silaha za nyuklia. Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumanne alisema Korea Kaskazini ndiyo ingetimiza masharti ya kufanyika kwa mazungumzo hayo.

Choe Son-hui amehusika kwenye mazungumzo mara kadha na Marekani kwa karibu miaka kumi iliyopita.

Alimuita Mike Pence mjinga kwa kuifananisha Korea Kaskazini, taifa la nyuklia na Libya, ambayo anasema ilikuwa na vifaa vichache tu ilivyokuwa ikicheza navyo.

"Kama mtu ambaye nimehusika kwenye masuala ya Marekani, siwezi kuficha mshangao wangu kufuatia matamshi kama hayo ya kijinga yanayotoka kinywani mwa Makamu wa Rais wa Marekani," alisema.

Bi Choe alisema Pyongyang haikuwa inabembeleza kufanyika mazungumzo. "Ikiwa Marekani itakutana nasi au kutukabili kinyuklia inafuatia na uamuzi na tabia za Marekani."

Mshauri wa masuala ya ulinzi wa Marekani John Bolton naye aliikasirisha Korea Kaskazini wiki iliyopita kwa kusema kuwa utatumiwa mfumo wa Libya katika kuondoa zana za nyuklia.



BBC
 
“Whether the U.S. will meet us at a meeting room or encounter us at nuclear-to-nuclear showdown is entirely dependent upon the decision. . . of the U.S.”

Hiyo statement ni noma kabisa, imesemwa leo na kiongozi wa juu wa NORTH KOREA.

Katika wording and intepretation inaweza maanisha yafuatayo:

a. mkutano wao na U.S siyo wa lazima kwao.

b. Bado wanaweza endelea kuishi na vikwazo ila tu walitaka ahueni ya muda mchache kwa kujifanyisha kutaka suluhisho ili wajipange upya jinsi ya kuishi na vikwazo lukuki vya trump (walitafuta diplomatic break ili kupunguza mtifuano wao na Trump).

c. wako tayari kwa lolote dhidi ya Marekani hata kwa njia ya vita vya kijeshi.

d. wanataka Trump apunguze masharti iwapo watakutana kuzungumza, hasa hasa awatambue kama nchi ya kinyuklia.

e. wao ni nchi ya kinyuklia, hivyo mpango wao siyo kuangamiza nyuklia zote bali ni kupunguza tu uzalishaji wa silaha hizo.

f. wao siyo pande dhaifu kwenye mazungumzo tarajiwa.

g. mengineyo
 
Hivi kuharibu maeneo ya kujaribia siraha za nyuklia wanafanya lini?, au shughuli hiyo nayo imeahirishwa?
 
Back
Top Bottom