Korea kaskazini yaionya Marekani kuhusu kusogelea pwani yake

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945
upload_2017-4-11_15-12-12.jpeg

Wizara ya Mambo ya nje ya Korea Kaskazini imesema haitasita kujihami na vitendo vya Kamandi ya majini ya Majeshi ya Marekani kuhusu kusogeza vifaa vya kijeshi na majeshi yao karibu na pwani ya Korea" Hatutaomba amani katika vitendo hivyo badala yake tutajihami kwa uvamizi huo usio na maana'

Wizara ya mambo ya nje ya Korea katika taarifa yake kituo cha habari cha Korea yaani KCNA, Aidha taarifa za Mkuu wa Majeshi ya nchi hiyo Vice Marshal Ri Myong-su zimesema hawatasita kuifuta Marekani bila kuacha alama yoyote kama wataendeleza uchokozi watatumia silaha za masafa marefu kujihami na uvamizi wowote katika pwani hiyo.

upload_2017-4-11_15-13-44.png
 
View attachment 494251

Wizara ya Mambo ya nje ya Korea Kaskazini imesema haitasita kujihami na vitendo vya Kamandi ya majini ya Majeshi ya Marekani kuhusu kusogeza vifaa vya kijeshi na majeshi yao karibu na pwani ya Korea" Hatutaomba amani katika vitendo hivyo badala yake tutajihami kwa uvamizi huo usio na maana' Wizara ya mambo ya nje ya Korea katika taarifa yake kituo cha habari cha KCNA, Aidha taarifa za Mkuu wa Mjeshi ya nchi hiyo vice Marshal Ri Myong-su zimesema hawatasita kuifuta Marekani bila kuacha alama yoyote kama wataendeleza uchokozi watatumia silaha za masafa marefu kujihami na uvamizi wowote katika pwani yake.



View attachment 494252
Mikwala tu kama ya yule msemaji wa serikali ya Saddam Hussein!
 
Hivi Wakuu mwaka huu kuna nini?? daah kila sehemu ni vitisho kule, Syria tayari zinaumana pale Korea Kaskazini moshi unafuka tayari kwaajili ya kuwaka, daha hapa na pale aaah Nabaki Afrika tu
 
Hivi N. Korea ni kweli inaweza kuifanyizia US au ni basi tu wanatishia waone

Coz huwa naamini US ina silaha kali mno na za kisasa!

Ama zile silaha huwa ni za kwenye series na Movies zao tu!
USA nao wanaelemewa na shida za kutosha.
Uwezo wa kupiga maadui zao kimsingi haupo. Nchi za magharibi wanatumia media zao kuelezea mazuri ya magharibi ilihali mabaya wanayaficha.

Kama US wangekuwa na uwezo wa kupiga Russia, Iran, au N.Korea, wasingesita kufanya hivyo.

Kwa sasa inabidi wajikombe kwenye mazungumzo pamoja na kutumia mashushushu pia mbinu chafu ili kuwadhorotesha maadui zao lakini kwa vita vya moja kwa moja kwao ni jambo gumu.
 
Wafyatue tu hiyo mikombola ya masafa.

Marekani wana kiherehere mno

Wamerikani wanacho sahau Korea Kaskazini siyo Iraq,Libya au Afghanistan - wakifanya ujinga wa kujaribu kuishambulia Korea Kasikazini, Korea Kusini itaharibiwa vibaya sana na Marekani ikijitia kuwaleta askali wa miguu watapata cha mtema kuni, Korea Kaskazini hawana mchezo hata kidogo na watapata usaidizi wa kijeshi wa kificho kutoka China na Urusi - ya vita ya 1950-53 yatajirudia tena na Uncle SAM atapata fundisho la mwaka - manake Wachina na Warusi watatumia mwanya huo kuwapa wanajeshi wa Korea Kaskazini silaha kali za kuhangamiza makombora ya THAAD yanayo tarajiwa kuwekwa na Marekani Korea Kusini, makombola hayo ni tishio kwa mataifa ya China na Urusi - Trump anapashwa kuwa makini sana anapo taka ku-deal na Kiongozi wa Korea Kaskazini watumie diplomasia zaidi kuliko ubabe, wakipuuzia watapata wakati mguma sana kuliko wa vita ya Viet Nam.
 
Ndo USA weshasogeza manuari yeye kama anajiamini afyatue hizo nyuklia zake ndo atajua laki si pesa

Kim ana haja gani ya kuvurumishia makombola Meli ya Merikani bila ya kuchokozwa, Uncle SAM akikosea step ndiyo watapata fundisho la mwaka nakwambia, huu mwaka wa 16 Wamerikani bado wanaendelea kutolewa kamasi na Wataleban huko Afghanistani,je,Korea Kaskazini si ndiyo itakuwa balaa zaidi kwa Wamarekani - yetu macho.
 
Back
Top Bottom