Korea Kaskazini yafanya zoezi la kushambulia makao ya rais wa Korea Kusini

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
160318081130_kim_jong_un_640x360_reuters_nocredit.jpg

Korea Kaskazini imesema kuwa imetekeleza mazoezi ya kuyashambulia makaazi ya rais wa Korea Kusini.
Zoezi hilo lilisimamiwa na rais wa taifa hilo Kim Jong-un,kulingana na chombo cha habari cha KCNA ambaye alilitaka jeshi kujiandaaa kuivamia na kuiharibu serikali ya kusini.

Ni hatua ya hivi karibuni ya ishara za hasira za Pyongyang.
Rais wa Korea Kusini Park Geun-Hye ameliagiza jeshi lake kuwa katika hali ya tahadhari.
Lakini alisema siku ya Alhamisi kwamba uchochezi utasababisha maafa makubwa kwa serikali na uongozi wa Korea Kaskazini.

Korea Kaskazini imekuwa ikijibu hatua ya Umoja wa Mataifa ya kuiwekea vikwazo kufuatia majaribio ya makombora yake ya masafa marefu ya kinyuklia.
Pyongyang vile vile imekasirishwa na mazoezi ya pamoja kati ya serikali ya Korea Kusini na Marekani kusini mwa mpaka wake.

Kama inavyojulikana kwa vitisho vyake ,ripoti hiyo iliotolewa na KCNA ilitishia kuilipua nyumba hiyo ya rais wa Korea Kusini inayojuliakana kama Blue House hadi kuwa jivu.
Makombora yalirushwa kama umeme na kuanguka katika maeneo yanayolengwa ikiwemo nyumba hiyo ya rais wa Korea Kusini.

Haijulikani ni lini zoezi hilo lilifanywa,lakini ripoti hiyo ilionya mwisho mbaya wa rais Park.
Makaazi hayo ya Blue House yalishambuliwa na makomando wa Korea Kaskazini mwaka 1968.
Hatahivyo jaribio la kutaka kumuua aliyekuwa rais Park Chung-hee halikufanikiwa,raia saba wa Korea Kusini pamoja na makomando hao 31 kutoka Korea Kaskazini waliuawa.

Source: BBC
 
Ahahahahaaaaa.....hakuna jipya!

Ni kelele zilezile za kila siku.

Hivi Samsung S7 Edge unaweza kuipata huko Pyongyang?

:D:D:D:D:D:D:D:D:D:D:D:D.

Jipya litajitokeza pale watakapofanya kweli. Wako baadhi humu JF wanaipuuza Korea Kaskazini. Lakini nawathibitishia kuwa Marekani na Korea Kusini kamwe hawaipuuzi Korea kaskazini. Ndiyo maana Marekani ina askari wapatao 30,000 huko korea Kusini na ambao wako tayari kwa vita.

Mazoezi ya kijeshi ya hivi karibuni kati ya Marekani na South Korea yaliyofanywa mpakani mwa South Korea na North Korea ilikuwa ni kujiweka sawa kwa lolote kama vita vitatokea. Korea ya kaskazini siyo ya kupuuzwa hata kidogo. Licha ya vikwazo vya kiuchumi North korea ina teknolojia inayoweza kuisaidia wakati wa mapambano. Miezi kadhaa iliyopita iliweza ku-hack hata mitandao ya Marekani. North Korea ina askari wapatao milioni moja (1,000,000) na ambao laki saba (700,000) wako msitari mbele wakikabiliana na South Korea kwa formation mbalimbali. Licha ya askari hao milioni moja lakini ina askari kadhaa wa akiba kati ya milioni 2 na 4. Yaani muda wote jeshi la North Korea limekaa mkao wa vita, of course vivyo hivyo South korea yenye jumla ya askari laki tano (500,000) hivi.

North Korea siyo ya kuchezea ingawa vyombo vya habari vya magharibi huwa vinajenga picha kuonyesha kuwa North Korea si lolote ingawa kiuhalisia wao wenyewe Marekani na nchi za magharibi huiogopa North Korea.
 
Hakuna lolote!

North Korea hana ubavu wa kupigana na jirani yake South Korea.

Hizo kelele zao wengine tushazizoea na kusema ukweli huwa zinachekesha sana.

Hususan zikiwa zinatangazwa na kile kibibi. Kibibi huwa kinajikakamua utadhani kimebanwa na haja ya mabungo:D.

Ushauri wangu kwako na wengine wenye mawazo kama yako ni kuwa: YOU SHOULD READ BETWEEN THE LINES TAARIFA AU NEWS ZOTE ZIWE ZA NCHI ZA MAGHARIBI AU ZA RUSSIA AU NORTH KOREA NA KADHALIKA. Hicho 'kibibi' mimi nakipenda kwani kinanikumbusha picha za akina JUMONG na KING GWANGAETO
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Ushauri wangu kwako na wengine wenye mawazo kama yako ni kuwa: YOU SHOULD READ BETWEEN THE LINES TAARIFA AU NEWS ZOTE ZIWE ZA NCHI ZA MAGHARIBI AU ZA RUSSIA AU NORTH KOREA NA KADHALIKA.

Sina hata haja ya kufanya hivyo.

Nachojua ni North Korea ni mbwa koko tu.

Ni watu wa kubweka hovyo hovyo tena kwa sauti kubwa lakini ikija kwenye kufanya kweli, hakuna kitu.
 
Duh, aisee, wewe dogo una msimamo, wewe ni ngangari kinoma kama mnavyosema wenyewe
 
Sina hata haja ya kufanya hivyo.

Nachojua ni North Korea ni mbwa koko tu.

Ni watu wa kubweka hovyo hovyo tena kwa sauti kubwa lakini ikija kwenye kufanya kweli, hakuna kitu.
walishazamisha meli ya korea kusini na hakuna mtu alikohoa,
washashambulia kwa mizinga kisiwa cha korea kusini hakuna mtu alikohoa.
Juzi hapa wameshambulia kwa mizinga misipika ya korea kusini,
mbona korea ya kusini hajibu?
 
Hebu weka sources zinazoonyesha ni lini na wapi hayo matukio yalitokea na kuwa South Korea haikufanya lolote.
 
Hakuna lolote!

North Korea hana ubavu wa kupigana na jirani yake South Korea.

Hizo kelele zao wengine tushazizoea na kusema ukweli huwa zinachekesha sana.

Hususan zikiwa zinatangazwa na kile kibibi. Kibibi huwa kinajikakamua utadhani kimebanwa na haja ya mabungo:D.

hahaha Shimitaaaa pyeaaaa
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Jipya litajitokeza pale watakapofanya kweli. Wako baadhi humu JF wanaipuuza Korea Kaskazini. Lakini nawathibitishia kuwa Marekani na Korea Kusini kamwe hawaipuuzi Korea kaskazini. Ndiyo maana Marekani ina askari wapatao 30,000 huko korea Kusini na ambao wako tayari kwa vita.

Mazoezi ya kijeshi ya hivi karibuni kati ya Marekani na South Korea yaliyofanywa mpakani mwa South Korea na North Korea ilikuwa ni kujiweka sawa kwa lolote kama vita vitatokea. Korea ya kaskazini siyo ya kupuuzwa hata kidogo. Licha ya vikwazo vya kiuchumi North korea ina teknolojia inayoweza kuisaidia wakati wa mapambano. Miezi kadhaa iliyopita iliweza ku-hack hata mitandao ya Marekani. North Korea ina askari wapatao milioni moja (1,000,000) na ambao laki saba (700,000) wako msitari mbele wakikabiliana na South Korea kwa formation mbalimbali. Licha ya askari hao milioni moja lakini ina askari kadhaa wa akiba kati ya milioni 2 na 4. Yaani muda wote jeshi la North Korea limekaa mkao wa vita, of course vivyo hivyo South korea yenye jumla ya askari laki tano (500,000) hivi.

North Korea siyo ya kuchezea ingawa vyombo vya habari vya magharibi huwa vinajenga picha kuonyesha kuwa North Korea si lolote ingawa kiuhalisia wao wenyewe Marekani na nchi za magharibi huiogopa North Korea.
Unatuthibitishia!!! Haya mkuu.
 
Hakuna lolote!

North Korea hana ubavu wa kupigana na jirani yake South Korea.

Hizo kelele zao wengine tushazizoea na kusema ukweli huwa zinachekesha sana.

Hususan zikiwa zinatangazwa na kile kibibi. Kibibi huwa kinajikakamua utadhani kimebanwa na haja ya mabungo:D.

Mkuu unaelewa hayo madudu ya bibi?
 
Hizi Korea mbili zina ishi kwa propaganda sana tena nafikiri ndio eneo pekee duniani watu wanaoishi kwa uhasama na propaganda za hali ya juu tangu kuisha vita baridi baina ya ujamaa na ubepari.

Huwenda siku moja wakazichapa tena. Korean war ya 1950-1953 hakukua na mshindi wakati ule naona hizi chokochoko na uchokozi baina yao unaweza leta vita ambayo kwa karne hii itakuwa mbaya sana kutokana na maenendeleo makubwa ya kisayansi yalioleta silaha hatari za nyuklia. Siku zote vita haianzi ghafla bali inaanza kidogo kidogo kwa njia ya kujibishana maneno (propaganda ) na mwisho vita kamili , ingawa hizi propaganda zimesha zoeleka sasa ila UN na mataifa makubwa yasikae kimya tuu bali watafute namna ya kutuliza uhasama kwa njia za kidiplomasia badala. ya kusubiri mbabe. ajulikane. kwa njia. ya vita.
 
Hebu weka sources zinazoonyesha ni lini na wapi hayo matukio yalitokea na kuwa South Korea haikufanya lolote.
aah unataka kunipa kazi tena hapa mkuu,,we niamini tu korea ya kasikazini miaka ya karibuni washazamisha sub ya korea kusini na hakuna kitu walimfanya
 
Sina hata haja ya kufanya hivyo.

Nachojua ni North Korea ni mbwa koko tu.

Ni watu wa kubweka hovyo hovyo tena kwa sauti kubwa lakini ikija kwenye kufanya kweli, hakuna kitu.
mbwa koko.. mbona baba yenu US na washirika wake wanakosa usingizi kwa sababu yake?

Unahitaji muda zaidi kuweza kuzijua mbinu za adui yako
 
Back
Top Bottom