Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,502
- 22,355
Nchi ya Korea Kaskazini asubuhi hii wamefanya jaribio la bomu la nyuklia katika milima ya Punggye-ri sehemu ambayo huwa wanafanyia majaribio hayo.
Safari hii nchi hiyo imejaribu bomu la hydrogen ambako lilisababisha tetemeko dogo la ardhi ambalo lilitambaa kiasi cha kilomita 49 sawa na maili 30 kutokea Korea Kusini.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un
Kituo cha utafiti wa matetemeko ya ardhi cha Marekani kimetoa taarifa ya kuonyesha kwamba tetemeko hilo likikuwa na upana wa kiasi cha 5.1.
Nchi za Korea Kusini na Japan wanafanya mawasiliano ili kupata taarifa rasmi kuhusiana na eneo hasa la tetemeko au Epicentre kufahamu kiasi cha athari zilizopo.
Nchi ya Korea Kaskazini imekuwa na tabia ya kujiamulia yenyewe ni lini na wakati gani wanaweza kufanya majaribio yao ya bomu ya nyuklia bila kutoa tahadhari na kuja kutoa baada ya tukio, jambo linalowakera nchi majirani za Korea Kusini na Japan.
Baada ya kufanya jaribio hilo viongozi wa Pyongyang waliamuru taarifa itolewe kwenye Jumatano asubuhi kuufahamisha ulimwengu kwamba majaribio yamefanywa na yamekwenda kama ilivyopangwa na yamekuwa ni ya mafanikio.
Kifaa hicho cha hydrogen au kwa jina lingine "thermonuclear device" kinatumia miali mikali ya moto inayoundwa kwa mithili ya mnyororo kutengeneza mlipuko mkubwa zaidi ya milipuko inayotengenezwa kwa kutumia Uranium au Plutonium.
Jaribio hili ni la nne kufanywa na nchi hiyo likiwa ni la tatu kufanywa raisi Barak Obama akiwa madarakani.
Majaribio mengine ambayo yamefanywa ni Mwezi October 2006, Mei 25 2009, February 12 2013, na hili la leo tarehe 6 January 2016.
Bado nchi za magharibi na Marekani hazijatoa matamko katika kujibu taarifa hiyo ya Korea Kaskazini.

Last edited: