Korea Kaskazini: Ahukumiwa kunyongwa kwa kutazama na kusambaza nakala za series ya 'Squid Game'

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,545
Mwanaume mmoja raia wa Korea Kaskazini ambae utambulisho wake haujawekwa wazi amehukumiwa kifo kwa kutazama na kusambaza nakala za series maarufu kutoka Netflix 'Squid Game'.

Inasemekana hukumu ya kunyongwa kwake hadi kufa ia tatekelezwa na kikosi maalumu cha kurusha risasi.
Mbali mwanaume huyo watu wengine pia wamehukumiwa kifungo cha maisha jela na kufanya kazi ngumu kwa kutazama shoo hiyo kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa Radio Free Asia iliripoti kwamba 'msafirishaji' huyo alipata nakala ya kipindi hicho nchini China na kuirejesha Korea Kaskazini na kudaiwa kuuza nakala za onyesho hilo kwenye flash.

Squid Game iliyoongozwa na muongozaji Hwang Dong-hyuk, imejizolea umaarufu mkubwa duniani na kuweka rekodi ya kipekee katika mtandao wa Netflix tangu ilipo-onyeshwa kwa mara ya kwanza mwezi Septemba 2021.
 
mkuu kweli sisi tumelogwa yaan unaona korea wanapelekwa puta wakati hata huku sisi kuna kundi la wahuni linatupekeka puta waafrica ndo tusiseme
Mkuu sikatai kwamba sisi tuna matatizo na CCM yetu la hasha,ila Kuna muda tunazidiana shida ujue angalau huku tunauwezo kumsagia kunguni Bi mkubwa huku nyuma ya keyboards na akapata wenge na kuchange maamuzi kama alikua anaenda wrong, sasa huko north Korea hao jamaa zetu hata access za internet hawana tv channel wanazo mbili tu na kuangalia mpaka jioni, imagine aiseee!
 
mkuu sikatai kwamba sisi tuna matatizo na CCM yetu la hasha,ila Kuna muda tunazidiana shida ujue angalau huku tunauwezo kumsagia kunguni Bi mkubwa huku nyuma ya keyboards na akapata wenge na kuchange maamuzi kama alikua anaenda wrong,Sasa huko north Korea hao jamaa zetu hata access za internet hawana tv channel wanazo mbili tu na kuangalia mpaka jioni,imagine aiseee!
Sema kumzingua kiduku si mchezo maana jamaaa kajipanga ww mpaka marekani yenyewe inanywea akipiga mkwara
 
Western Propaganda tu

Marekani na nchi za magharibi zina namna yao ya kuwa portray viongozi wa nchi zenye uadui nao
Hio story ni ya kutunga
 
mkuu sikatai kwamba sisi tuna matatizo na CCM yetu la hasha,ila Kuna muda tunazidiana shida ujue angalau huku tunauwezo kumsagia kunguni Bi mkubwa huku nyuma ya keyboards na akapata wenge na kuchange maamuzi kama alikua anaenda wrong,Sasa huko north Korea hao jamaa zetu hata access za internet hawana tv channel wanazo mbili tu na kuangalia mpaka jioni,imagine aiseee!
Udikteta wa Korea Kaskazini kwa maoni yangu utakuwa ndio mbaya sana duniani kwa sasa katika karne hii ya 21. Huyo anayelinganisha changamoto za hao raia wa Kiduku na huku kwetu, namshauri ajitahidi kusoma taarifa za taifa hilo, kwa bidii kupitia vyanzo mbalimbali, halafu arudi hapa aje atupe ushuhuda.
 
Kwani wanatofauti gani na sisi watz?
Huenda hata sisi kuna wanaotushangaa tunavyozoea shida haraka kama za tozo, mgao wa umeme na maji.
wewe jamaa Ile Nchi ni Soo Aisee Yaani ni Mali Halali ya familia ya Kim jong UN anafanya anachotaka Kwa wakati wowote yaani akiamka na akitangaza watu wote hakuna kula hakuna mtu anapinga ni amri Moja,akisema wote mnashinda mnalia na sharti utoe machozi yakupasa ufanye,wale wapo kwenye deep dictatorship
Wanatia huruma sana wale watu,wanahitaji seeker wa kuwatoa pale Hali ni Mbaya sana!
Wanashindwa hata ikimbia Nchi maana ni kama imepigwa pin no escape anywhere!
 
Shida ya huyo Bwana mabangi ,nikufikiri kupitia hizo series wakorea watafunguka vichwa na kumbadilikia
 
wewe jamaa Ile Nchi ni Soo Aisee Yaani ni Mali Halali ya familia ya Kim jong UN anafanya anachotaka Kwa wakati wowote yaani akiamka na akitangaza watu wote hakuna kula hakuna mtu anapinga ni amri Moja,akisema wote mnashinda mnalia na sharti utoe machozi yakupasa ufanye,wale wapo kwenye deep dictatorship
Wanatia huruma sana wale watu,wanahitaji seeker wa kuwatoa pale Hali ni Mbaya sana!
Wanashindwa hata ikimbia Nchi maana ni kama imepigwa pin no escape anywhere!
Nchi ya hovyo sana
 
Back
Top Bottom